Kutoka kushoto ni kikombo cha chai ambacho kina chunjio na mfuniko wake si mnajua nilivyo mpenzi wa chai, hicho cha maji ya bahari ni flip cover kwa ajili ya simu yangu, ya tatu ni sceen protertor, nilipata na bahati nasibu /TRISS, ila bahati mbaya sijapata bahati nasibu.. NA MWISHO hicho mkionacho cha bluu ni kwa ajili ya kuhifadhi simu yangu nikimbiapo maana huwa napenda kusikiliza miziki......haikuishia hapo nikaandalia...
....keki na ni dada Camilla ndiyo aliyetengeneza keki hii maalumu kwa ajili ya mama---inaitwa rabarberkaka/keki ya rhubarb...karibuni bado ipo......
13 comments:
Yummy, yummy cake! Nakutakia sherehe njema na bab kubwa. Mbarikiweni jamani. Faidini majira haya ya joto baada ya kukong'otwa na baridi ya winter.
Mwal. Mhango ! Ahsante ...ni kweli baridi ilikuwa kali na bado ipo ..lakini leo nimekuwa nje na ndala , sketi na t-shirt tu :-D
Hongera sana Yasinta.
Keki tumekula kwa macho, mwambie Camilla ilikuwa tamu sana! Siku ingine apike special kwa ajili wa wanablog wa mama tu. haya mie wa kupostiwa sijui keki ntaipata?
Hongera kwa zawadi, unastahili kwa kweli...Hivi Camilla kumbe ni mpishi mzuri hivi?
Mpe hongera zangu..
Hongereni sana!!
duh! hongera sana dada. Sasa hiyo keki ndio tinekula pekee bila kutualika?
Udiye na jina wala usikonde atatengebeza tu maana anapenda mno kuoka....
Dada mkuu msaidizi! Ahsante. ..jana nilistarehe kweli. Mija mtoto wa nyoka ni nyoka.
Kaka Ray. ..ahsante.
Kaka mrope..kwanza karibu tena nimekumiss. ..ahsante kaka. Kaka si nimesema hapo juu karibuni..karibu alo
Mwe wajameni tutakaribia sana tu. hakikisha ni vya kutosha kwa wote
Kaka Mrope! Wala usikonde utaacha mwenyewe, wewe njoo tumbo waziiiii
mh namashaka na hizo budget zenu nje!kuna kushiba kweli au maneno tu.
Usiye na jina! Ukija utajionea mwenyewe. Hakuna gaja ya kuandikia mate.....
Duuhh nilipitwa "KACHIKI" Hongera sana KADALA na kina MAMA wote, Bila shaka keki nimewekewa..kizuri kula na nduguyo!!!!!
Kchiki! Si unajua hakuna kuchelewa...Ahsante na hongera nawe pia kuhusu keki usikonde:-)
Post a Comment