Thursday, April 3, 2014

UKIFIKA/PITA SONGEA USIKOSE KUPITIA HAPA ILI KUPATA CHAKULA CHA HARAKA NA KINYWAJI KIDOGO....SONGEA/LIZABONI!!!

Sehemu hii ipo Songea katika mtaa wa LIZABONI kwa wale wasio wenyeji wa Songea...Mara nyingi sana hapa huwa ni kituo chetu kupata nyama ya Nguruwe/kitimoto..mtanisamehe kwa wale waiotumia/kula mnyama huyu.
Kitu kingine kilichonifanya kuweka hii picha ni kwamba nimekumbuka enzi zileeee mtu unaweza kuwa safarini na usione sehemu ya kula kunywa ndo kabisa kama usipokuwa na chakula  mwenyewe au kupita kwa ndugu na kupata chakula kidogo. Nakumbuka nilipokuwa nasafiri  enzi hizo mama na baba walikuwa wananiandalia karanga zilizopondwa na chumvi(wangoni tunaita CHIMBONDI) Basi ukila hii inabidi uwe karibu na mto ili kupata maji ya kutelemshia. Leo vyakula vya haraka kila mji(Fasta food) Sijui ipi ni bora? Je nawe unakumbuka  kitu kama hiki au tofauti? 

7 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yacinta bila shaka hapa unatochukoza maustaadhi na mashariff tukukalie itikafu na kukusomea al badir bure. Si kila kilaji ni mlo na si kila kanywaji ni kinywaji ati. Tuombe msamaha mapema kabla hatujapiga mtu zongo. Kwa wanyasa ni simpo ukigusa maji anatokea mamba anakumalizia kazi yako. Kwa mashehe sijui watatumia method gani hapa.

Yasinta Ngonyani said...

Mwal. Mhango kakangu! Hii ndio maana nikaanza kuomba RADHI. Halafu nilijua tu kakangu utasema hivyo..Samahani tena naona nastahili bakora hapa...LOL

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Usikonde ni udadisi tu. Kula au kutokula hii kitu ni haki na suala binafsi. Twanga tu hakuna atakayekukwaza dadangu.

Yasinta Ngonyani said...

Mwal. Najua na nilijua ni udadisi tu kama mimi mwenyewe KAPULYA:-) Sasa nimegundua wadadisi tupo wengi...

John Mwaipopo said...

Mwalimu Mhango kwa udodosaji hutamuweza. dada mkuu Yasinta kitimoto ndio mpango 'nzima'

Yasinta Ngonyani said...

Eeeeh mwee! Kaka mkuu John yaani ni leo tu nimekukumbuka mno. Karibu kaka mkuu...halafu nimependa msemo wako "kitimoto ndio mpango 'mzima'"

obat cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat penggugur