Tuesday, April 9, 2013

PALE WATU WANAPOJIULIZA KWA NINI WANGONI WANA VIBONGO/MAJINA YA UKOO KAMA WANYAMA????

Dhumuni la leo ni kutaka kumjibibu dada msaidizi katika mada hii swali lake lilikuwa kama lifuatavya hapa chini
Mija Shija Sayi said...Yasinta umependezaje?
Hebu naomba utusaidie wadau wako kwamba, ni kwanini wangoni majina yao mengi wamechukua kwa wanyama?
Ngonyani, Mapunda.. n.k, Je kuna historia yoyote? Kaka S mtaalamu wa mambo ya Tamaduni,swali hili unaweza tusaidia pia..
Asanteni..
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
nami nitajaribu kujibu kama ifuatavyo....
Wangoni wanajulikana sana kwa kuwa na mvibongo/majina ya wanyama wa pori, na hata wanyama wa nyumbani ama majina ya miti au hata ya nyasi. hii ilianzia pale ukoo wa mwanzo ulitoka wapi, wangoni wana majina ambayo yanaelezea kile wanachokifanya, jinsi walivyokuwa hapo kale nk- Walipoanza kutembea na kupiga vita na watu wengine ndo hapo wakaongezea  na majina ya wanyama, ndege na ya miti. kwa mfano:- Cawe, Gama, Kapungu, Komba, Kunguru, Mbawala, Nyati, Nguruwe, Ngonyani, Soko, Nyoka na Tembo.....na mengine mengi sitaweza kuyataja yote maana ni mengi mno..

5 comments:

Interestedtips said...

Nafuu Da'Mija kauliza hilo swali, kwani na mimi huwa napenda sna kujua kwakweli

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Si wangoni tu. Hata wanyasa au wanyanja au waite wachewa ama watumbuka wana mchezo huo. Nadhani hii inaonyesha ukaribu wa wanyama na wanadamu. Pia inaonyesha aina Fulani ya kukubali kuwa sayansi nyingi kama vile kutengeneza mitumbwi, madawa, aina za vyakula binadamu amejifunza toka kwa wanyama. Pia kuna kukiri kuwa fikra nyingi na ushujaa umeigwa toka kwa wanyama. Mfano twiga kuona mbali. Simba ushujaa na ukali. Sungura ujanja n.k.
By the way, da Yacinta nilikuuliza habari za mwalimu Matondo Masangu wa Nzulilima bila majibu. Je una habari zake?

Yasinta Ngonyani said...

Ester! hata mie nimefurahi Mija kauliza hili swali...
Mwl. Mhango ! kwa kwa kweli nimeipenda tafsiri yako mno..kwani hata nami naamini ni hivyo. Kuhusu Mwl. Matondo sio kwamba nilikaa kimya makusudi ni kwamba hata mie sijui wapi yupo ila nitalifanyia kazi ,,,,ahsante kwa kujali..

Mija Shija Sayi said...

Asante Head Prefect Yasinta,...Kwa kweli majina yetu yana maana sana. Halafu swali lingine eti kuna uwiano kati ya tabia ya mtu na tabia ya jina alilonalo?... kwamba kama ukimpa mtoto jina la furaha basi kuna uwezekano mkubwa wa mtoto huyo kuwa na tabia ya furaha, ukimwita Shujaa basi tabia zake zinakuwa za kishujaa shujaa, ukimwita Komba, basi jiandae na Ulevi..

Sijui wenzangu mnasemaje hapo..

Yasinta Ngonyani said...

Dada mkuu msaidizi! Hii ya uwiano kati tabia na majina tupatayo kwa kweli hii inatokana na imani
Ukiamini jivuo basi itakuwa hivyo.