Friday, April 12, 2013

LEO TULIKUWA TUKIMSINDIKIZA DADA YETU MPENDWA MARIANA KATIKA SAFARI YAKE/MAKAO YAKE YA MILELE....

Kama nilivyowataarifu hapa basi leo imekuwa siku ya mwisho kumsindikiza dada yetu, Mama yetu na rafiki yet mpendwa Mariana katika makao yake ya milele..................................................................


HAPA NDIPO ATAKAPOLALA DADA MARIANA
 PAMOJA NA MWANAE MANUELA
Siku ya leo imekuwa siku ndefu na ya masikitiko kwa familia, ndugu jamaa na marafiki na imekuwa siku ya kujifunza mengi kwangu, kutoka kwa da´mkubwa Mariana kwa kweli. Ama kweli wote watendao mema huwa wanatutangulia kwanza. Katika maisha yangu hapa nimewahi kwenda  kwenya misiba/mazishi mingi/mengi sana lakini huu leo hapana. Watu walifurika kuliko kawaida kiasi kwamba nikajiona nipo kwangu Afrika. Na kanisa lilikuwa halitoshi kabisa. Kweli ukitenda mema utarudishiwa hapa hapa duniani. Watu walifumuka pande zote. Au niseme hivi kwa kifupi dada huyu hakuna neno la kutosheleza maelezo yake kwa kweli,,,,alijali sana wengine na mpaka kujisahau mwenyewe. NITAKUKUMBUKA DAIMA. MWENYEZI MUNGU NA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMINA

11 comments:

Rachel Siwa said...

poleni sana wapendwa..Mlale kwa amani dada Mariana na Manuela...Tumshukuru MUNGU katika yote..

Ameen.

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki! Yaami hata mie mamshukuru mungu mazishi yameenda salama kabisa na watu wote wsliohudhuria napenda kuwsombea kwa moyo wso mkunjufu. Amani na baraka viwe nanyi. Mlale mahali pema peponi.

Anonymous said...

Pole sana Yasinta na familia yake yote na wote waliohudhuria mazishi. Mungu azidi kuwafariji.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina tumeipokea pole kwa moyo mkunjufu. Na tunamshukuru mungu kwa hili.

Mija Shija Sayi said...

RIP dada Mariana... Poleni Yasinta!

Anonymous said...

Pole dada Yasinta, Mungu awafariji sana! By Salumu

ray njau said...

Pole kwa dada Yasinta na kwa ndugu jamaa na marafiki.Daima urafiki unashinda undugu.

Salehe Msanda said...

Habari
Ama kweli ni somo kubwa alilotuachia....
Pole kwa majonzi ya kifo na mazishi da mkubwa.
Lililombele yetu ni nasi kutenda mema hapa duniani ili tuweze kukumbukwa kwa wema
Lakini kubwa zaidi kwa kutenda wemu kunatuwezesha kuwafanya wengine wahisi na kusikia furaha na amani
Kila la kheri.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Siku zote ukubwa una huzuni kuliko utoto. Kifo ni somo ambalo kila siku lazima tulizingatie maana hakuna ajuaye siku wala saa. Waliotangulia wamemaliza ngwe yao bado yetu.
TUNAWAOMBEA PUMZIKO JEMA LA MILELE AMINA.
Familia na marafiki tunawatakia faraja na heri katika kuendelea na maisha. Ushauri ni kwamba yale mema waliyotenda marehemu yaenziwe na kuendeleza huku tukiwasamehe pale walipokosea.

Mwanasosholojia said...

Poleni sana dada yangu Yasinta kwa msiba huu. Bwana alitoa, ametwaa jina lake lihimidiwe. Muwe na nguvu na uvumilivu katika kipindi chote hiki.

Anonymous said...

Poleni wapendwa!