Monday, September 7, 2009

WANAUME WA KITANZANIA

WASAMBAA
Ana mke mmoja,
ana mpenzi mmoja (rafiki wa kike),
Lakini anampenda zaidi mkewe.

WACHAGA
ana mke mmoja,
Ana mpenzi mmoja (rafiki wa kike),
Lakini anampenda zaidi mpezi wake.

WANGONI
Ana mke mmoja,
Ana mpenzi mmoja (rafiki wa kike),
Lakini anampenda zaidi mfanyakazi wa nyumba.

WASUKUMA
Ana wake wawili,
Ana wapenzi wawili,
Anampenda zaidi dada ya mke wake.

Coateriana/waZanzibar
Ana wake wanne,
Hana mpenzi,
Ana mpenda zaidi mke yule mpya.

WAJALUO
Ana wake wanne,
Ana wapenzi wanne,
Ampendaye zaidi ni mke wa jirani.

WANYAMWEZI
Ana mke mmoja, wake wawili,wake watatu,
Ana wapenzi kadhaa,
Ampendaye zaidi ni muhudumu wa baa/mgahawa.

WAKURYA
Mke mmoja,
wapenzi wengi,
Anawapiga wote.

WAMASAI
wake wawili,
mpenzi mmoja,
Ampendaye zaidi ni ngómbe wake.

WASOMALI
Wake wanne,
Hana mpenzi,
Anachokipenda zaidi ni miraa.

12 comments:

Simon Kitururu said...

DUH!

Fadhy Mtanga said...

Kesho wanaume tutaandamana kupiga hayo.
Lakini hata hivyo azavali sie hatumo.

chib said...

Tunaomba ututolee na wanawake wa makabila hayo wasifu wao :-)

viva afrika said...

jamani yasinta, hili kweli ni shambulio makini kwa wanaume kwani tukiuliza juu ya uchunguzi wa hoja hii najua utasema "si tunawaona kila siku, ndio mlivyo" anywayz nahisi ukweli kwa mbali hv.....

Mzee wa Changamoto said...

Mmmmmhhhhhhhhhhhh!!! Ok nimesoma mara mbili nimepata jibu la kukubana wewe Da Yasinta. Hahahahahaaaaaaaaaa
Huu uwiano mzuri saaana. Inaonesha kila palipo na mwanaume mmoja anayevunja agano la ndoa, kuna zaidi ya mwanamke mmoja afanyaye hivyohivyo.
Sasa nadhani kuna haja ya ku-focus zaidi kwa wanawake kwani wakielewa na kuacha kutembea kabla ama nje ya ndoa, hawa wanaume hawatakuwa na mwanamke wa kutembea nao.
Nikitumia TAKWIMU ZAKO, kuna mifano ya wanaume kumi lakini hao wanaume wanahusiana na jumla ya wanawake (at least) 37(nahesabu wawili kila uliposema "wengi"). Huoni kuwa tatizo ni wanawake? Kama wanaume ni waongo, basi wanawake wana matatizo ya kudanganywa na wanastahili kutibu ugonjwa huu. Ila nadhani wanasingizia tuu kwani hakuna lolote wasilolijua. I mean kama si mumeo kaa mbali naye. Haijalishi kama ameoa ama hapana. Hiyo ndio ingekuwa dawa. Kuwalaumu wanaume kwa kuwa na mitara, ni kuwapa wanawake fikra dhaifu kuwa wenye maamuzi ni wanaume. "Wakiwataka mkubali na wasipowataka basi msilalamike" Lol.
Naacha hili. Kwanza WAHAYA hatupo. Nadhani kwa kuwa ni mke mmoja na hakuna mpenzi na tunapenda zaidi mke huyohuyoooooo. Hahahahaaaaaaaaaa.....Simo

Serina said...

Lol...umenifurahisha sana leo na ukweli huu... Mube, sio uwongo, wanawake twapenda maneno matamu!!!

Anonymous said...

Mi ndio maana nilikataa kuolewa na mombi hii nyumbi hii kwa sababu hii. nikweli kabisaaana aya uliyoyaweka apa ni maneno ya kweli.

chib said...

Mzee wa changamoto, haleluyaaaa
Umefungua ukweli

Unknown said...

mi naungana nawe na hiyo ya wachaga..kabisaaaaaaaaaaaaaaa..dah sijui mambo haya yataisha lini na vile magonjwa yakila aina sasa:(

Yasinta Ngonyani said...

Sijaelewa ni vipi mtu anaweza kumudu wanawake wawili. Labda hii yote kutokana na mmoja akiwa na mimba basi anaenda kwa mwingine au?:-) nawaza tu!!! Asanteni wote na najua kila mtu kuna kitu amejifunza kwa namna yake:-)

Chacha Wambura said...

Msee ya changamoto, wahaya nao wamo!!! muke moja, hakuna mupenzi, wanapenda senene na matoke !!!!!!!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana Chacha Wambura kwani M/wa changamoto alikuwa anajidai sijaliweka kabila lake .....LOl