Monday, January 2, 2012

NIMEONA TUUANZA MWAKA MPYA 2012! KWA MTINDO HUU!!!!!!

Mwaka mpya huwa ni wakati wa malengo mapya na mwelekeo mpya. Kila binadamu ana malengo yake hapa duniani. Mimi nina malengo yangu na wewe pia una yako. Kila kukicha huwa tunajitahidi kuyatimiza. Tunapasua vichwa kujaribu kuyatimiza malengo yetu . Ndio maisha.

Bila shaka na wewe umeshaketi chini na kujiuliza swali hili:- ninataka kutimiza malengo gani mwaka huu? Je? ni kurudi shule kuongeza ujuzi? Je? ni kuoa au kuolewa? Je? ni kujitolea zaidi katika jamii yako/yangu? Je? ni kutunza na kulinda mazingira? Msururu wa malengo unaweza kuwa mkubwa. Kama kutimiza malengo fulani fulani ndio mkakati wako wa mwaka huu basi zingatia ushauri ufuatao:-

Weka malengo yanayotimizika au yenye uhalisia-Jiangalie ulipo, angalia vitendea kazi ulivyonavyo, tazama kwa makini ujuzi ulionao kisha yapime vizuri malengo yako.

Jiulize swali au maswali:- Nitayatimizaje malengo yangu? ukishafanya hivyo jiwekee utaratibu wa jinsi ya kutimiza malengo yako. Yaani mpango wa utekelezaji wako.

Nenda utaratibu -Mwaka ndio kwanza umeanza, yakaribiribie malengo yako kwa mwendo wa taratibu. Usiwe na haraka wala pupa. Si unakumbuka kwamba mambo mazuri hayataki haraka?

Usiogope kurekebisha malengo-Kadri mwaka unavyoanza kusonga mbele, unaweza kugundua kwamba huenda kutimiza malengo fulani. Hiyo inawezekana kutokea kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, kiafya au kibinafsi. Usihofu kurekebisha malengo yako.

Usiogope kushindwa-Yawezekana kabisa ukashindwa kutimiza malengo fulani fulani. Kwa sababu zaweza kuwa kama hizo nilizozitaja hapo juu, usiogope. Cha muhimu ni kujaribu na kujaribu na kujaribu. Jitahidi kadri unavyoweza, nina uhakika ukijaribu utafanikiwa kwa hiyo mwisho wa siku hadithi ya kushindwa wala haitokuwepo.

La muhimu ni kuomba msaada inapobidi yapo mambo mengine ambayo hutaweza kuyatekeleza peke yako. Hilo linapotokea, usiwe mgumu kuomba msaada.
Kwa mara nyingine tena nawatakieni wasomaji wa blogya MAISHA NA MAFANIKIO kila la kheri katika mwaka huu wa 2012.

8 comments:

ray njau said...

Kwa wadau na familia ya kibaraza cha maisha na mafanikio naona pazia la mwaka 2012 limefunguliwa.Karibuni sana!!

chib said...

Swadakta!
Mipango tunapanga, lakini inakuja badilika :-)

Faith S Hilary said...

Mmmh, si ndio mambo ya "new year's resolutions?"...sijui inakuwaje lakini watu wengi wakiweka hiyo mipango kwa mwaka mpya, siku zote hawatizimi au hata mwezi wa pili haufiki basi wanashindwa. Nawatakieni heri nyote mlioweka "resolutions" kwa mwaka huu lakini upande wangu, I take life as it is :-)

Mzee wa Changamoto said...

Mimi RESOLUTION yangu ni kuRESOLUTE resolutions zote zilizoRESOLUTE-iwa na RESOLUTORS ili zikiRESOLUTE vizuri, ziniRESOLUTE-ishe mwakani
Happy New Year (even though the word NEW is TOO OLD)

Mija Shija Sayi said...

Hilo la kuomba msaada ni la muhimu sana kama unataka kufanikisha mambo yako, ila sababu ya ubinafsi watu tumekuwahatufiki mbali...tunaogopa kuomba msaada kwa vile tunadhani tutaonekana hatujui...

Heri ya mwaka mpya kwenu wote.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

aksante kwa ujumbe murua. Happy New Year

sam mbogo said...

Sijuwi hata niseme nini !!!? nawatakia ninyi wote mwaka mpya mwema, namipango yenu yooooote iwe safi. WEKELEA KANYAU. kaka s

Rachel Siwa said...

Baraka kwa wote hapa, kheri na mafaniko!Mungu ni Pendo....