Saturday, June 27, 2009

MUZIKI NI MOJA YA KITU MUHIMU SANA KATIKA MAISHA:- HAYA NGOJA LEO TUMSIKILIZE SI MWINGINE TENA BALI NI MARLWA - Pii pii(missing my baby)

3 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Ni kweli. Jumatatu ya wiki hii nilitazama kipindi kimoja kinaitwa "Music and Your Brain" na kilikuwa kipindi chenye kuhabarisha kweli kuhusu faida za muziki. Mbali na faida zake nyingine wanasayansi sasa wameshathibitisha kwamba muziki unasaidia ubongo kukua na kuimarika zaidi hasa katika maeneo muhimu yanayoshughulikia utambuzi, uundaji wa dhana dhahnia n.k. Ndiyo maana vingunge wengi wa sayansi (mf. Albert Einstein) na wengineo walikuwa ni wanafunzi wa muziki na walikuwa wanacheza angalau ala moja ya muziki. Hitimisho: muziki una faida kubwa katika kukua na kupevuka kwa ubongo. Hapa nakubaliana nawe moja kwa moja!

Mzee wa Changamoto said...

Mmhhhhhh! Swadakta. Nimeburudika na (naamini) nimenufaisha ubongo kama alivyosema Profesa Matondo. Asante kwako Da Yasinta kwa burudani na Profesa kwa kututanabaisha kuhusu faida za muziki ambao wengine tunausikiliza kila uchao lakini hatujui faida zake za ndani na uhusiano wake na "chaji" za ubongo.
Baraka kwenu

Nicky Mwangoka said...

Huyu kaka yupo makini, sauti imetulia sana, yaani unapata mantiki ya wimbo kwa sababu ya utulivu wake. Big up Marlow na Asante Da'Yasinta