Sunday, May 26, 2013

LEO NI SIKU YA AKIMNA MAMA (MORS DAG)


Hapa Sweden leo ni siku ya akina mama duniani. Nasi leo tumeamua kumpongeza mama yetu mpendwa ktk blog yake ni sisi Camilla na Erik. Tunampenda sana mama yetu hasa akiwa na hasira, huwa tunapata kila kitu tutakachotaka/omba.( kwa niaba ya mama)
Ok, basi nami nimepata nafasi ya kusema machache ni kwamba. Najua sehemu nyingine siku hii imeshapita ila hapa Sweden ni leo. nami napenda kuwapa pongezi akina mama wote duniani bila kumsaau mama yangu. NAWAPENDA AKINA MAMA WOTE DUNIANI.NA TUTAFIKA TU.

5 comments:

Anonymous said...

Hongera Dada Yasinta na wamama wote duniani! Tunasubiria leo mapishi kwa hamu utakayowapikia hapo nyumbani mana ni siku yako, au leo unapumzika baba na watoto ndio wapishi? Kama utapika madiko diko tuwekee hapa angalau tule kwa picha tu, mana nasikia njaa! Siku njema.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante usiye na jina. Leo ni siku yangu hakuna kupika nitapikiwa...yaani raha kweli:-)

Anonymous said...

Hongera kupikiwa nilidhania utaingia kupika. Tunashukuru kuona keki nzuri ya Dada Camilla. Na hongera kupata zawadi kem kem.

Yasinta Ngonyani said...

Siku moja kustarehe si mbaya...nilifurahia kila dakika...ndiyo keki ilikuwa tamu sana. Bahati mbaya ulishindwa kuja:-)

mumyhery said...

Shukran na Hongera sana