Tuesday, June 9, 2009

KWELI HII NI HAKI?

Haya na maoni ya msomaji kwa picha hizo hapo chini.

Hii niliwahi kusikia imetokea Uganda mabapo mzee mmoja, alikuwa akimlazimisha mke wake anyonyeshe watoto wa mbwa ambaye mama yao alifariki. Kwani kabla mama yao hajafariki alikuwa na ng'ombe ambao walikuwa akitoa maziwa kwa ajili ya hao mbwa. Na hao ng'ombe huyo mzee alitoa mahari ya huyo mama hivyo mbwa wakawa hawana sehemu ya kupata maziwa ndipo yule baba akawa anamlazimisha mke wake awanyonyeshe hao mbwa. Kwani yeye alikuwa ni muwindaji, na hao mbwa walikuwa wakimsaidia katika shughuli zake za uwindaji. Lakini watoto wa huyo mama mmoja alifariki kwa ugonjwa ambao unakisiwa ni kichaa cha mbwa, na yule mmoja aliebaki nae alianza kukuhoa kama mbwa, na mama chuchu zake zilikuwa na madonda kwa ajili ya kung'atwa na mbwa wakati akiwanyonyesha, lakini kwa india ni mambo ya kawaida. Ikiwa ni pamoja na kuuza viungo vya mwili na kupandikizwa mimba za watu wengine kwa ujira.

Hapa bado sijaelewa yeye huyo mzee alijisikia raha gani. Na pia kweli alimpenda mke wake na watoto au aliwapenda zaidi mbwa. Kumsaidia kuwinda, labda wenzangu mnisaidie hapa. Kwali kumlazimisha mkw wako knyonyesha mbwa hivi wanaume wanakiri wao ni akina nani kuwatesa wanawake kiasi hiki?

2 comments:

chib said...

Usijumuishe kuwa wanaume wote wana akili sawa na vichaa wachache waliopo!!

MARKUS MPANGALA said...

Siku zote wakati wote nimekuwa nikiwaeleza wanawake kuwa kwamba huenda tabia yangu haiwakilishi tabia za wanaume wote waliopo duniani. Lengo langu ni kuondoa dhana kwamba imani wanaume ni watu wanaofanana tabia na kufanya mambo kwa mlinganyo.
Daima tuweke mpaka wa kuamua na kufikiri, mpaka wa kuhoji na kuuliza au kudadisi. Inawezekana huyo aliyemlazimisha mwanamke ni kichaa kweli lakini hajathibitishwa ni kama yu kichaa- ingawa sikubalani na tabia yake.

Hata hivyo jukumu la kutatua haya mambo ni lazima tujiulize sana. Je hiki kitu kinachoitwa mfumo dume ni nini? Ni kweli adui wa wanawake ni mwanaume? Ingekuwa vipi wanawake wangekuwa peke yao hapa duniani?

Labda awali sikuelewa ndugu zangu waislamu kwanini hawataki wanawake katika mazishi, ila sasa najua kiasi fulani cha mambo.

tunatakiwa kupigana kwa pamoja dadangu, lakini tupigane huku tukijua adui yetu ni nani. ni hayo tu, nawaza tu mkuu, haya tutaonana mida basi kama kawaida.