Thursday, January 5, 2012

LEO NI SIKU YANGU YA KUZALIWA!!!

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kunilinda salama mpaka kufika siku hii ya leo na kuongeza limwaka limoja zaidi. "AU uzee". Namshukuru kwa kuniepusha na mambo mabaya, magonjwa na pia vishawishi. Pia nawshukuru sana wazazi/walezi wangu kwa kunilea na kuwa kama nilivyo. Na halafu napenda kuwapa HERI YA KUZALIWA wote waliozaliwa mwezi huu walitimiza tayari miaka na watakaotimiza siku zijazo.
NAPENDA PIA KUSHEHEREKEA SIKU HII KWA WIMBO HUU:-)

NAMSHUKURU MUNGU KWA YOTE, FAMILIA YANGU PIA NINYI NDUGU ZANGU NA MARAFIKI WOTE NA NASEMA NAWAPENDENI SANA:-)

34 comments:

Baraka Chibiriti said...

Heri nyingi sana Dada Yasinta kwa kuzaliwa upya: HAPPY BIRTHDAY...Kila laheri katika maisha yako.

Mimi ni tarehe 05/02.

Rachel Siwa said...

Hongera sana da'Yasinta Mungu akubariki sana katika yote yaliyo mema,Akuguse na Kutamalaki katika Kaya yako pia.

Unknown said...

Epi besdei ya siku ya kuzaliwa kwako dada Yasinta. Mungu azidi kukulinda na kukupa afya njema wewe na familia yako. Amen na ahsante kwa yote..

Evarist Chahali said...

Heri kwa siku yako ya kuzaliwa.Mungu akushushie kila baraka na mafanikio.Enjoy your big day

Ng'wanambiti said...

Kheri kwa siku yako hii muhimu! Pamoja sana!

EDNA said...

Hongera sana mdada kwa kuongeza mwaka mmja zaidi,Mungu na akupe miaka mingi duniani.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

heri yako umeifikia mapema mwaka huu

ISSACK CHE JIAH said...

Mimi nakupongeza kwa hilo na mwenyezi mungu akujalie uishi kama jiwe ila TUNATAKA KUJUWA UNATIMIZA MIAKA MINGAPI? Auunaogopa utaitwa bibi?

sam mbogo said...

Hongera sana,bibie,kwani maisha nimatamu lakini mafupisana.kula tano binti wa kingoni . unaanza mwaka vizuri kwa kusherhekea siku ya kuzaliwa hongera sana. kaka s.

Goodman Manyanya Phiri said...

Hongera! Na ubarikiwe sana! Sehemu yako mioyoni yetu hachukui mtu mwingine hata siku moja!

MissPosh said...

wish you all the happiness in the world! Happy Birthday!

Mzee wa Changamoto said...

Dadangu mpeeeeenzi.
NI SIKU MUHIMU KWAKO.
Well!!! Si kwako tu, bali hata kwa "WAKO". Yaani wale wote ambao maisha yao huguswa ama kuathiriwa na uwepo wako.
Nami nakuombea kila jema katika maisha haya. Ili mafanikio yakuandame katika kila jema utendalo, busara itawale katika kila uwazalo na maamuzi ufanyayo na kisha watu wauone UKUU WA MUNGU NDANI MWAKO
Happy EARTHday Dada yangu

ray njau said...

Haya ndiyo maisha na mafanikio.
Salamu kwako,familia,ndugu,jamaa na marafiki.
Kizuri kula na nduguzo na kichungu meza mwenyewe.
"SIKU NJEMA"

Justine Magotti said...

nami nakutakia heri na baraka tele za mwenyezi mungu

Sara Chitunda said...

Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa Mungu akubariki, akuepushe na magonjwa, na vitu vyote vibaya akuzidishe na zaidi uishi miaka mingi kadiri ya yeye apendavyo

Penina Simon said...

Happy birthday my love,

Ausal said...

Hongera sana Yasinta!Mungu akupe afya na hekima zaidi,ili uwezo kutujuza sisi wafuasi wako pamoja na kutufundisha!

Raymond Mkandawile said...

HERI YA KUZALIWA DADA YANGU KAPUYLYA,NAKUOMBEA MAISHA MAREFU NA YENYE MAFANIKIO MAKUBWA SANA.HAPPY BIRTHDAY TO YOU KAPULYA...

John Mwaipopo said...

kutokufika kabisa ndio kitu kibaya lakini kuchelewa ni uafrika pia. nadhani sijachelewa kukupongeza kwa kutimiza miaka hiyo. uwe na wakati mujarabu

Mbele said...

Hongera, na kila la heri.

Mija Shija Sayi said...

Yasinta hongera sana dadangu, Mungu akuzidishie miaka na miaka, uzidi kupendeza nje na ndani daima na daima....Na..

...Mbarikiwe wote mliomtakia heri dada yetu Yasinta.

Kila la heri Mrs K. usilewe sana.

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii kuwashukuruni wote kwa jinsi mlivyokuwa nami siku hii ambayo ndo nilikuja hapa duniani. Mwenyezi Mungu azidi kuwapa moyo wa upendo na azidi kuwapa afaya njema. kuna mmoja ameuliza nimetimiza miaka mingapi? nimeona iwe ni kitendawili ila mwakani nitawaambia nimetimiza miaka mingapi...AHSANTENI SANA na mnakaribishwa kuendelea kutoa pongezi...NAWAPENDENI SANA:-)

mumyhery said...

Hongera sana Mama Erick, nakuombea maisha marefu yenye furaha na afya tele

Unknown said...

Happy belated birthday Yasinta. Endelea kuwa mrembo, mpole, mvumilivu na jasiri.
Angie Dodoma

Mija Shija Sayi said...

Upole haufai wakati mwingine @da'Angie Dodoma..lol!!

Salehe Msanda said...

kila la kheri kwa kuanzimisha siku yako ya kuzaliwa

Rafikio wa Hiari said...

Hongera sana Rafiki yangu kwa siku yako ya kuzaliwa. Natumaini siku yako ilienda vizuri. Napenda kukutakia Heri na Baraka tele, Mungu azidi kukubariki, akujalie na akutimizie kile unachokiomba kutoka kwake ukapate kuanza mwaka kwa mafanikio na uweze kutimiza malengo yako yote. Nakufurahia sana rafiki yangu wa hiari!

Anonymous said...

Upole wa ujasiri Da Mija, sio ule wa kuonewa... ha ha haa. unakua mpole lakini jasiri mpaka mtu anakuogopa, ntamuingiaje yule....
Angie

Anonymous said...

Sijachelewa........ nakupa hongera kwa kusherehekea siku yako ya kuzaliwa

Kaka yako wa hiyari SHABAN KALUSE WA BLOG YA UTAMBUZI NA KUJITAMBUA

Anonymous said...

happy birthday! umri unaongezeka, nakumbuka miaka ya 80 wakati ule ukiwa mdogo kule mahenge songea.

Yasinta Ngonyani said...

Dada M! ahsante sana nawe pia uwe na afya njema.

Da´Angie Dodoma! ahsante kwa yote na karibu sana hapa kibarani.

Mija! unataka niwe mkali?

Kaka Salehe! Ahasante sana kwa kuwa nami kwa siku hii.

Kaka yangu wa Hiari Shabani Ahsante sana na wala usiwe na shaka kuwa umechelewa kwani mwezi huu wote ni mwezi wangu..LOL

Wewe usiye na jina nwe nashukuru sana ingawa umenifanya nijiulize mara elfu wewe ni nani maana inaelekea unanifahamu..ningefurahi kujua. AHSANTE.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Aiiii....hata naona aibu kuchelewa namna hii. Ngoja nipige moyo konde tu.

Hongera Da Yasinta. Ubarikiwe sana wewe pamoja na familia yako !!!

Simon Kitururu said...

Hongera Yasinta!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Matondo na kaka Simon AHSANTENI. uzee naukaribia:-) maana kuongeza mwaka ndo kuukaribisha uzee nasikia.