Tuesday, June 23, 2009

KUOA BILA KUTOA MAHARI (POSA)

Kutokana na maoni ya msomaji mmoja katika mada ya WANAWAKE UGHAIBUNI (SWEDEN). Nimeona ni vizuri mkijua ya kwamba:-

Maisha ya ndoa ya Afrika na hapa Sweden kila ninapojaribu kuwaelezea watu kuwa. Sisi waAfrika tunapokaribia umri wa kuoa kitu cha kwanza ni kutafuta mchumba na ukishampata zinaanza shughuli za kupanga mahari (posa). Lakini wao wanashangaa sana hata hawaelewi kabisa kwa nini tunatoa MAHARI(POSA). Wao wanadai ya kwamba tunauzwa, kama kuku. Yaani mzazi wa msichana anamuuza binti yake. Wanasema kama tunatoa mahari (posa) kwa kuwashukuru wazazi wa upande wa kike je? kwa nini na wazazi wa upande wa kiume wasipongezwe kwa kazi nzuri ya kumtunza kijana wao. Hata kama ukiwaambia ni njia ya kuonysha respect pia hawaelewi kabisa.
Hapo zamani hapa Sweden ilikuwa hivi , msichana akiolewa yaani anapoenda kuanza maisha kama mke. Alikuwa anachukua vitu toka kwao kama vile shuka, vyombo nk. Ni kama nyumbani TZ
Lakini siku hizi hiyo haipo hapa wanaoana/ishi tu hivihivi. Hakuna kutoa mahari ( posa) .
Naomba niseme hivi inaonekana kama watu wengi wanafikiri ukitoa MAHARI (POSA) basi ndio utakuwa mtawala. Yaani wanaume wengine wanakuwa na kasumba, wanajiona wakubwa wa nyumba, na mke anakuwa hana sauti. Anasema mi nimetoa MAHARI (POSA) kwa ajili yako.
Ndugu wasomaji kusema kweli sisi wanadamu tunaishi katika mila na desturi tofauti kabisa. Kwani hapa wao hili jambo la ndoa halihusishwi kabisa kwa wazazi. Ni baina ya kijana na msichana. wanaelewana wao wawili tu kama kufunga ndoa au kuishi hivihivi Naweza nikasema hii ni moja ya sababu ndoa zao hapa hazidumu muda mrefu. Haya wasomaji je kuna maelezo zaidi ya kuwaeleza watu hawa. Naomba MCHANGO basi.

14 comments:

Francis Godwin said...

Huo utaratibu wa Sweden ni mzuri sana kama hata huku Tanzania ingekuwa hivi mambo angekuwa safi sana ila ni kweli ukichunguza zaidi unabaini kuwa Tanznia bado kuna biashara ya binadamu kwani ukitaka kuoa leo mahali unayopangiwa unafikiri binti hata kwao hata rudi tena ,ila bado unatoa mahali kubwa na ndugu wote wanahamia kwa kijana iwapo una maisha poa, japo baadhi ya makabila kwa sasa yanaanza kukwepa kutoza mahali kubwa ila makabila mengine ukijaribu kumpenda binti yao ujue mahali ni mamilioni ya shilingi yatupasa kubadilika sasa

Faith S Hilary said...

Kama ulivyosema tupo tofauti na hao so huwezi kubadilisha mawazo yao no matter what you do. Lakini hata hivyo mahari hi hiari na sio lazima inategemea na wanandoa na wazazi pia na mahari isiwe kama binti anauzwa vile vile.

By the way is it "MAHALI" or "MAHARI"

Mahali - Place

Mahari - ?

Kama nimekosea nirekebishe.

Fadhy Mtanga said...

Inaitwa mahari.

Da Yasinta, huo utaratibu nauunga mkono mia kwa mia. Maana wengine hupanga mali utafikiri nini sijui.

Wenzetu kumbe wana mfumo wa kiungwana zaidi.

Ni hayo tu.

Yasinta Ngonyani said...

Asanteni ndugu zangu. Na Candy1 asante kwa kugundua kosa nililolifanya si unajua tena nadhani karibu wengu tunachanganya ri na li. Ahsante kwa kuona kosa hili ila sasa nimebadili.

Simon Kitururu said...

Kwa Wahindi kama nakumbuka vizuri ni Msichana anatozwa Mahari na Mvulana na sio kama Bongo.

Ila Bongo kuna maeneo Kuku tu anatosha halafu bomba la Totozi linaweza likanyanyasiwa hiyo mahari!:-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kuna jamaa yaangu kaoa mke, kalipisha mahali hadi sh milion1

anahasira, kazilipa lakini anasema kamnunua mke,.kwa hiyo baada ya ndoa, hataki uhusiano wowote na familia ya mkewe kwani amelipishwa kiasi cha kutosha.

mimi nikiombwa mahari zaidi ya laki2 za kibongo sitoi kwani sikotayri kumnunua mtu. itozwe ya utamaduni sio kununuana

mumyhery said...

kwangu hakuna cha fadhy, simon wala kamala kwa binti yangu nataka ng'ombe tena sasa hivi nachagua nataka ng'ombe wa maziwa na sio mmoja

chib said...

Kitururu, ha hah haaa

Anonymous said...

Am newkama in your blog, Sio sahihi kabisa,kwasababu kunakijana mmoja alimpenda binti tatizo lilikua mahari kutoka kwa wazazi,noamba wazazi waache kuuza wanawake.

Fadhy Mtanga said...

Mumyhery heshima yako (tena mamamkwe kuanzia leo)
Mi nakwambia sitoi ng'ombe wa maziwa wala nini. Ntampa mistari hadi ye mwenyewe atakubembeleza usipange mahari. Na jinsi umpendavyo nina hakika utamkubalia.

Bado nadhani Waswidi wana mfumo mzuri sana. Ningependa hata Bongo kuwe vivyo hivyo.

Ni hayo tu!

EDWIN NDAKI (EDO) said...

vita ya kacha..

Koero Mkundi said...

Mzee mkundi alishasema hataki Mahari, yaani anaozesha binti zake wote nikiwepo na mimi bure kabisa.
Ole wake mtu amnyanyase binti yake...!!!
atamtambua........

Mzee wa Changamoto said...

Kwani maana halisi ya mahari ni nini? Na wanini wengine walipiwe na wengine wasilipiwe?
Mie sijui kama nimetoa ama nitatoa lakini sibishani na ukweli. Na pengine ukweli waweza kuwa uongo maana hata wapokeao na kula mahari badhi yao hawakuchangia lolote katika malezi. Sijui ndio kuuzana? Lakini akishalipiwa unakuwa na nafasi gani kwake? Da Koero katangaza kuwa HAKUNA MAHARI lakini ni kwa kuwa haihitajiki ama kumkinga binti na manyanyaso? Lakini pia sio chanzo cha mabinti kuwa na kiburi wakijua kuwa wanaweza kurejea nyumbani wakati wowote?
Kulipa mahari kwaweza kumfanya mtu aangalie thamani ya alicholipia na kukithamini na lazima tukubali kuwa uwe umelipia mahari ama la, lakini mke ni THAMANI KUBWA ndani ya nyumba. Sasa ni bora kulitambua hilo ama la? Ila kulipia mahari kwaweza kumfanya mtu ajione KAMILIKISHWA HAKI MILIKI ZOOOOTE za mkewe na kumfanya afanyavyo maana amesha-pay off kile alichonacho. Utamfanya nini?
Lakini kutolipa mahari si ni kuonesha kuwa mmeamua a kukubaliana kuwa pamohja bila gharama yoyote? Ama kutolipa mahari ndio kule kuonesha kuwan mume (ama mke kwa wale kina nanii ambao mke anaoa) ni ubia na huna miliki naye?
Lakini kwanini tusilipe ama tulipe mahari?
Mnapendwa

Albert Kissima said...

Kulipa mahari ni utamaduni ambao hauna maana.Wazazi wengi wanachukulia mahari kama namna ya kujipatia kipato, ndio maana kuna wazazi wengine wanadiriki kupokea mahari kutoka kwa watu tofauti walionadi kuwa wanampenda mwanawao bila kujali mtoto wao anampenda yupi.

Kuna huu utamaduni wa harusi nao unanikera kupita maelezo.Mimi binafsi sifagilii kabisa utamaduni huu.
Hivi ingekuwaje badala ya harusi, ndugu, jamaa na marafiki wangekuwa wanawachangia wanandoa fedha za kuanzia maisha.
Matayarisho ya harusi yanapoteza wakati, fedha nyingi(ijapokuwa mara nyingi watu huwa wanaandaa harusi wakijua kuwa fedha ile itarudi)
Mbaya zaidi michango ya harusi kwa sasa imewekewa kiwango fulani, hili huwakandamiza sana wa kipato kidogo kwani wanalazimika kutoa la si hivyo watatengwa na jamii.