Saturday, April 6, 2013

JUMAMOSI YA LEO NINGEPENDA MLO WANGU UNGEKUWA HIVI...NAOTA NDOTO...

 
 

Nimeamka na kuanza kufikiri huu ungekuwa mlo wangu wa siku ya leo chai kwa maandazi au vitumbua...
 ....chai ya rangi bila sukari
 ...au labda chai kwa Vitumbua na chapati...
Na hapa ungekuwa mlo wangu wa mchana huu sambusa....Sambusa tamu sana ila inabidi uwe na muda haswaaa..
na kumalizia siku kwa ugali kwa samaki na kachumbali kidogo---
kumalizia na glasi ya maji...mmmhhh hivi ndivyo ningependa siku yangu ya leo ningekula lakini sasa sitaweza ....nakula kwa macho. baadhi ya picha nimezipata hapa. JUMAMOSI NJEMA.

8 comments:

Anonymous said...

Hapo kwenye ugali na samaki umeniua kabisa!
By Salumu.

Said Kamotta said...

Wow!...mimi breakfast yangu hapo ningechukua kila "bite" kimoja kimoja andazi, chapati, sambusa, kitumbua na hiyo chai....Hahahaha! itapendeza kama kila kimoja nikionje na kujua kimepikwa kwa mapishi ya gani....

Said Kamotta said...

Wow!...mimi breakfast yangu hapo ningechukua kila "bite" kimoja kimoja andazi, chapati, sambusa, kitumbua na hiyo chai....Hahahaha! itapendeza kama kila kimoja nikionje na kujua kimepikwa kwa mapishi ya gani....

Amina mzava said...

Hapo kwenye samaki mimi hoi dada siunajua tena mpare kwa samaki hata picha tu mm ugali unashuka

Mija Shija Sayi said...

Yasinta kwa nini uote wakati uwezo wa kuvitengeneza unao? nakuaminia dada mkuu..

Anonymous said...

Ni kweli da Mija nami nilitaka kumwambia kuwa anayaweza hayo mapishi, muda wake tu. Mie ukipika vitumbua naomba nitaarifu ili niwe mgeni wako Yasinta. Pia chapati na samaki.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa kula nami kwa macho na wale waliokula kwa ukweli. ..Mija tatizo si uwezo ni uvivu hasa hizo sambusa ....usiye na jina wala usikonde nitakutaarifu:-)

Ester Ulaya said...

Duh, milo mitamu mno, sasa hapo kila sahani unatakiwa ule kidogo ili usiishie njiani, mweh