Thursday, December 15, 2011

JE? UMEWAHI KUWASHWA NA UPUPU?

Leo nimekumbuka siku moja nilikuwa navuna mahindi halafu nikajisikia mwili wote unawasha. Kumbe niligusa UPUPU bwana, wacha nianze kurukaruka, mama akachukua majani ya mihogo/kisamvu na kunipikicha pikicha na muwasho ukatulia. Je? wewe umewahi kugusa upupu na kisha kupata muwasho kama huu? na kama ndiyo ulitumia nini ili kupunguza muwasho?

13 comments:

Baraka Chibiriti said...

Dada Yasinta....acha kabisa habari hii ya Jamaa huyu Upupu, ni balaa si mchezo...mziki wake mkubwa mno. Yaani hata kusikia tu naogopa...maana nilishaonja joto ya jiwe huko vijijini nilipokuwa nikifanya kazi za kusaka maji. Hadisiwa tu, usiombe yakukute ya upupu....utajikuna mpaka kucha ziishe kabisa!

Baraka Chibiriti said...

Kusikia tu Mpaka mwili wangu umenisisimuka kabisa!

Unknown said...

Baah ana wewe kukunoga uchokozi kweli!! Basi ilikuwa miaka hiyooo enzi hizo naishi na bibi yangu Binti Ndembo (RIP) huko Masasi.. vichaka vyote vya kuzunguka nyumba ilikuwa ni upupu mwingi... kuwashwa ilikuwa kawaida lakini dada Yasinta sikuzoea hata siku moja... Swali: umeshawahi kula upupu???

ISSACK CHE JIAH said...

Dada usitaje habari hizo za upupu HICHO Ni chakula cha watu kwani mulize mrope atakujulisha utamu wake lakini kwa kuwasha kama ukikutana nao hautatamani kuula ila ni mtamu sana kule kwa wajomba zangu wanauita maharage ya zambia kwani huwa wanachanganya na kachumbari duu wee sitaki kumaliza utamu ila unawashaa ile mbaya
che JIAH

Unknown said...

Che Jiah... LOL!! habari za upupu na kachumbari achana nazo bwana... utamu wake hapo ni kiboko.... muulize Mzee wa Changamoto... toka Kagera hadi Ndanda Sec.. mpaka leo anasimulia...

ISSACK CHE JIAH said...

Ukiwaswa na upupu dawa yake ni majivu bila wasiwasi huwa unatulia ila ulaya hakuna upupu kama upo unaitwa upupu ulaya huwa hauwashi hata ukiuona ushike tuu si kama ule wa kwetu kunyumba kuchijiji ,kuna aina mbili za upupu upo ambo hauwashi na huo ndiyo unatumika sana kwa kuliwa na wa pili ni huo wa kuwasha ni pori yaani upo mdogo na mkubwa ipo siku nitafafanua aina za upupu kwetu kule upo mwingi

ISSACK CHE JIAH said...

Ukiwaswa na upupu dawa yake ni majivu bila wasiwasi huwa unatulia ila ulaya hakuna upupu kama upo unaitwa upupu ulaya huwa hauwashi hata ukiuona ushike tuu si kama ule wa kwetu kunyumba kuchijiji ,kuna aina mbili za upupu upo ambo hauwashi na huo ndiyo unatumika sana kwa kuliwa na wa pili ni huo wa kuwasha ni pori yaani upo mdogo na mkubwa ipo siku nitafafanua aina za upupu kwetu kule upo mwingi

ISSACK CHE JIAH said...

NI kweli ndugu yangu mrope subiri bethdai yake mtani wetu dada yetu
mwenye nyumba hii ikifika mpelekee ule upupu ulaya si ule wa masasi hapana jitahidi nitakuletea mbegu upande uko ulaya na umtumie dada yangu huyo aliyeuliza kama upupu tunaujuwa,ila mimi nitantumia ile wanaita YEILA kule nyumbani siku hizi wamepewa jina WAJUMAPILI umenipata hapo huyo wa kagera mwache akumbuke akiwa NDASECO mpe pole maana alijuwa siri ya mtungi je akuwahi kula supu yetu?

ray njau said...

Mambo ya upupu tena.Mhhhhhhhhh!!

Rachel Siwa said...

Sijawahi kuwashwa na UPUPU,pia sikujua kama ni mboga, kweli nimejifunza kupitia hapa,Baraka kwa wote!

LILY said...

dada Yasinta umekose kuandika au ndio unavyoitwa huo wa kuliwa?

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii kuwashukuruni wote mnliopita hapa na pia napenda kuwaambia kuwa wiki ijayo nitawaambieni tofauti ya UPUPU WA KUWASHA NA ULE UPUPU WA KULA (MANGATUNGU) YANAITWA kule nilikokulia mimi. Msikonde ..ruksa kuendelea kusema lolote.

MWITA HARDSON said...

POLE SANA KWA KUWASHWA NA UPUPU NDUGU YANGU,HERI YA MWAKA MPYA KWA WOTE JAMANI