Tuesday, April 16, 2013

KANGA YA VIKOMBE VYA CHAI...NIMEIPENDA HII KANGA!!!!!

Maandishi yanasema ISIKUHADAE RANGI TAMU YA CHAI NI SUKARI...Hivi ni kweli?

6 comments:

Ester Ulaya said...

hehehehe ila bila sukari sidhani kama itakamilika kuwa chai.....na majani nayo yana uzito wake kwakweli ili kukamilisha neno chai

Yasinta Ngonyani said...

Hapa tutatofautiana bila Sukari ni kweli ndo CHAI...Ni kweli bila majani haiwezi kuitwa chai...

NN Mhango said...

Mi napenda khanga yenye kijungu so to speak.

Mija Shija Sayi said...

Hii ilikuwa kweli enzi za mwalimu!

sam mbogo said...

Hapa sasa inakuwa kasheshe! maana ya chai ninini? na maana ya sukari ninini?. ila maneno ya kanga yana athiri sana fikra na mitazamo/mtazamo wa wanajamii kwa ujumla.mfano ukitaka kumpa zawadi mama mkwe wako ya kanga,inabidi uwe makini,hasa ukizingatia maneno au misemo itakayao kuwa imeandikwa katika kanga hiyo.muhimu hapa ni tafasiri maana ya neno hilo ,wengi mama wakwe( baadhi) waweza fikiri umemchagulia kanga nzuri namaneno mazuri kumbe umelikoroga,mfano neno NANI KAMA MMA!. wachangiaji wote hapo juu nimependa jinsi mlivyo weza kuonyesha hisia zenu,mitazamo yenu, kifikra juu ya kanga,hasa maneno yake amabayo ,chai na sukari vimeibua mjadala.ila msisahau kuna asali pia ni nzuri katika chai. kakas

sam mbogo said...

samahani,kuna kosa kidogo .kuhusu uneno/usemi nilio uandika katika herui kubwa,nina maana,NANI KAMA MAMA,nasiyo MMA.kakas