Thursday, September 10, 2009

USICHOKE

Maisha ni kama vita, usichoke kupigana,
Hata kama ukigota, endelea kupambana,
Bado muda wa kutweta, bado ni mapema sana,
Usichoke mwanakwetu.

Nenda shule ukasome, uongeze maarifa,
Ukiwa huko jitume, uliinue taifa,
Nenda kakazane shime, utajipatia sifa,
Usichoke mwanakwetu.

Amka wahi kazini, ili uongeze tija,
Ujuzi wako kichwani, taifa linaungoja,
Ujitume ofisini, na wenzako kwa pamoja,
Usichoke mwanakwetu.

Pigana pasi kuchoka, yapiganie maisha,
Jitihada zako weka, ustawi kufanikisha,
Kwa dhamira ya hakika, malengo kufanikisha,
Usichoke mwanakwetu.

Mwiko kukata tamaa, bado ni ndefu safari,
Kurudi nyuma kataa, pambana nazo hatari,
Tumia kila wasaa, maisha kutafakari,
Usichoke mwanakwetu.

Usifanye masikhara, maisha hayendi hivyo,
Kwa hiyo kuwa imara, vile iwezekanavyo,
Nawe utazidi ng'ara, namna itakiwavyo,
Usichoke mwanakwetu.

Kwa idhini ya Usichoke
Maisha ni kama vita, usichoke kupigana,
Hata kama ukigota, endelea kupambana,
Bado muda wa kutweta, bado ni mapema sana,
Usichoke mwanakwetu.

Nenda shule ukasome, uongeze maarifa,
Ukiwa huko jitume, uliinue taifa,
Nenda kakazane shime, utajipatia sifa,
Usichoke mwanakwetu.

Amka wahi kazini, ili uongeze tija,
Ujuzi wako kichwani, taifa linaungoja,
Ujitume ofisini, na wenzako kwa pamoja,
Usichoke mwanakwetu.

Pigana pasi kuchoka, yapiganie maisha,
Jitihada zako weka, ustawi kufanikisha,
Kwa dhamira ya hakika, malengo kufanikisha,
Usichoke mwanakwetu.

Mwiko kukata tamaa, bado ni ndefu safari,
Kurudi nyuma kataa, pambana nazo hatari,
Tumia kila wasaa, maisha kutafakari,
Usichoke mwanakwetu.

Usifanye masikhara, maisha hayendi hivyo,
Kwa hiyo kuwa imara, vile iwezekanavyo,
Nawe utazidi ng'ara, namna itakiwavyo,
Usichoke mwanakwetu.

Shairi hili linatoka kwa http://fadhilimshairi.blogspot.com/ nimeona sio mbaya kama likisambaa ili wengi wasome ni ujumbe mzuri.

3 comments:

Fadhy Mtanga said...

Ahsante sana da Yasinta kwa utu wako wa kiwango cha juu mno.
Tusichoke jamani!

Mzee wa Changamoto said...

Nimesoma, ndio nimemaliza kutafakari na sasa nayaweka moyoni na mawazoni.
Blessings

Yasinta Ngonyani said...

Fadhy ni furaha sana kusoma mashairi yako na huu ujumbe niliona si mbaya kama ukiendelea kusambaa. Ni kweli tusichoke jamani.

Mubelwa usimalize kutafakari endelea kutafakari na pia usiyaweke moyoni na mawazoni tu wagawie na wenzako:-)