Monday, April 16, 2012

Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi?

Fikiri, matumizi nyumbani: chakula, umeme, gesi, maji, soda/juisi za wageni. Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu. Matibabu hospitalini, pesa ya walinzi kwa mwezi, sherehe za kuaga na kukaribisha mwaka mpya; Zaka ya kanisani na misikitini, Kupanda Mbegu/ Sadaka, Shukurani ya Neno, Ahadi na Collect, shukrani ya Chakula cha Bwana church, marekebisho ya kitasa cha mlango kabla mwenye nyumba hajashtuka, gharama za marejesho ya mkopo wa saccos kazini. Tozo za Flying (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzit...upa hapo hapo), Madalali wa nyumba/viwanja, Pango la nyumba, Fremu ya biashara/ofisi, Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers]; Mafuta ya gari, Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo apaaa); Tozo za kuegesha magari, Makato ya Mikopo, Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf. Rambirambi ya mfiwa mtaani kwetu, Harusi ya ndugu yako wa ukoo na zawadi, Sendoff ya mtoto wa mdogo wake rafiki yako na zawadi, Kumuaga mfanyakazi mwenzetu na zawadi, Michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara; Michango ya besdei party na zawadi; Ndugu wa kule kijijini, Mshahara wa Hausigeli na hausiboi; Bodaboda, teksi na bajaj; Duka la dawa kwa Mchaga, Tuisheni ya mtoto, Kuchangia wahanga wa mabomu na mafuriko. Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa, Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu. Chakula cha mbwa, Machango wa Ujenzi wa Kupanua Kanisa, Kuchangia Uinjilisti Masasi, outing ya kitimoto, Ujenzi wa Nyumba Mabwepande, Kuendeleza shamba mkuranga (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa). Na kwa wale wenzetu wanaokwenda umbali wa Viti Virefu, moja moto moja baridi. Maji ya Traffik, Chai ya Nesi na Daktari, Kahawa ya Hakimu, Karani na PP. Vishoka waunganisha maji na umeme; Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa, makaribisho ya get together na dinner kwa rafiki wa kikazi ambaye hamjuani ila kweye simu tu, Mchango wa matibabu ya mtoto Nyumba ndogo kule Ngusero, mchango kidogo kwa rafiki aliyevamiwa na Vibaka na kuumizwa vibaya, gharama za malipo ya mtura Mkulima Bar Moshi, manunuzi ya maji ya Kilimanjaro Uwanjani Sheikh Amri Abeid Ukicheck mechi ya Yanga na JKT Oljoro, malipo kwa ajili ya Uji wa Shanga baada ya kazi Njiro jioni ya Alhamisi, Vipi manunuzi ya kandambili kwa ajili ya matumizi ya home.Hivi hali inakuwaje? Mia mbili ya watoto wa mtaani/ombaomba, kitu kidogo cha wale wanaolazimisha kuosha kioo cha gari kwenye foleni. umeme uliopanda bei, gesi iliyopanda bei, maji yaliyoadimika, bado contingency mana huu usafiri unaotembelea ball joint, bush, feni belt havijafa - hapo bado service. Bado msosi wa mchana kazini esp kama maofisi yetu mama ntilie wanakaribiana bei za restaurants, bado mchango wa kitchen pati na sare, baby shower. Na hapo bado hujatoa watoto outing jumapili, Upo wapi uwezekano wa kununua laptop mpya ambayo ni muhimu katika mfumo wa maisha ya kisasa, desktop nyingine kwa ajili ya watoto at home, rim mpya za gari ambazo zimeingia ku modernize gari lako kuu kuu, vipi kuhusu gharama za kujipendekeza kwa kimwana wa job ambaye amekubali kwenda nawe out leo, gaharama za matibabu ktk hospitali binafsi kwa kuwa madaktari wa serikali wapo ktk mgomo, Dogo naye “bro ninunulie basi japo kasimu ka promosheni, ile yangu imedondoka chooni” Mara “Bro/Sister Next week on sato shuleni tunavisit snake Park na sina shilingi 3000 za mahudhurio”, Wife naye “ Daddy leo Mwakasege yupo relini, vipi tutapitia? Hapo ujue kichwani gharama ya taxi baada ya semina, vipi tozo za toyo kwa kuwa nimeachwa na gari la staff. Dullah the balhead kama kawaida anakusubiri uwajibike kwa gharama zako. Mama yangu!!!!!!!!
Hapo mwajiri amekuongezea mshahara kwa 7% tu wakati inflation ni above 19%.Ukifikiri kwa makini, unajiuliza watanzania wana-survive vipi kwa style hii???Ndipo unapoimba "Mwokozi nitoe roho niepuke, hili balaaa"
HABARI HII NIMETUMIWA NA RAFIKI YANGU MUPENZI NA NIKAONA NIWAHABARISHE NA WENZANGU!!!

5 comments:

Rachel Siwa said...

Duhhh kazi kwelikweliiiii!!!!

ray njau said...

Wakubwa shikamooni,wenzangu hamjambo na chekechea amani kwenu.
Kwa ujumla hakuna mjadala kuhusu mada ya influeshoni ulimwenguni ila hapa ni tofauti za kijiografia kutoka eneo moja kwenda lingine.Gharama za maisha ya kila siku ulimwenguni zimepanda na hapa sasa nakumbuka maneno ya wanamuziki:"Maisha ni mchezo,dunia ni jukwaa na kila mmoja anacheza awezavyo".
Wahenga walisema:"KATA KOTI LAKO KULINGANA NA KITAMBAA CHAKO".[Mungu siku zote anapokea lawama za ugumu wa maisha ya mwanadamu. Lakini mwanadamu huyo akiulizwa katika maisha yake ya kila siku anatanguliza mambo gani maishani katika kile kiduchu anachopata?Je kwanini mitaani kwetu baa ni nyingi kuliko shule na nyumba za ibada?Je kwanini michango ya arusi na maziko inazidi ile ya elimu na matibabu?]

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mmmmh!

kaazi kwelikweli

emuthree said...

Kazi kwelikweli...ukiona kwako kunafuka moshi kwa mwenzako kunaungua

Unknown said...

Aisee ni ngumu sana,maisha ya mtanzania yamekuwa magumu kweli sasa