Saturday, April 20, 2013

JUMAMOSI ...UJUMBE WANGU NI HUU....

Ukiwa DUNIANI USIHUZUNIKE na usiwe MNYONGE hata kama una UMASKINI kiasi gani. Mungu yuko pamoja nawe na unatakiwa kuzingatia haya:-
1. Usijilaumu kwa lolote lililokutokea
2. Usihofu kuhusu hali uliyo nayo sasa.
3. Usijilinganishe na mtu yeyote duniani.
4. 5. kumbuka Mungu ndie mpangaji wa kila linalokutokea.
6. Usiwaze sana kuhusu kesho waza kuhusu leo.
7. Kukikosa ulichokikusudia yote ni mipango ya Mungu.
MUWE NA SIKU/JUMAMOSI  NJEMA

7 comments:

Baraka Chibiriti said...

KABISA DADA YASINTA, UMENENA.....UJUMBE WAKO NI MZURI NIMEUPENDA!

Anonymous said...

Ni kweli Yasinta. Mungu atusaidie mana kwa akili za kibinadamu ni ngumu sana kuepukana na hayo, ila kwa uwezo wa Mungu tunaweza na kushinda. Ubarikiwe sana na ujumbe huu mzuri sana na wa kutia moyo.

Anonymous said...

maneno mazuri sana mimi peke yangu hapa sijiamini sijui ni kwa nini sijui ni malezi au nini najiona niko down saa zote sijui kwa nini

Rachel siwa Isaac said...

Asante sana KADALA kwa ujumbe mzuri....J'Mosi iwe njema kwako na familia pia.

NN Mhango said...

Da Yacinta mimi sikubaliani kabisa nawe. Kwanini kumsingizia Mungu hata kwenye upuuzi? Hivi wabakaji, mafisadi, wauaji, wababaishaji na watenda maovu wote ni mpango wa Mungu? Ingekuwa hivyo basi asingetoa amri kumi. Kwa ufupi ni kwamba alipopewa akili tofauti na wanyama, mwanadamu alianza kuwajibika kwa matendo yake. Nitatoa mfano toka nyumbani. Hivi kweli umaskini wa watanzania ni mpango wa Mungu au wa kutengenezwa na binadamu waroho na wenye roho mbaya wasioona mbali? Hamuwezi kupewa raslimali zote hizo na Mungu halafu akajipinga. Tafakarini upya jamani.

Anonymous said...

Yasinta siku hizi huchangii comments, ukishaandika hiyo mada ndio basi. Upo lakini?

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu zangu ahsanteni kqs mchango wenu...tupo pamoja...

Usiye na jina wa 2:05 pm sio hivyo michakato ni mingi tu ila nipo