Saturday, June 20, 2009

UJUMBE WA LEO:-WANAWAKE UGHAIBUNI (SWEDEN)

Kama waSwahili wasemavyo tembea uone, basi nimeona.
Kwani nakumbuka, pia najua ya kwamba wanawake Afrika ni wanyeyekevu mno kwa waume zao.

Lakini kwa muda nilioishi hapa Sweden. Nimeona ni kinyume, yaani nikinyume kabisa. Hapa ni wanawake ndio wanaamua /maamuzi yote ya ndani ya nyumba. (Wana amri sana kwa waume zao)

Nategemea uasili wangu utakuwa kama nilivyofunzwa yaani sitaambukizwa na hali hii. Kwani jambo hili limesababisha hapa Sweden kuwa na asilimia kubwa ya kupeana talaka
Au nisema wanawake wengi wanaona

Kitu kingine kwamba waswidi wengi wanaona sababu kubwa ya kuachana ni kwa sababu hakuna ubaguzi, yaani kikazi wanawake na wanaume. Wanawake wengi wanafanya kazi na wana mshahara ambao unatosheleza, Pia hata kama hawafanyi kazi kuna misaada mingi wanawake wanaweza kupata kutoka katika serikali ya kijiji kwa mtindo huu ndio maana wanaona hawawategemei sana waume zao kwa kuweza kuishi na kupata chakula.

5 comments:

chib said...

Kweli tembea uone!!

Mzee wa Changamoto said...

kwa ufupi ni kuwa wanawake wa ki-Swid wamepoteza maana halisi ya neno ama kitu ndoa. Maana ndoa ni zaidi ya amri ama ni zaidi ya msaada ama ni zaidi ya nani anatoa nini na kufanya nini ndani ya nyumba.
Kama hizi ni kati ya sababu za kuwafanya waendekeze talaka, basi wanahitaji darasa kuhusu ndoa. Lol

Anonymous said...

Kama wanawake ndio wana sauti katika familia zao ni nani anayetoa posa kati ya mwanamke na mwanaume huko Sweden? kwa ufupi nimependa ujumbe wa leo ila sijui wanaume wenzangu huko wanaionaje hali hiyo?

Francis said...

www.francisgodwin.blogspot.com said...