Tuesday, June 2, 2009

KISWAHILI

Mara nyingi huwa nakasirishwa kuona / kusikia watu wanatumia vibaya baadhi ya maneno ya kiswahili. Hapa nimechukua au nataka kutoa mfano haya maneno matatu. Karibu, Jambo na Habari

Karibu: Ni kuto kuwa mbali kwa wakati au mahali, kiasi cha kukadria. Lakini watu wengi wanaelewa zaidi karibu ni tamko litumikalo kuitikia hodi au wakati mtu anapokaribishwa au kupokewa mahali fulani.

Jambo: Watalii wengi wanafikiri wanaweza kiswahili, kusalimia wasemapo jambo hawajui kwamba Kiswahili sananifu hutamkwa hujambo/haujambo/hamjambo? kwani ukisema hivi anashindwa kuitikia sijambo. Si afadhali hata wangefundishwa kusema hali yako.....

Habari: Neno habari limekuwa linanitatanisha sana. Kama kawaida maneno mengi ya kiswahili yana maana mbili azu zaidi. (1) Habari ni melezo ya jambo fulani lililotokea, taarifa, ujumbe na ripoti.
2) Habari hutumika katika kuamkiana na kuulizana hali. Lakini inaonekena wengi hatuwazi sana tunapoongea hili neno litumikeje.

9 comments:

Unknown said...

Yasinta, umesahau neno la HAKUNA MATATA, wenzetu wazungu hulitumia sana kumaanisha neno NO PROBLEM.

Fadhy Mtanga said...

Mi si mtaalamu wa lugha ya Kiswahili, lakini katika pilika za kutafuta maarifa nimekutana nacho. Kwa mtazamano wangu, neno karibu halitumiwi vibaya. Kama yalivyo maneno mengi, kama ulivyolitaja neno habari, karibu pia lina maana zaidi ya moja.
Moja, kama ulivyoainisha, ni kinyume cha mbali.
Pili, nusura! Yaani jambo limenusurika kutokea.
Tatu, hutumiwa kukaribisha mtu, aidha agongapo mlango ama aoneshwapo pahala pa kuketi. Huyu aambiwapo karibu, huitikia, 'starehe!'
Nne, hutumika kumuaga mtu anaeondoka.
Tano, hii pengine ni maana mpya, mtu anaposhukuru jambo, huitikiwa 'karibu' kwa kuiga 'you're welcome' katika Kiingereza.
Lugha hukua kadiri ya wakati, mabadiliko ya kijamii, muingiliano wa tamaduni na uvumbuzi mpya.
Mfano wa kwangu uwe neno 'fisadi' maana ya neno hili imekuwa zaidi miaka ya hivi karibuni ikianzia Kenya. Kutokana na kukithiri kwa vitendo viovu kwa viongozi wetu, hususani ubinafsi na ubadhirifu neno ufisadi likapata mwelekeo mpya na wenye nguvu zaidi.
Nirudie, lugha hukua, kwa mtazamo wangu.
Ni hayo tu.

chib said...

Congrats

Albert Kissima said...

Kaka Fadhy,neno 'karibu' kwa mtizamo wangu, linapotumika kuaga, nadhani halitasimama lenyewe bali litakwenda pamoja na maneno kama "tena" yani "karibu tena" au .Nami naomba kukiri kuwa mimi si mtaalamu wa lugha hii adhimu ya kiswahili.

Hivi Compyuta kwa kiswahili fasaha inaitwaje?

Na Website?
Mouse ya kompyuta?

Tofautisha maneno haya,
mboga, kitoweo, mboga za majani.

John Mwaipopo said...

Wakenya ndio waliopotosha neno hujambo na kulirahisisha kuwa 'jambo'. Wazungu wanawasikiliza zaidi wakenya kuliko sisi. Wazugu ndio waliokuza 'jambo'

Kissima, 'mboga' ni mwenza wa chakula kikuu kama ugali na wali. Ni msindikizaji tu, lakini wa muhimu kweli. Hebu fikiri ugali bila mboga,

Kitoweo ni aina ya mboga inayotokana na viumbe hai kama ng'ombe, samaki, kitimoto (samahani kwa wengine) aghalabu kipikwe na mchuzimchuzi hivi ili maana halisi ya 'kutowezea' (kuloweka)itokee.

Mboga za majani ni anina ya mboga pia. Hizi hutokana na mimea kama kabechi, mlenda, majani ya maboga/maharage na kadhalika. Ila kuna baadhi ya watu kwa kuogopa kusema moja kwa moja kwa kufumba hivi)mboga za majani humaanisha 'bange'

upo hapo

Albert Kissima said...

Kaka Mwaipopo nimekupata vizuri na ninashukuru kwa maelezo yako.

Anonymous said...

@Mwaipopo. Kwa hisani yako hii lugha ya Wakenya hivi wakenya vile. Mbona huyasema ya Watanzania kupitia miziki yao kusema KIBOKO YAO? Wala si watanzania wote wanaosema hivyo. Unaposema wakenya tafadhali ainisha maana kwangu mimi ni sawa na kunitukana. Huu si uungwana hata kidogo. Mintarafu hoja hii ya "Wakenya hivi wakenya vile" nimewahi kumsikiya bwana mmoja kutoka Arusha akisema eti wakenya khaswa kutoka MOMBASA hawajui Kiswahili. Jamani Mombasa iweje hatukijui Kiswahili ilihali Kiswahili chenyewe kilijulikana mwanzo kutokana na miswaada tokeya Mombasa na Lamu? Ninakuomba kwa hisani yako, unaposema Wakenya hivi au Wakenya vile wala si tabiya nzuri! Je watanzania wote ni magwiji wa Lugha ya Kiswahili!

Anonymous said...

@Mwaipopo. Kwa hisani yako hii lugha ya Wakenya hivi wakenya vile. Mbona huyasema ya Watanzania kupitia miziki yao kusema KIBOKO YAO? Wala si watanzania wote wanaosema hivyo. Unaposema wakenya tafadhali ainisha maana kwangu mimi ni sawa na kunitukana. Huu si uungwana hata kidogo. Mintarafu hoja hii ya "Wakenya hivi wakenya vile" nimewahi kumsikiya bwana mmoja kutoka Arusha akisema eti wakenya khaswa kutoka MOMBASA hawajui Kiswahili. Jamani Mombasa iweje hatukijui Kiswahili ilihali Kiswahili chenyewe kilijulikana mwanzo kutokana na miswaada tokeya Mombasa na Lamu? Ninakuomba kwa hisani yako, unaposema Wakenya hivi au Wakenya vile wala si tabiya nzuri! Je watanzania wote ni magwiji wa Lugha ya Kiswahili? Watanzania wengi, sio wote, hawawezi kutamka DHA. Hawatafautishi kati ya R na L. Mtu huitwa LAMAZANI badala ya Ramadhani, husemwa AFAZALI badala ya AFADHALI. Neno RUNINGA ambalo asili yake yajulikana, jamaa husema LUNINGA nk nk.

obat vimax said...

vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg