Monday, December 19, 2011

TOFAUTI YA AINA HIZI ZA UPUPU WA KUWASHA NA USIOWASHA MANGATUNGU (velvet beans au cowitch beans)

Wiki iliyopita niliweka hapa picha ya upupu na baadhi ya wasomaji walisema kwamba ni chakula kitamu sana ingawa unawasha. Lakini nijuavyo mimi picha hii hapa juu ndio huliwa kule kwetu tunaita MANGATUNGU. Chakula hiki inabidi upike kwa makini sana. Kwanza unachemsha kisha unamenya. Na hapo kazi inaanza unachemsha na kumwaga maji zaidi ya mara kumi. Sababu ni kwamba inasemekana kuna sumu ndio maana maji ya mwanzo huwa meusi sana . Kwa lugha ya kiingereza huitwa "velvet beans au cowitch beans"...pia inasemekana:- Mangatungu ni dawa kama viagra, ni kahawa, na ni dawa ya kutibu magonjwa ya nerves kama vile Parkinson disease. Kwa habari zaidi soma http://en.wikipedia.org/wiki/Mucuna_pruriens#Uses
Na hapa ni ule upupu wa kuwasha ambao kaka Mfalme Mrope na kaka ISSACK CHE JIAH wanasema ni chakula kitamu sana. Inawezekana ila mimi najua ni aina mbili tofauti...kwa kujikumbusha soma maoni hapa.

8 comments:

ray njau said...

Duh;hapa ni vigezo na masharti kuzingatiwa!!

chib said...

@ Ray, tehe teh teh

Yusuph Mcharia said...

Hodi jamani, za siku tele? poleni kwa michakato ya maisha.

Niliadimika sababu ya majukumu ya kiutayarishaji.

Naulizia kama upupu wa aina yoyote umebaki, au njia ipi niifuate ili nifike ulipo?.

Tehe...siuogopi.

Issack jiah said...

Hi jamani jana nlikuwa sipo kiofisi ila leo nimefika lazima nichungulie MAISHA du kumbe wenzangu jana wamekula sana upupu ni kweli kabisa upup upo aina hizo mbili una washa na usiowasha ila aina hizi zote zinaliwa.Ila kuna kazi kwa kuutayarisha unajuwa upupu wa kuwasha ni mdogo sana na huu usiowasha ni mkubwa na mpana sasa kinachotakiwa wakati wa kuutayarisha ndipo kazi kubwa, kwanza unapikwa na maganda mpaka yale maganda yanawiva ,yakiwiva unaumenya na kisha unausafisha mpaka yale maganda yote yatoke ,hapo ndipo unaanza kuupika tena,unachemka kila baada ya muda unamwaga yale maji ,unafanya hivyo mpaka kama mara sita nikazi ya kutwa mzima alafu utaona upo mweupe au ule wa kuwasha unaweza uona mweusi si sana ,hivyo kujuwa kama umewiva unaangalia ndani ukiona kiini bada cha njano juwa bado ila ukisha ona unameguka kiurahisi basi tayari kwa kuliwa ,kiungo kikubwa cha chakula hiki cha upupu ni chumvi ile kachumbari ni kama kiungo mbadala au makorombwezo kwa wale wenye uwezo,Nilimuliza bibi kwanini chakua hiki utengenezaji wake ni mrefu Na kwanini walifanya kuwa chakula alisema hiki chakula kiliandaliwa miaka hiyo kwaajili ya njaa mwaka wa njaa ndiyo chakula kikuu kwa maeneo ya kule MASASI,NACHINGWEA NA HATA NEWALA mwaka 1945 njaa ilikuwa imeenea na hali ya hewa ilikuwa mbaya na mwaka ukiwa na ukamwe huwa njaa na madudu kama haya huwa yana kuwa meni ila kwasasa kama hayo mangatungu watu wanayapanda kama zao na kisha upup ni biashara kubwa kwa pale sokoni mjini masasi na vijiji vyote vya masasi ukiwa na upupu wewe ni pesa kwa kwenda mbele ila kwetu tumesifika kwa kula vitu vya ovyo hii sijajuwa ni kwanini kwani hata wale PANYA MWITU NAO NI DILI JE DADA UNAIJUWA HIYO
KWA HERI CHE Jiah

Mwita Hardson said...

Wanaosema upupu ni mtamu basi haujawawasha .Kitu mangatungu ni noma ina wanga wa kutosha.Na ukiipata ile original kama hauna maji ya kunywa pembeni yanabana ile mbaya.Therefore mangatungu na upupu ni vitu viwili tofauti na upupu hauliwi ila mangatungu ndiyo yanayoliwa.Huo ni mtazamo wangu

Issack che Jiah said...

Lakini jamani kwani jina la mangatungu ni kiswahili au kilugha cha kwenu kwani nijuwavyo sasa kuwa upup ni kiswahili na mangatungu ni lugha yakweni maama mapishi yake mtiririko wake ni mmoja mbona dada yasinta haujamaliza maada hii kwani umensikia mwita alichosema hapo? toa maamuzi tofauti yake nini hapo

Mtesuka said...

Asante dada nilirudi hapa kuwaonesha watu ninaposema mangatungu na maanisha nini? Wamenielewa sana!