Wednesday, September 2, 2009

HII MLIWAHI KUISIKIA? - MKE NA MUMEWE

Kulikuwa na njemba moja imeowa ,tatizo la njemba huyo ni kukojoa kitandani kila siku ,hatimae mke ustaarabu na uvumilivu ukamshinda ,na siku moja akaamua kumkoromea mumewe kuwa ,kazi ya kufua mashuka na kuanika godoro kila siku itamshinda na anaona aibu maana majirabu wameanza kuhoji mbona kila siku kunafuliwa mashuka na kama haitoshi hata yeye mikono imeanza kuota masuguru na kuchunika kwa tindikali ya kojo lake.

Sasa akamuweka kiti moto mumewe na kumwambia kuwa leo ni siku ya mwisho na ikiwa usiku wa leo atakojoa kitandani basi itakuwa ndio mwisho wa wao kuwa mke na mume kila mtu atashika njia yake na kwa ufupi ndio atakuwa ameachika.

Kwa kweli siku ile njema yule alipata mtihani mkubwa sana na aliona hatima ya ndoa yao inafikia mwisho au ipo ukingoni kabisa.

Kwa bahati usingizi ukawachukua ilipofika alfajiri ,yule mke kitu cha kwanza alianza kupapasa kuona kama kuna kojo limetapakaa kwenye kitanda ,hakuona kitu na kufikiri kuwa mkwala aliomchimbia mumewe umefanya kazi ,dah kuja kutahamaki anasikia harufu ya mavi na kuona kila kukicha ile harufu inazidi kunukia ndani ya chumba chao ,kutahamaki kumbe mumewe siku ile hakukojoa amekunya.

Yule mke akili ikamzunguluka na kuona ya leo ni mpya tena ya aina yake ,ikabidi atulie na kumwita mumewe kwa upole kabisa kabisa huku akionekana mwenye kumshangaa na siejua la kufanya ,haya mume wangu embu nieleze hii ya leo ni ipi maana mtu mzima wewe sasa unaniletea miujiza ?

Yule njemba akamwambia mkewe ,kwanza akataka msamaha na kumwambia kila alalapo inapofika usiku wa manane humjia mtu usingizini na kumuamrisha akojoe kitandani au sivyo atamuua ,ila usiku wa kuamkia leo alipokuja kuja nikampa ile issue na mkataba wako ,hata hivyo haikuwa salama akaniamrisha nifanye kitendo mbadala ,ninye au sivyo atanitoa roho ,nikaona bora ya hivyo kuliko kutolewa roho ,nisamehe mke wangu sio lengo langu ila ni maswaibu ambayo yapo nje ya uwezo wangu ,yule mke kusikia hivyo aliangua kilio haijulikani kwa nini.
Habari hii nimeipata Jamii forum.

Inafanana:-

Nilipokuwa naisoma habari hii nikakumbuka habari moja ambayo inayofanana na moja ambayo niliishuhudia, walikuwa ma jirani zangu wakati naishi Matetereka - Madaba. Mumewe alikuwa kikojozi na akawa anasingizia watoto ndio wanaokojoa. Ndani mlikuwa hamkaliki kwani halafu ilikuwa kali mno. Na hali ya kule Ubenani kulikuwa na ubaridi kila wakati kwa hiyo ilikuwa ni vigumu kukausha godoro na mashuka/mablanketi kila siku. Nikaona sio mbaya nikiweka hapa ili tujadili . Karibuni.

7 comments:

Simon Kitururu said...

DUH!
KATIKA HILI swala:

Ukweli ni kwamba kuna watu wanatatizo hili la kukojoa KIUGONJWA kikweli kutokana na matatizo ya misuli a.k.a breki za kibofu.....,.....

Nakumbuka Mchikichini Primary School pale Morogoro wakati nasoma pale kuna mwanafunzi alikuwa ana hilo tatizo na mara kibao ilitokea anajikojolea hadharani atake asitake pamoja na kujaribu kwenda msalani mara kwa mara.


Kwa wakumbukao wale waliokuwa wanaishi MORO miaka ya tisini Mwanzoni,kulikuwa na bomba la sister duh Tafiki Polisi pale Moro ambaye wachumba walikuwa wanamkimbia kwa sababu hiyo ingawa wengi kabla hawajastukia ishu walikuwa wanavunja sheria barabarani makusudi wakimuona ili washikwe naye ili tu wapate kuongea naye.

DUH na unajua tena zile nyumba za polisi pale Moro zilivyokuwa karibu karibu, hakuna jambo hata la chumbani majirani waache kulistukia na kufanya mpaka wa mbali tuliostukia mvuto wa kimwana tupate feedback kuwa pale tatizo ni nini ingawa jichoni kanona.


Na inasemekana mpaka mmoja wa viongozi walioanzisha CCM Tanzania alikuwa na hili tatizo/Ugonjwa kikweli , kitu ambacho serikali ililipia sana matibabu yake.

[Tahadhari : nukuu hii nimeitoa baa kwa wadaio kushuhudia alivyokuwa anateseka na ugonjwa huu. Kwani unafikiri baa hakuna wambea?]


CHakusikitisha: Bongo ukiwa na huu ugonjwa utachapwa sana viboko na kuimbiwa KIKOJOZI HUYO.... wakati kumbe kweli wewe ni mgonjwa! Na ukiwa mkubwa unawezajikuta unashindwa kutafuta msaada kwa kuogopa kujulikana na JAMII unajikojolea au ndio hivyo utaanza kusingizia watoto wakati mkojo wa kubwa zima unamirindimo ya nguvu kuliko mtoto kama wewe ushawahi nusa.:-(

chib said...

Hata mie wakati nasoma Morogoro, shule naihifadhi kwa sasa, maana ni almaarufu sana kwa watu wenye vipaji, kuna jamaa yeye kila asubuhi ilikuwa inabidi turuke mto wa kojo, maana ulikuwa unapitiliza kwenye godoro na kwenda chini hadi vyumba vingine, lakini watu wote tulikuwa tunaelewa hilo tatizo, na tulikuwa tunampa moyo, na mwishowe alikubali kwenda hospitali kwenda kupata msaada wa tiba

Faith S Hilary said...

Sijui nicheke ama nisikitike ama vipi maana hata sielewi lol!!! Oh Lord have mercy.

Ila nadhani inakuwa condition wale wanajiokojolea kitandani. My cousin alikuwa anakojolea watu anaolala nao halafu anamalizia kwenye godoro ila watu wakiamka asubuhi wadhani sio yeye but tukajua mchezo wake haha. Smart but stupid anyway.lol

Fadhy Mtanga said...

Ya leo kali kali kali kali kali sijui kama nini!
Mola awasaidie jamaa kama hao!

Unknown said...

si mchezo hii kali! sema hili tatizo lipo hadi ukubwani.

Yasinta Ngonyani said...

Nakumbuka binamu yangu alikuwa na shida hiyo na alikuwa anapata adhabu ya viboko kweli kweli mpaka huruma,Tatizo hakuna aliyejua kuwa ni homa. Halafu sisi tulikuwa tukimwimba kama alivyosema Mt. Simon, Kikojozi huyo, nguo zake tuzime moto ..... utoto kazi kwelikweli. Namuhurumia huyo mke alikuwa mvumilivu sana kama ningekuwa mimi sijui kama ningeweza kuvumilia hivyo:-)

Chacha Wambura said...

Mt Simon, huyo wa mchikichini alikuwa na fistula, ama?

Chib, si utoboe hiyo shule yenye vipaji? mbona mie nshaistukia?

pengine wengine wanapenda na sio kaugonjwa...lol