Saturday, January 14, 2012

NAPENDA KUWATAKIA WOTE MWISHO WA JUMA NA MUSIKI HUU HAYA TUFURAHI PAMOJA


NA UJUMBE WA LEO NI :- UKITAKA KUJUA MENGI BASI NI KUULIZA NDIO DAWA YAKE. MWISHO WA JUMA MWEMA NDUGU ZANGUNI. TUSISAHAU KUWAKUMBUKA TUWAPENDAO PIA HATA WALE TUWACHUKIAO KAMA WAPO.!!!

5 comments:

sam mbogo said...

Yasinta, leo umenifurahisha saaaaaaana,kwa kuniwekea/kutuwekea, nguli wa muziki wa kiasili,marehemu,mwalimu wangu,aliye fundisha chuo cha sanaa Bagamoyo,Dakitari Hukwe Zawose(apumuzike kwa amani). Mwaka 2002,niliweza kufanya manesho nafamilia ya Mwal,Zawose, huko Scotland, kwa muda wa miezi miwili . Familia hii imebarikiwa vipaji . pia shukrani kwa ujumbe wa leo, ni kweli usipo uliza hutajuwa maana,hutajuwa kitu. nahuu ujumbe ni muhimu sana kwa akina sisi tunaojifanya tuna juwa ili kuficha uthaifu wetu. je na usemi huu usemao" kuuliza si ujinga" je unaukweli ndani yake? wakati wa uhai wa baba yangu niliwahi kumsikia akisea kuuliza ni ujinga! nimekuwa natafakari juu ya usemi huo wa baba yangu,ambaye kwa taaluma alikuwa mwalimu,kuna mengi nime ya gundua katika usemii huu hasa katika hoja ya baba yangu. kaka s.

Baraka Chibiriti said...

Asante sana Dada yasinta, nawe pia Weekend njema sana na Familia yako yote.
Pia umenifurahisha sana, kwa mziki huu mzuri wa nyumbani kabisa, umenirudisha kwetu kabisa Ugogoni, nimekumbuka mengi leo. Asante!

EDNA said...

kwako pia mdada na familia yako.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! unajua mimi napenda sana mambo ya asili kuanzia mziki, chakula, mavazi na bila kuasahau uasili yangu. Nimemkumbuka Zawose leo kwani nilishawahi kuonana naye ana kwa ana alipofika hapa miaka ya 1990...nafurahi kusikia kuwa umefurahi saaaaana ..
Kaka Baraka! nafurahi kama umekumbuka nyumbani na nilijua tu utasema na utakumbuka mengi...Ahsante
Edna ahsante ndugu wangu!

sam mbogo said...

Haswa ndo yeye mwalimu,Dakitari, hiyo miaka ya 90 ndo wakati niko mwaka wapil chuo cha sanaa bagamoyo,wakati huo walimu walikuwa na safari nyingi tu za sweden, kumbe miaka ya 90 ulikuwa sweden utakuwa umekaaa sana,hakika wewe ni mtanzania halisi kwa kuzaliwa endelea hivyohivyo mtu kwao. kaka s