Saturday, April 26, 2014

HAYA NI MAPISHI YA JIONI YA JUMAMOSI YA LEO.......KARIBUNI KUJUMUIKA NASI!!

 Maandalizi:- Muhogo, Kabichi/Kebichi, kiazi kitamu, nyanya, binzari, chumvi, limau, kitunguu saumu,  kitunguu cha kawaida, tui la nazi, nyanya kopo,  maharagwe, mchele na mafuta.
 Wali wa nazi, Kachumbali, Maharagwe yaliyoungwa kitunguu, nyanya moja, chumvi na kijiko kimoja cha chai cha binzari, Kabichi/Kabichi iliyoungwa kwa nyanya na kitunguu, na mihogo na viazi vitamu vilivyokaangwa (chips)
Na hapa ndivyo ilivyoonekana sahani ya Kapulya jioni hii  na cha kuteremshia si kingine tena bali ni maji. KARIBUNI SANA...MIJA UPO...NA WENGINE WOTEEEE....TWAWATAKIENI JUMAMOSI NJEMA SANA WOTE!

13 comments:

Rachel Siwa said...

Duhh...Njaa,Usimalize KADALA.Nanyi muwe na J'mosi njema.

Yasinta Ngonyani said...

KACHIKI! Usiwe na shaka kipo kingi tu utakula mpaka kusaza......ahsante kwa yote:-D

Anonymous said...

Yaani ni chakula cha afya (diet), sio ile yenye minyama ya mafuta mafuta yanayo ongeza cholesterol. Heko da Yasinta kwa msosi mzuri! By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu..usengwili...mpaka nimejisahau na kukushukuru kwa kingoni. Nakwambia jana kulikuwa hakuna nyama wala samaki........ahsante na karibu

Anonymous said...

Naona Dada jana uliamua kabisa, hongera kwa mapishi. Mie nauliza hiyo mihogo umenunua wapi? Na je ni mitamu au?

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu yangu!..hakika jana nikawaweka samaki pembeni pia nyama..nikapika mlo huu..tena maharagwe ni ya kutoka kwetu Songea mihogo inapatiikana kwenye maduka ya vyakula viazi pia hata ndizi za kupiks

Anonymous said...

Asante kwa taarifa ya wapi pa kupata mihogo. Ila ina maana maharage uliyobeba hayajaisha? mana naona umeandika ni ya Songea.

Yasinta Ngonyani said...

Karibu sana ndugu yangu...ni kweli ya kunyumba/Songea ...nilibeba mengiii si kwa ajili yetu tu na marafiki pia majirani wakikutembelea

Mija Shija Sayi said...

Yasinta uchokozi huo...Eeebanaee!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Jamani Mija... Nimefanya nini sasa..LOL Najua umetamani kweli hapo ulipo:-)

Bashikulu Mligo said...

Huo msosi wa nguvu. wanawake mnajua kuchanaganya mahanjumati. yaani hapo unaposogea tu mezani unaanza kushiba.Hongra maana bado unakumbuka vyakula vya nyumbani

Interestedtips said...

Duh,,,,dada hapo ukishiba unanyoosha kabisa na miguu...full afyaaa

obat cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat penggugur