Wednesday, May 1, 2013

SIKUKUU YA WAFANYAKAZI ..MEI MOSI!!!

Mwenzenu nina swali hapa:- Hivi Wafanyakazi ni akina nani? Wakulima akina nani?...Na wafanyabiashara ni nani?.Maana katika akili yangu naona kila kitu ufanyacho na kutoka jasho ni kazi. Naomba tujadili kwa pamoja hapa...JUMATANO YA MEI MOSI IWE NJEMA.....KAPULYA

4 comments:

Kiu ya Haki said...

Dada umemsahu na Mfanya biashara.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa kunikumbusha , kiu ya haki ngoja niingia na kuongeza.

Mija Shija Sayi said...

Yasinta hizi ni Concrete na Abstract meaning..
Inabidi ziwepo ili kutofautisha mambo, kwa sababu ukiangalia kwa undani mambo yote duniani ni kama kitu kimoja....hivyo kuzuia kuleta mkanganyiko ndio maana kukawa na abstract na concrete concepts..

Ni hayo tu kwa leo head prefect...

ray njau said...

Kwa ujumla kila sekta ni kazi tuna sababu nzuri ya kutafakari ili tujue mfanyakazi ni nani hasa?