Wednesday, May 8, 2013

UJUMBE WA LEO NI HUU:- MAISHA NI ZAWADI!!

Leo kabla ya kusema neno baya, mfikiria mtu ambaye hawezi kusema.
Kabla ya kulalamika kuhusu ladha ya chakula, fikiria mtu ambaye hana kitu cha kula. Kabla ya kulalamika kuhusu mume wako au mke wako, fikiria mtu ambaye amliliaye Mungu kwa ajili ampe rafiki. Leo kabla ya kulalamika kuhusu maisha. Fikiria mtu ambaye alikwenda mbinguni mapema mno amekufa mapema mno. Kabla ya kunung'unika kuhusu umbali gani unaendesha gari lako, fikiria mtu ambaye anatembea umbali huo kwa miguu yake. Na wakati wewe ni mchovu na ulalamikapo kuhusu kazi yako, fikiria wale wasio na ajira, walemavu, na wale ambao wanataka wangekuwa na kazi kama yako . Na wakati mawazo yanakutawala na kukufanya uwe na huzuni, tabasamu na ufikiri. Wewe ni hai na bado upo.
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!! SIKU NJEMA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA.

13 comments:

Anonymous said...

Dada Yasinta yani leo umependeza sana sana. Nimependa sana muonekano wako wa leo au kila siku uwe unavaa hivyo?!!!!!!! Jamani rangi ya mwili yote imebadilika mana umekuwa mweupe sana sana, au ndio mabadiliko ya hali ya hewa hayo? Kwa kweli nina ombi maalamu naomba uweke picha yako nzima mpaka chini na mavazi hayo hayo, na style hiyo hiyo. Kama huna unaweza kupiga utuwekee hapa. Hongera sana kwa kutoka mchicha leo.

Anonymous said...

Da Yasinta nina uhakika hata wewe leo umejiona ulivyotoka bomba!Kama hujaona basi itabidi uende kwenye kioo kujitazama tena kwa mara nyingine. Mana mie nisiseme mengi zaidi. Jamani nakumbushia picha yako na Camilla....au Camilla alikataa nini? Chonde chonde nasubiria kwa hamu sana.

Rachel siwa Isaac said...

Asante kwa ujumbe mzuri..umetokelezea sana KADALA wa mimi..

Wako KACHIKI.

ray njau said...

Nenda, ukale chakula chako kwa kushangilia na kunywa divai yako kwa moyo mchangamfu, kwa sababu tayari Mungu wa kweli amependezwa na kazi zako.Katika kila pindi, mavazi yako na yawe meupe,wala kichwa chako kisikose mafuta. Furahia maisha pamoja na mke unayempenda siku zote za maisha yako yaliyo ya ubatili ambayo umepewa na Yeye chini ya jua, siku zote za hali yako iliyo ya ubatili, kwa maana hilo ndilo fungu lako maishani na katika kazi yako ngumu unayoifanya kwa bidii chini ya jua.Yote ambayo mkono wako unapata kufanya, yafanye kwa nguvu zako zote, kwa maana hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi, mahali unapokwenda.
Nilirudi, nikaona chini ya jua kwamba si wenye mbio wanaoshinda katika mbio, wala wenye nguvu wanaoshinda katika pigano,wala pia wenye hekima wanaopata chakula, wala pia wenye uelewaji wanaokuwa na utajiri,wala wenye ujuzi wanaopata kibali;kwa sababu wakati na tukio lisilotazamiwa huwapata wote.Kwa maana mwanadamu pia hajui wakati wake.Kama vile samaki wanaonaswa katika wavu mbovu,na kama ndege wanaonaswa katika mtego,ndivyo wana wa binadamu wenyewe wanavyonaswa wakati wenye msiba,unapowaangukia ghafula._Mhubiri 9:7-12

Anonymous said...

Maneno yako ni ya hekima sana. Umegongelea msumari katikati ya mbao. Hongera da Yasinta. By Salumu.

Said Kamotta said...

"Huo ni ukweli halisi wa maisha, natamani kila mtu angeyaelewa vizuri maeneo hayo. Kwa ujumbe huo pekee unatosha kubadilisha na kutibu nyoyo za watu na maisha yao."

Ester Ulaya said...

ujumbe mzuri sana Dada, kweli maisha i zawadi, huo mkanda uliovaa umekupendezesha sana

emu-three said...

Hilo ni Wazo la hekima kweli: Na mara nyingi mtu analalamika kuwa `hakitoshi' kwa vile anacho, hajui kuwa kuna mwenzake hana, anatamani angalau akipate hicho kidogo unacholalamika nacho kuwa hakikutoshi.

saraha mgaya said...

kweli
kabisa.....hapa wengine tunaomba Mungu atupe waume wengine hata chakula
hawawapi,kutwa kuwasengenya....haijakaa vizuri.....tuwe na mioyo ya
shukrani na Mungu atatubariki.....

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni wote kwa mchango wenu Ahsanteni wote na tupo pamoja na tuzidi kudumisha ushirikiano ili kazi zetu ziwe nzuri na za kutia moyo.AHSANTE.

Noel mbise said...

Nimependa sana ujube wako umenifariji vya kutosha

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante Noel na karibu sana gapa kibarazani. Pia nafurahi kusikia umepata faraja.

obat penggugur said...

obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat cytotec