Friday, June 8, 2012

WATU TUMETOKA MBALI/KUJIFUNZA MAISHA!!!

Picha hii imenipeleka mbali sana. Hakika watu tumetoka mbali na changamoto nyingi tumepitia. Binafsi napenda kuwashukuru wazazi/walezi wangu kwa kunilea, kuniongoza vipi jinsi ya kuishi maisha. Je? wewe pia unakumbuka kazi za utotoni?.......IJUMAA NJEMA TENA!!!

16 comments:

Interestedtips said...

nimekumbuka kijijini kwetu, kusenya kuni milimani, yaani kuna muda nilikuwa nabeba nyingi kwa sifa ili bibi anisifie, ila shingo sasa kuuma ni balaa, ila naamini ndi iliniweka strong hadi leo

Yasinta Ngonyani said...

Ester amini ni kweli umekuwa mkakamavu kwa kazi kama hizo...Je? kwani hukupata sifa na bibi? Na kweli umenikumbusha hata mie unabeba limzigio la kuni halafu sasa unapokaribia kufika nyumbani wewe mzigo unakuwa mzito ajabu...

sam mbogo said...

Kusenya kuni,Ester umenikumbusha usemihuu ni maarufu sana katika badhi ya sehemu nilizo wahi kuakaa na ila baadae nilikuwa nasenya kuni mjini!dsm.kumbukumbu nzuri kuishi na babu na bibi ningepata bahati hiyo nafikiri ningejifunza mengi.nikiwa naumri kama wa huyo mtoto/binti na kumzidi kidogo ,kipindi cha kukaribia kumaliza msingi na kuingia sekondari nilifanya kazi za kufyeka kufagia uwanja,kupalilia nyasi kuzunguka nyumba,kumwagilia bustani yamchicha,kukatia michongoma,kulisha kuku nk.nilikuwa na muda mfupi sana katika ukuwaji wangu na maisha ya kijijini,siunajuwa enzi hizo ukiwa na ndugu mjini,kaka au dada anakuja kukuchukua mkaishi naye mjini,yaani anakutunza kusaidia wazazi,kipindi hicho hakika ni kigumu na nishule tosha. shukrani kwa kumbukumbu hii ya kusenya kuni.kaka s.

Rachel Siwa said...

Ahsante da'Kadala kwa kumbukumbu nzuri!!

ray njau said...

Asante kwa mada husika.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! kumbe ww hodari wa kazi nyingi na bado unakumbuka...kazi ambayo mimi nilikuwa siipendi ni kukoboa mahindi..halafu tukumbuke kuwa kufanya hizi kazi ndio inawanya watoto kujifunza maisha...
Rachel/kachiki, kaka Ray tupo pamoja.

Interestedtips said...

yaani bibi alikuwa ananisifia kwa baba alipokuwa anakuja likizo,anamwambia Ester mkokomavu ananisaidia sana kusenya kuni, ikifika muda wa chai napewa vikombe viwili vya chai, nikikumbuka nammiss sana bibi, alikuwa akipika chochote kama sipo ananihifadhia

MARKUS MPANGALA said...

maisha yetu yana kitabu chake kwa kila hatua unayosonga mbele. kuna wengine tumetokea kwenye hali kama hii maeneo tuliyoishi. muhimu ni kutambua mazingira na kukabiliana nayo, sio tatizo ila ni changamoto

emuthree said...

Tupo pamoja ndugu wangu, angalau nimepita, yaani ..

nyahbingi worrior. said...

Watoto wa leo hawatakuwa na kuadisia kwasababu sisi wazamani tumeweza kuadisi kwasababu tulifanya mambo kama hayo katika picha.Mtoto wa leo,wa mjini atakata kuni wapi?

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua tena fursa hii na kusema kweli sisi tulikua wakati ule tuna mengi sana ya kukumbuka na kuwasimulia wanetu na ikiwezekana kuwafunza. Bahati mbaya wengi sasa wanakimbilia mjini kwa hiyo watakosa utirhi huu. Maana kwa kweli ukiangalia mtoto aishiye kijijini na mjini kwa sasa hakika ni hasara sana kwa yule wa mjini hawezi hata kuchuma matembele...

Rachel Siwa said...

Teh tehthetehh kaka Nyabingi na da'Kadala!!!!!Pia Mazingira yanachangia.

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki! si umwongo usemala

batamwa said...

kushenya enkwi(kushenyakuni)kihaya hakuna maisha mazuri kama hayo ni kweli ukija na mzigo mwingi mama lazima akwihukyeyo(akupepole na kukupongeza)yaani ni raha kabisa ila tu wakati mwingine mlikuwa mnaenda kushenya kuni mnaanza kucheza halafu kustuka usiku umeingia unarudi nyumbani bakora zinatembea lakini yote ilikuwa ni kujifunza asanta dada Yasinta unatupeleka mbali sana ndio maana lazima nipite humu kijiweni kilasiku kuona nini kipya na chazamani ubarikiwe sana

aisha said...

Kwakweli umenikumbusha mbali, nilikuwa nabeba mzigo wakuni nanikimaliza . shingo yote inaniuma

Salehe Msanda said...

Nami umenikumbusha mbali.
Hiki ni kitu wanachokikosa wanetu sisi watanzania na kusababisha kuwa na matumaini ya maisha ya kufikirika na kuwa na matarajio ya kufikirika.
Unakumbuka siri iliyoko katika kitendo cha kula katika mduara. Na kuhakikisha kila mtoto anakuwepo nyumbani muda wa kula. Mduara nikiwa na maana ya kula kwa kutumia sahani moja familia kwa maana ya wanawake peke yao na wanaume peke yao.
Pia nakumbuka jinsi babu yangu alivyokuwa anatukataza kutumia mikono miwili wakati wa kupata kifungua kinywa kunywa chai au uji.
Kuna mambo mengi ya enzi hizo yalikuwa yanayofundisha kuhusu kuishi kama wamoja na kwa kujaliana.
Kila la kheri