Wednesday, April 24, 2013

KATIKA MAISHA KUNA KUPENDWA NA KUCHUKIWA NA WATU ....!!! UPENDO!!!

Kupenda/upendo ni kitu cha ajabu sana mara nyingi nimekuwa nimejiuliza kwa nini sisi binadamu tuna upendo tofauti kwa kila mtu. Nikisema hivi nina maana kuna wakati mtu inaweza kutokea unampenda mtu kiasi kwamba huwezi kujizuia. Na cha ajabu mara nyingine uanaweza kumpenda mtu ambaye hujawahi kumwona ana kwa ana(uso kwa uso) na upendo ukawa wa nguvu kali sana.
Halafu sasa inaweza kuwa kinyume kabisa. Yaani watu tunaweza kuwa na chuki. Unaonana na mtu siku moja tu na utasikia simpendi kabisa jamaa huyu. Au hata kuangalia tu picha yake unapatwa na chuki. Nashangaa sana kwa uwezo kama huu ambao MUNGU amatupa na pia SHETANI anaingilia na kuharibu.Swali:- Hivi hii inatokana na nini?
Leo nimeona niimbe mwenyewe ila samahani hamtaisikia sauti yangu:
Upendo, upendo, upendo ni amri ya bwana, Yesu alisema pendaneni, pendaneni kama nilivyowapenda. Nanyi pia, nanyi pia mpendane palipo na upendo Mungu yupo nasi tupendane tupendanex2.
NAWATAKIENI WOTE UPENDO NA AMANI KATIKA KILA MFANYACHO...KAPULYA

 

5 comments:

sam mbogo said...

kupenda/kupendana/kupendwa ni hali ambayo kila binaadam anayo hasa anapokuwa akipambanua vitu viwili au makundi iwe ni kwa picha au hata anakwaana/usokwauso.pia kupendwa /kupenda kunatengenezwa na binaadam.pia chuki husababishwa na binaadam mwenyewe. huambiwi na mtu sasa mchukie fulani au sasa mpende fulani.pia yawezekana ukavutiwa katika kupenda au kumpenda huyo binaadam mwenzako(kike/kiume) anavyo cheka tuu au midomo yake au muonekano wake kwa ujumla yaani FIGA/BODI/SHEPU nk.na vivyohivyo hata kuchukia.pia kuna kupendana kwa kawaida ambayo huwa wengi hatuiseme hadharani kama nikupenda tuahishia kusema ,jamaa anaelewana sana na fulani,au hawa ni marafiki sana,kwa dada zetu mara nyingi huitana shoga/mashoga(siyo ile maana nyingine).maranyingi huji sahau na kudhani kupenda/kupendana/kupendwa ni kwa ajili mapenzi ya kimwili hapana au lazima yawe ya jiinsia tofauti(mke/mume). na kuhusu kuchukiwa/kuchukiana kupo huwezi ukapendwa na wote kwa hiyo kama unauhakika hujamfanyia kasa lolote akuchukiaye basi wewe mlipe mema.kaka s

Anonymous said...

no comments

Anonymous said...

Yasinta,tupe uhalisia kwako, je umewahi kumchukia/unamchukia mtu?

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! ulichokisema ni kweli kabisa..nimependa jinsi ulivyoelezea:-)
Usiye na jina wa 8:21..no comments nayo ni maoni pia..

Na usiye na jina wa 9:55 ntajaribu kukujibu ..Hakuna binadamu asiye chukia ..maana kuchuukia ni kama kupenda..Kwa ukweli sina tabia ya kuchukia mtu..ila kwa vile mimi ni binadamu inatokea nachukia na kusamehe ila si kuchukia milele.

Mwanasosholojia said...

Asenti Da'Yasinta....siongezi zaidi neno umesema yote!