Tuesday, June 19, 2012

JINSI NILIVYOWAZA NINI CHA KUPIKA JIONI YA LEO/NIMETAMANI MBOGA!!!



Nimeiangalia picha hii na kujikuta :-) ebu angalia hayo matembele na naona hapo kwenye hilo kapu kuna zaidi ila nikakaza moyo na kuendelea kuwaza.....

Jioni inaingia nimekaa hapa nawaza nini cha kupika mwanamke mimi...Ghafla natoka nje naangalia bustani . Uwiiiii..bado  bado kabisa. Naingia tena mtandaoni ili kupata mawazo nakutana na picha hii. Kamoyo kanadunda na hamu ya kupa huo mchicha, matembele,chaina ...halafu naangalia akina mama walivyojipanga hapa nami naanza kupata wazo nitawauzia majirani mboga zangu...ujanja eeeh:-)  Picha kutoka kwa Mjengwa.

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ngoja nikuelezeni jambo moja picha hiyo inanikumbusha kila jumapili Songea/manzense huwa ni siku maalumu kwa wakulima kwa hiyo kila kitu kinakuwa kimetoka tu shambani. EEeehh bwana wewe yaani mpaka raha kwa hiyo zimenifikisha mpaka huko na ndo hamu inazidi kwelikweli...

nyahbingi worrior. said...

Huku nyumbani hatuchagua cha kupika bali tunapika kilichopo.

Mija Shija Sayi said...

Nyumbani ni nyumbani kwa kweli....

Anonymous said...

nimeipenda hiyo NYUMBANI HATUCHAGUI CHA KUPIKA WALA HATUNA RATIBA KILICHPO NDO TWAPIKA HATA KA MWEZI MZIMA TWALA UGALI MBOGAMBOG AWALAAAAAAAAAAAAAAA HAITUSUMBUI

ray njau said...

@Yasinta;
Ukisema bora mapishi na siyo mapishi bora kwa laazizi wako na familia yako,wenzako wanasema...........!!

Interestedtips said...

tena mboga zote hapo shurti kwa ugali

Anonymous said...

Waboreshe mazingira.Kuweka chini namna hiyo si vizuri kiafya na hata kumvutia mteja.Watengeneze meza na juu take waweke hizo mboga na matunda.

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu zangu Ahsanteni sana kwa michango yenu...Maana bila uwepo wenu nisingepata nguvu...

ray njau said...

@Yasinta;
Uwepo wako ndiyo furaha yetu na raha yetu ndiyo uwepo wako na bila uwepo wako hakuna raha wala furaha yetu.