Tuesday, April 23, 2013

KUNA NJIA NYINGI YA KUITANGAZA BENDERA YETU YA TANZANIA...

Nimependa magauni haya nafikiri safati ijayo nami nitashona maana duh nimepeata hamu kweli--kama tusemavyo ni rangi nzuri na kila moja ina maana yake..tukianzia na..
1. Nyeusi- Huonyesha watu wa Jamuhuri ya Tanzania.
2. Kijani - Huonyesha mimea na ardhi ya Tanzania
3. Njano - Huonyesha utajiri wa mali ya asili.
4. Bluu - Huonyesha bahari inayoziunganisha sehemu za Jamuhuri ya Muungano
Haya ni maelezo  ya Bendera yetu ya Jamuhuri ya Tanzania....Si mnakumbuka tulijifunza darasa la tatu-nne vile au?......Nawatakieni wote JUMANNE NJEMA!!!!

8 comments:

Ester Ulaya said...

ukweli wamependeza sanaaaaa, nitashona nguo kama hiyo nami nipendeze

Yasinta Ngonyani said...

Ester! basi tutakuwa saresare maua halafu tusisahau na kilemba pia:-)

Anonymous said...

Tanza-nia Tanzania! Nakupenda kwa moyo wote...........By Salumu

emu-three said...

Mhh, ni kweli mpendwa, utaifa mbele, mengine baadaye. Na moja ya kuonyesha utaifa wako ni kujali alama za nchi kama bendera, huenda na vazi la taifa liwe hivyo...

Mija Shija Sayi said...

Daah!! Wamependeza, halafu bendera yetu ina rangi nzuri kweli!

Yasinta Ngonyani said...

Wote ni kweli mliyosems.
Da " moja je ww hutakikiwa sare nasi ? Ili kszi uifanye au labda shem wetu? Kwani mie na Ester twapenda.