Monday, April 2, 2012

JIPATIA KITABU:- JINA LA KITABU MALIPO NI HAPAHAPA MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE

Ambaye pia ni mtangazaji wa radio passion FM ambayo inarusha matangazo yake jijini Dar es salaam. Ninayo furaha kukamilisha kitabu cha simulizi cha MALIPO NI HAPAHAPA ambacho kimebeba simulizi tatu za kusisimua ikiwemo simulizi inayoitwa DADA YANGU, MAMA MDOGO pamoja na simulizi iliyobeba jina la kitabu MALIPO NI HAPAHAPA
Kitabu cha Malipo ni Hapahapa na simulizi nyingine za maisha kinaonyesha hali halisi ya maisha tunayoishi, matatizo tunayokutana nayo na namna ya kutatua matatizo tunayoyapata kwa wakati huo. Pia kwa kusoma kitabu hiki utajifunza mengi kwani kinatoa picha halisi ya maisha yetu ya kila siku.
Ndani ya kitabu hiki nimezungumzia maisha na mapenzi katika mtazamo halisi na pia kinaonyesha namna mapenzi yanavyoweza kuyageuza maisha kuwa machungu na mafupi.
Ukianza kusoma kitabu hiki hutakiacha hadi ukimalize kwani hadithi zilizomo zimesheheni matukio ya kusisimua ambayo moja kwa moja yanalenga maisha yetu ya kila siku.
Kupitia vitabu vya simulizi za maisha kama vile kitabu hiki, tunajifunza mambo mengi ambayo yanatusaidia kuishi katika mazingira tofauti ikiwa ni katika shida au raha na hata kujua namna ya kuishi na watu wanaotuzunguka.
Utapata kitabu hiki kwa bei ya sh 5000 tu.
Kwa mawasiliano kuhusu upatikanaji wa kitabu hiki.
Tafadhali tumia no zifuatazo +255652343430 au +255752817444Au kavisheadela@yahoo.com Unaweza pia kuingia humu http://www.adeladallykavishe.blogspot.com/
Nimetumiwa hii na mtunzi wa kitabu .Samahani rafiki mpendwa naomba uniwekee katika blog yako:-

2 comments:

simba deo said...

Adela, hongera kwa kuandika kitabu. Tunahitaji Watanzania wengi zaidi kama wewe. Vilevile tusome vitabu jamani ... kuna siri na maarifa mengi ya maana.

ray njau said...

Hongera sana Adela kwa kuonyesha kipaji chako kwa jamii yako.Hongera sana Yasinta kwa kuungana na Adela katika kazi yake.Changamoto yetu ni jinsi ya kuaendelea kuwaibua wanazuoni wenye vipaji vya uandishi katika uga wa tamthiliya na riwaya kwa manufaa ya jamii yetu.