Saturday, May 4, 2013

AINA ZA UFUJAJI..HII NI MOJA YA AINA YA UFUJAJI,,UFUJAJI WA KIROHO...

Ni pale ambapo mpenzi anatumia dini au imani ya mwenzake kumwendesha. Kuna wakati anabaini kwamba, kwenye imani ya mpenzi wake kuna kipengele anachoweza kukitumia kumkandamiza mwenzake, ambapo hukitumia.
Kwa mfano, kama imani ya mwenzake inasema mwanamke amtii mumewe, kipengele hicho kitapindwepindwa na mpenzi hadi mfujwaji akubali anayotaka mfujaji, kupitia kipengee hicho.
Lakini pia kumzuia mpenzi kuchiriki kwenye ibada au maombi au huduma yoyote ya imani yake. Kuzuia huku kunaweza kuwa ni kwa moja kwa moja au kwa mbinu za kulaghai na kukashfu. Mara nyingi hata hivyo, kashfa, matusi , kebehi na matumizi ya nguvu hutumika katika sula hili.
Kuna wakati watoto hulazimishwa kufuata imani ambayo mzazi mmoja haitaki na ambayo pengine haikuwa imani ya yeyote kati ya wapenzi wawili. Mpenzi mmoja kabadili  dini wakiwa tayari kwenye ndoa, halafu analazimisha watoto kufuata hiyo dini yake mpya, bila makubaliano na mwenzake ambaye yeye hajabadili dini.
Kuna mkazi mmoja wa Magomeni Mwembechai ambaye aliwahi kuja kwangu, akilalamika kuhusu ndoa yake na mumewe. Alisema, mumewe ameingia kwenye imani mpya. Mume huyo hurejea nyumbani usiku saa tano au sita. anapofika hapo nyumbani huanza kuimba kwa kelele akitukuza imani yake na Mungu.
Mume huyo huwaamsha watoto na kuwataka waimbe usiku huo wa saa tano au sita, akimtaka mke wake naye kujiunga nao. Mke yule aliniambia kwamba, anapojaribu kukataa au kuwatetea watoto kwamba, inabidi walale kwaajili ya kuwahi shule kesho yake, mume huyo humtukana kwa kumwita, ibilisi, mpottevu, mtu wa mataifa, mlaanifu mwenye mapepo wachafu wa ujeuri na kashfa za mataifa, mlaanifu mwenye mapepo wachafu wa ujeuri na kashfa za matusi ya nguoni.
Hii ni aina ya udhalilishaji kupitia dini au imani, ambao ni udhalilishaji wa kiroho. Imani inatumika kutoka maumivu kwa mwingine,
INATOKA KATIKA KITABU CHA MAPENZI KUCHIPUA NA KUNYAUKA....

3 comments:

ray njau said...

Hapa kuna changamoto ambazo ni lazima kila upande ukubali kuwajibika kwa mwingine kwa kuwa ndoa ni mkataba wa hiari kati ya watu wawili wanaoamua kujenga maisha na mafanikio ya pamoja kwa ridhaa njema.

Yasinta Ngonyani said...

Hakika katika maisha kuna changamoto nyingi . Ila hii ya ndoa ni kiboko...hivi kwanini inakuwa hivi?

ray njau said...

BIBLIA haisemi kuwa ndoa ni mpango rahisi. Mtume Paulo aliongozwa na roho ya Mungu kuandika kwamba wenzi wa ndoa wangelazimika kupambana na “matatizo ya kila siku.” (1 Wakorintho 7:28, Today’s English Version) Lakini mume na mke wanaweza kufanya mengi kupunguza matatizo yao na kuzidisha furaha ya mmoja na mwenzake.