Monday, June 1, 2009

JE? NI VIGUMU KUISHI BILA NGONO?

Wengi tunajua/pia tunajadili ukimwi na ngono, lakini tunahitaji kukumbuka kuwa sio waTanzania wote ama binadamu wote ni hivyo. Cha muhimu ni kuelewa kuwa ugonjwa huu unaua binadamu, na kwamba, hawa binadamu wanatokea katika kila sekta ya maisha, wanadini, wapagani, wasio na elimu, wenye elimu, wamjini, wanavijiji, nk.
Je? kuna ubaya gani kuwaelimisha wengine kuhusiana na matumizi ya ndomu?

Tukumbuke ya kwamba baada ya Hawa na Adam kula lile tunda baya, sote tulizaliwa madhambini, na tunashawishika kirahisi. Yaani, hata Hawa na Adam , ghafla waligundua ya kuwa wako uchi, nadhani mle bustanini kulikuwa kuzuri na kulikuwa na hewa bora yaani jua lilikuwa haliwachomi, majani hayakuwakata.Walipofukuzwa ndio walilazimika kuvaa nguo kwa sababu ya jua kali, mavumbi, miiba nk. Hakuna aliyewaamrisha kuvaa nguo.

Ngono inashawishiwa maishani kwa mbinu nyingi ambazo ni vipofu tu wasioziona. Katika magazeti, mavazi, sinema, hadithi za waliojaribu, umbea nk. Ni kama vile Hawa na Adamu, walivyoshawishika kula lile tunda hata walivyojua Mungu wao aliwakataza, lakini sisi wengine tunashawishika kirahisi kula hili tunda liitwalo "ngono". Wote tunajua tukishalionja tunda hata yeyote akikuambia "basi acha" wengi tunacheka ana kushangaa? Hii in kama vile mtoto akishaonja pipi, halafu ategemewe kutotamani pipi mbeleni.

Pipi zitakuwepo duniani kwa miaka mingi, vishawishi vya ngono vitakuwepo duniani kwa miaka mingi. Hii ndio sababu tunahitaji kuelimishwa kuwa pipi si nzuri kiafya. Lakini pia tunahitaji kuelimishwa kuwa wale watakao tamani basi wale nyingi na wasisahau kupiga mswaki. Naamaanisha, ujumbe wa kuacha ngono uambatane na ujumbe wa kupunguza kufanya ngono na watu wengi NA elimu ya kutumia ndomu.

5 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sikuelewi vizuri mrembo. unamaanisha ngono ni mbaya? kwani we unafanya hufanyi? twambie kwa nini unafanya na labda uwe wa kwanza kuacha. tunaweza tu kuishi lakini sijui kama Adam na hawa walifanya ngono! wao walikula mti wa kujua Mema na mabaya na sio ngono au? mimi sio mkristo

takisomike

chib said...

Ujumbe wako ni mzuri kama njia ya kuwafanya watu wajitambue na kuwa na breki kwa ngono isiyo ya lazima na pia isiyokuwa salama

Faith S Hilary said...

Well said dada Yasinta ila maoni yangu ni hivi,

Binadamu hata umwambie nini lakini atafanya tu ili aone kitatokea nini (humans are very funny creatures) japo anajua what's gonna happen , next. Mfano mmoja kuhusu topic hii, huku UK kisheria unarahusiwa kufanya mapenzi kuanzia umri wa miaka 16 ila bado watoto hata wa miaka 11 wanafanya, it doesn't matter how but they still do it no matter what the consequences.

Sex will never end, there are advantages and disadvantage of it but a human being will still be a typical human being.

Mzee wa Changamoto said...

Mmhhh!! Wacha nijifunze tuu. Asanteni wachangiaji

Anonymous said...

du naona msisitizo wa kutumia viffanyio hapo! mhh hivi kuna ukimwi au ni ujanja ujanja wa wajanja wachache kuleta hofu duniani? mhh imagine dunia bila ukimwi, si itakuwa crisis nyingine hiyo!! ni mtazamo tu!!!