Thursday, September 3, 2009

MADAWA YA KULEVYA NA UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KATIKA MAISHA

Duniani wote tunapenda sana kijisikia vizuri. Tunataka kujisikia kuwa na raha, wenye nguvu na sio kuwa na wasiwasi. Hivyo wengi wetu tunaanza kufikiria kuwa dawa za kulevya, pombe na sigara zitatupa raha. Angalia sana! usidanganyike! kutumia vitu hivyo ili kupata furaha bali ni kuhatarisha maisha kwani unaweza kujikuta umeingia ulevini. Kujinasua kwenye hali hiyo itakuwa kasheshe kwelikweli (si lelemama) inahitaji moyo na pia kujizatiti.

Halafu nimefanya utafiti kidogo kupita katika mashule nimeona ni asilimia kubwa wavutao sigara ni wasichana yaani hapa nazungumzia watoto wa shule za misingi. Na ukizingatia watoto hao si zaidi ya miaka 16. Yaani ni watoto wadogo pia wanakunywa pombe. Sijui watakapofikia mia 30 maisha yao yatakuwa ya aina gani. Nimejaribu kujiuliza wanapata nini katika kufanya hivi lakini sijapata jibu naomba tujadili pamoja ndugu zanguni.

Leo nimejisikia kuandika kwa kiswidi pia ili nao wafurahi:

LIVSSTILS HOT:-

Tobak är gift för kroppenRökning är extremt skadlig och ökar risken för cancer, sjukdomar i luftvägarna, hjärt-kärlsjukdomar, typ 2- diabetes, magsår, benskörhet, nedsatt fruktsamhet och dålig sårläkning. Tobaksrök innehåller över 4000 olika ämne, varav många är giftiga - till exempel koloxid och nikotin - medan en del är tjärämnen och andra partiklar som sätter sig i luftvägarna.

Alkohol ger organskadorAlkohol i en mängd överstigande 15ml ren alkohol per dag är skadlig för bukspottkörtel, tarm, lever samt nervcellerna i hjärnan och andra ställen i kroppen. Organskadorna kan leda till dåligt upptag av vitaminer och mineraler, viliket i sig påverkar hälsan negativt. Alkoholens skadeverkningar beror på att det är ett lösningsmedel som irriterar cellerna och belastar leve.

6 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nimefanya utafiti juu ya masuala haya, hali inatisha saana duniani kote na hapa tanzania. kuna baadhi ya nchi zinaongozwa na wavuta unga na wana nguvu kuliko serikali. inasemekana kuwa sera ya nchi za kiarabu kulewesha ulimwengu wa magharibi na ndio maana marekani naitwanga nchi ile ya akina Afghan kwani inalewesha kizazi chao.

madawa haya utokea nchi za kiarabu kama Iran, nk na lengo ni Marekani,China, Ulaya nk kulewesha kizazi kijacho japo ngoma inageukia afrika, hali inatisha ndugu ya madawa.

suruhu ni kulea vizuri watoto, kupata muda wa kuwa nao na kuwapa motisha wa kukuiga badala ya kuwaacha waende zao kinyume nyume, wajitambue

Bennet said...

Huku Bongo hali ni mbaya sana kuhusu unga maana unauzwa kama vile ni halali, polisi wanajua na kila siku wanapita kuchukua kidogodogo yaani jamaa ni kama vile wanalindwa na polisi
Bangi na mirungi ni halali kabisa bado tu kukatwa kodi maana hata watumiaji watumia hadharani kabisa bila kujificha

Anonymous said...

Hej vännen... ville bara hälsa lite kort... hoppas allt är bra med er. Stora kramar från Kenya. Serina

Mzee wa Changamoto said...

Kwani ni nani wa kulaumiwa kati ya wanaolima, kutengeneza na wanaosambaza na wale wanaonunua na kutumia licha ya maonyo wanayopewa.
Labda kuongeza bidii katika kuelimisha jamii maana nadhani kutotofautisha ukweli na uzushi ni mbaya na inafikia wakati tunataka kujua uzuri wa kibaya kwani tunaona tunatishwa kuliko kufunzwa
Tufunzwe na kuelezwa ukweli na si kutishwa
Mtoto hatishwi, bali vitisho tuonavyo vinafanya kazi, vinawajengea "upande wa ndani" wa ubishi na ukaidi na matokeo yake wanakuwa wakaidi kuzidi.
Na hapa si wazazi tu, bali WALEZI NA NAMAANISHA JAMII

Unknown said...

Det är så sjukt och livsfarligt men tyvärr så är det ju inte så många som tänker på det,det värsta är att börja man röka vid 15 års åldern så är det ju inte så lätt (för dem flesta) att sluta:(:(
Jag vet inte hur det är i andra länder men här i Sverige daah ndio basi tena!!

Yasinta Ngonyani said...

Watu wengi wanafikiri wanapata raha kumbe wanajitafutia kifo. Juzi nimesikiliza na kuona hanari kutoka Afghstani wanalima madawa ya kulevya na ni watoto wadogo walikuwa wanavuna. Nahisi kama sasa ndio mwisho wa dunia maana naona magonjwa ya aina mbalimbali yanatokea yenye majini ya ajabu ajabu na pia wavutaji wanaongezeka na mbaya zaidi wanaanza mapema miaka 10. Hivi wanapata nini ndani yao?