Thursday, June 14, 2012

HUU KWELI NI UUGWANA? AU AKINA MAMA TUNA MOYO WA KIKATILI HIVI KWELI?


Nimesoma habari hii na kuona picha hii nimepatwa na maumivu yasiyosemekana. Na nikaanza kuwafikiria  watu wanaofanya kila mbinu ili kupata watoto/mtoto halafu wengine wanatupa. Yaani nimeguswa na habari hii si kawaida. Nikaanza kuwa kubeba mimba miezi 9 maumivu yote ya kujifungua halafu anamtupa mtoto. Kama haku/hawataka watoto/mtoto kwa nini kutafuta mtoto? Mbona kuna vizuizi? Malaika kama huyo hana kosa... nashindwa kuendelea kuandika. Soma hapa chini...
----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Wewe na mie tuchunguze vizuri photo hiyo, ni dampo la takataka eneo moja huko Mtwara,lakini ukichunguza sana utaona ni uchafu uliyokuwa pamoja na binadamu,binadamu aliyezaliwa na mwanamke.
Ni kitoto kichanga kilichozaliwa na mama huko Mtwara na kukitupa kwenye lindi la mikusanyiko ya kila aina ya uchafu,Hivyo wimbo wa nani kama mama una maana yoyote kwa akina mama wenye moyo wa ukatili kama huyo? .je ni kitu gani kilicho msibu mama huyo hadi kufikia kufanya kitendo hicho kiovu.( Source Mitandao ya Kijamii ) Picha na habari nimeipatahapa

8 comments:

ray njau said...

Hakika huu ni ukatili mkubwa.Sijapta maneneo sahihi ya kuelezea hisia zangu za uchungu............!!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray mwenzio nimeishia kulia... Mau yoyo! halafu yaani nimepatwa na maumivu ya tumbo na kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu...Malaika kama huyo jamani kweli akina mama....

emuthree said...

Duuh, raha twapenda, lakini matunda yake hatuyataki. Najiuliza kwanini alivumilia miezi tisa,halafu ashidwe kulea, .....hii ni laana,...!

Rachel Siwa said...

Inatisha,ndiyo ya Walimwengu!!!

Interestedtips said...

mimi mwenzeni hii issue siku ya leo kila nikiwaza naumia sana, yaani nawaza huyu mtoto ana hatia gani hadi afanyiwe hivi. Mungu atuepushe na majanga haya

Yasinta Ngonyani said...

emu3!Hata mie nimejiuliza mara kadhaa kulea mimba na mtoto ipi ni kazi...sijui aliweza vipi kumtupa huyo malaika na yeye kuondoka tu na kuendelea na safari..Halafu najiuliza sijui mtoto huyo alimzalia hospitali au alikuwa pekeyake. Na je alikuwa ameshakufa?

Rachel/Kachiki! Yaani inatisha mno naona ni mwisho wa dunia unakaribia..
Ester! mwenzio kwanza nilishindwa kuangalia nilipoona. Na kutwa yote sijala. Sikujua kama wanawake tu wakatili hivi...na aliwezaje kuondoka hapo bila hata huruma ...yaani naishiwa hadi maneno...

Mija Shija Sayi said...

Labda alikuwa ni mwanafunzi, na akaogopa kibano cha nyumbani.

Kuna mambo mengi sana ambayo sisi wananchi wenyewe tunachangia watoto kutupwa wanapozaliwa, mara nyingi tunawasimanga sana wazazi wanafunzi, au ukali wetu unakuwa hauna kipimo kiasi kwamba mzazi anafikia hatua hiyo ili kujisalimisha na walimwengu.

Cha msingi ni walimwengu kuanza kuwa karibu na watoto wao, tuwape elimu nzuri kuhusu uzazi na njia za kujiepusha na wadanganyifu, na pia kwa bahati mbaya ikitokea mimba basi tuwasapoti vinginevyo haya yataendelea kuwepo tu.

Nimeongelea kwa upande wa wanafunzi...

Mwenye masikio na asikie...

Yasinta na wadau wote mbarikiwe sana.

Penina Simon said...

akina mama wengi wana roho mbaya tena akijaliwa kuwa nayo hiyo mbaya inakuwa mbaya sana tena hatari,
tuombeane Mungu atupe moyo wa nyama na tuwe na hofu ya Mungu.