Sunday, June 28, 2009

MATUNDA NI MUHIMU KATIKA MWILI LAKINI BEI MBAYA MNO!!!!


Mti wa matunda damu. Matunda haya hapa Sweden moja unalipa 12kronor ni sawa na 2000Tsh
Halafu kula embe hapa embe moja inauzwa 9.90kronor ni sawa na 1584Tsh, pia papai bei yake ni kama 20,000Tsh. kwa hiyo ndio maana watu wengi wakija Afrika wanakula sana matunda kutokana na bei kuwa nafuu.

10 comments:

Bennet said...

Hivi nikikutumia kwa kutumia email yatafika maana sasa hivi kuna mapapai, machingwa, maparachichi, maembe na mananasi kiasi

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Dada Yasinta: Kwa nini matunda ni ghali namna hiyo hapo Sweden? Nataka tu kujua.

Faith S Hilary said...

Duh! That sounds expensive..
...ila huku matunda yako reasonable priced ila mpaka yakifika MABOVU! hehe

Nicky Mwangoka said...

Aaaa Yasinta unanikumbusha mbali,we acha tu maana haya tulikuwa tukitumia kupikia mboga badala ya nyanya kule kwa bibi.Nimefurahi sana.Tulikuwa tukiyaita "matunguja" hahhhahaa

mumyhery said...

Bennet huku tuliko embe ni mapapai ni hadithi tu ukipata ni yale yaliyo sindikwa na hayana ladha nzuri kwani yanakuwa jamejazwa syrup au unywe juice

Simon Kitururu said...

Yasinta hayo matunda kwenye picha sijayaona siku nyiiiingi!

:-(

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza napenda kuwashukuru wote kwa maoni yenu. Ndungu zangu ni hivi hapa yana bei kwa vile hayalimwi hapa yanasafirishwa toka mbali hii ndio sababu yana bei sana.

Simon Kitururu said...

Yasinta usisahau kuwa na kodi ni kubwa Sweden na inamchango wake kwenye bei.

Yasinta Ngonyani said...

sante kwa hiyo Simon!

Mzee wa Changamoto said...

Mimi bei si shida sana kama ladha. Unakula kitu kwa kulazimisha ladha ya hisia uliyonayo toa home. Yaani!! Kila kitu kimepitia kwenye kemikali na kisicho na kemikali basi ni balaa. Pengine Da Yasinta unanunua organic ndio maana. Tofauti ya bei huwa kubwa saaana. Mfano, nyama ya ng'ombe waliochomwa masindano ya kukuza ni kama sola 4 kwa paundi wakai yule kama wa Babake Mubelwa ni zaidi ya dola 10 kwa uzito huohuo.
Labda ukijiuliza sababu utapata jibu.
Blessins