Friday, June 15, 2012

VYAKULA VYA ASILI NI VITAMU/ HAPA MIMI NIMEFIA KABISA

Hakika ebu angalia hapa ugali tena bongo BONDO, samaki na mboga majani  na matunda/matikiti maji baada ya chakula. Halafu sasa fikiria hapo ugali umelima mahindi/mihogo, ulezi au sijui mtama, mboga umelima mwenyewe bustani, samaki umewavua mwenyewe au tu umetoka kuwanunu wakati tu wavuvi wamerudi. Matikiti maji nayo labda umeyalima mwenyewe ....ashilia mbali viungo. Yaani hakuna kitu kilichokaa kwenye kopo wala nini? Mmmmhhh!! Yamu yamu yamu  ngoja niache ...picha toka kwa kaka Mjengwa.

10 comments:

emuthree said...

Mmmmmh njaa kweli kweli, siku hizi bnongo mifuko yote imetoboka,....nashukuru ndugu wangu!

ray njau said...

Sina hakika kama kuonja ni ruksa!

Yasinta Ngonyani said...

emu3! Sio peke yako mie hapa yaani bonge la njaa na mate yanadondoka kama fisi. Ni katikati ya mwezi ndo kabisaaaa...mifuko imetoboka zaidi.

Kaka Ray! Nadhani unaruhusiwa kuonja...

Interestedtips said...

ndo nimetoka site, nina njaaaaaa, niliishia kutafuna vidaa tu, halafu hapa nakuta msosi mtamuuuuuuuuu, unanitegaaaaaaaa

Yasinta Ngonyani said...

Ester! pole sana, ila nimepita kule kwako nimeona umekula dagaa nami nimetamani wewe acha tu... mwenzio nimetamani kiasi kwamba niruke mpaka huko na kulitwanga hilo bondo...

Rachel Siwa said...

Kwetu ni kuzuri!!ila kulima nako kazi,lakini si mbaya wengine walime wengine wanunue au?Pamoja sana da'Kadala kwa kututengenezea njaa tehthethee

Wenu Kachiki.

sam mbogo said...

Kudadadeki,mmeniuzi! au mmeniudhi,kwanini mnatamani picha inayo onyesha chakula? ndugu yangu Ray hebu wakumbushe,kutamani ni....... DHAMBI.Ester,Yasinta na bisikuti yangu,kachiki Rachel pigeni magoti na mtubu! - nawatania!? kaka s.

ray njau said...

Kaka na utani wako hongera sana.Ujumbe wako unasema kutamani ni dhambi.Hapa tuwekane sawa kuwa kuwa kuna tamaa nzuri na mbaya.Katazo lipo kwenye tamaa mbaya.Hapa watu wana hamu ya chakula na hakuna ayetamani hicho chakula.
----------------------------------
17 Basi alipokuwa ameingia katika nyumba akiwa mbali na umati, wanafunzi wake wakaanza kumuuliza habari ya mfano huo. 18 Kwa hiyo akawaambia: “Ninyi pia hamna ufahamu kama wao? Je, hamjui kwamba hakuna chochote kutoka nje kinachoingia ndani ya mtu ambacho kinaweza kumtia unajisi, 19 kwa kuwa hicho hupita na kuingia, si ndani ya moyo wake, bali ndani ya matumbo yake, nacho hutoka nje na kuingia ndani ya shimo la choo?” Kwa njia hiyo akatangaza vyakula vyote kuwa safi. 20 Tena akasema: “Kile ambacho hutoka ndani ya mtu ndicho humtia mtu unajisi; 21 kwa maana kutoka ndani, kutoka katika moyo wa watu, hutoka mawazo mabaya: uasherati, wizi, mauaji, 22 uzinzi, kutamani, matendo ya uovu, udanganyifu, mwenendo mpotovu, jicho lenye wivu, makufuru, majivuno, ukosefu wa akili. 23 Mambo hayo yote maovu hutoka ndani nayo humtia mtu unajisi."_Marko 7:17-23

sam mbogo said...

Ray,unauhakika hawa akina dada walishindwa kusema nina hamu na chakula hiki badala yake wakasema natamani au nakitamani chakula hiki.Lugha pia yaweza kuwa nimgogoro kimatamshi,nafikiri umefafanua vizuri na nimekuelea mkuu! waweza sema ninahamu ya ugali na si natamani ugali? kaka s

Interestedtips said...

hahahahhaa sasa hao dagaa niliwala wakavu bila wali wala bondo, kupoza njaa tu