Friday, May 24, 2013

MAISHA YA NDOA:- MKE NA MUME!!

Nipo kazini mara nasikia simu yangu ya mkononi ujumbe ukiingia, nachukua kuangalia ni nani na nini..nakutana na ujumbe huu na maagizo :- Kuwa  "wape wanandoa wote unaowafahamu ujumbe huu. Mungu na  awatie nguvu!! Ameeeen....!!" Na kwa vile najua wengi ninaowafahamu wanapita hapa nikaona itakuwa njia nzuri kuweka hapa...na ujumbe wenyewe ni kama ifutavyo:-
"Ukiona mko vizuri kwenye ndoa, Usimsifu mumeo/mkeo, Endelea kumtukuza Mungu na kuweka maombi ya akiba. Usitoke bila KUMWOMBEA mkeo/mumeo.
Jifunze pia kumwelewa mwenzako na kutokuuona udhaifu wake kama sababu ya wewe kumfanyia mabaya. Zungumza naye, mtie moyo, mshauri katika usiyoyapenda, mweleze uliyonayo.
Ondoa maswali nafsini mwako. Pata majibu sahihi kutoka kwake. KUMBUKA NI NYAKATI ZA MWISHO. Taasisi ya shetani isiyotaka ichanue ni NDOA. Ikiharibika familia nayo inaharibika. TAFAKARI"....IJUMAA NJEMA NA MWANZO MWEMWA WA MWISHO WA JUMA!!!

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nukuu..."Ondoa maswali nafsini mwako. Pata majibu sahihi kutoka kwake. KUMBUKA NI NYAKATI ZA MWISHO. Taasisi ya shetani isiyotaka ichanue ni NDOA. Ikiharibika familia nayo inaharibika" mwisho wa nukuu..Hivi ni kweli NYAKATI ZA MWISHO?

ray njau said...

“Kamba yenye nyuzi tatu haiwezi kukatika upesi.”—MHU. 4:12.

BAADA ya kuumba mimea na wanyama, Yehova Mungu alimuumba mwanadamu wa kwanza, Adamu. Baadaye, Mungu alimfanya Adamu alale usingizi mzito, naye Mungu alitumia ubavu mmoja wa Adamu kumfanyia msaidizi mkamilifu. Adamu alipomwona mwanamke, akasema: “Mwishowe huyu ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu.” (Mwa. 1:27; 2:18, 21-23) Yehova alifurahishwa na kazi hiyo ya uumbaji, naye akamuunganisha mwanamume na mwanamke wa kwanza katika ndoa na kuwabariki.—Mwa. 1:28; 2:24.
Inasikitisha kwamba baada ya muda mfupi tu mpango wa ndoa ulioanzishwa na Mungu ulishambuliwa. Jinsi gani? Roho fulani mwovu, ambaye baadaye aliitwa Shetani, alimdanganya Hawa ale kutokana na mti mmoja tu ambao wenzi hao wa ndoa walikuwa wamekatazwa. Muda mfupi baadaye, Adamu aliungana na mke wake kupinga haki ya Mungu ya kutawala na kukataa mwongozo wake mzuri. (Mwa. 3:1-7) Yehova alipowauliza wenzi hao wamefanya nini, ilionekana wazi kwamba tayari uhusiano wao ulikuwa na matatizo. Adamu alimlaumu mke wake, akisema: “Mwanamke uliyenipa awe pamoja nami, alinipa tunda kutoka katika ule mti nami nikala.”—Mwa. 3:11-13.
Katika karne zote tangu wakati huo, Shetani ametumia mbinu mbalimbali za ujanja kusababisha mgawanyiko katika ndoa. Kwa mfano, nyakati nyingine amewatumia viongozi wa dini kuendeleza maoni fulani kuhusu ndoa ambayo hayapatani na maandiko. Viongozi fulani Wayahudi walipunguza uzito wa kanuni za Mungu kwa kuwaruhusu waume kuwataliki wake zao kwa sababu ndogo-ndogo kama vile kutia chumvi nyingi mno katika chakula. Lakini Yesu alisema: “Mtu yeyote anayemtaliki mke wake na kumwoa mwingine, ila kwa sababu ya uasherati, anafanya uzinzi.”—Mt. 19:9.
Shetani angali anajitahidi sana kuvunja ndoa. Ndoa za watu wa jinsia moja, wanaume na wanawake wanaoishi pamoja bila kufunga ndoa, na talaka zinazofanywa kwa sababu ndogo-ndogo ni kati ya mambo yanayoonyesha kwamba anafanikiwa sana. (Soma Waebrania 13:4.)

Anonymous said...

Ni kweli hizi ni nyakati za mwisho dada Yasinta. Ishara hizi zinadhihirisha yaliyoandikwa kwenye Biblia. Mungu atusaidie katika ndoa mana yote yaliyoandikwa ni ukweli mtupu. Ndoa za sasa jamani tunamhitaji sana sana Mungu,kwani hazikai zinavunjika shauri ya ugomvi, kutoelewana mume na mke! Yaani sijui huwa nasema heri walioolewa na wazungu wana raha, dada Yasinta ´nifahamishe kama niko sawa au vipi, mana kuolewa na hawa wenzetu watanzania kwa siku hizi mh ni mizigo sana! Mungu atusaidie.

Mija Shija Sayi said...

Ameen..!!

Yasinta Ngonyani said...

Ndoa ni ndoa jamani hakuna tofauti cha muhimu ni kwamba kweli mnapendana kwa dhati? Na je mnawasilina kama mke na mume? Na kusikilizana

Anonymous said...

0753200267