Saturday, September 5, 2009

GEOGRAFIA YA LEO, TWENDENI PAMOJA NAMI KATIKA MKOA WA IRINGA:- WABENA


Mkoa a Iringa
Wabena ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Njombe. Mwaka 2001 idadi ya Wabena ilikadiriwa kuwa 670,000 [1].

Lugha yao ni Kibena. Kutokana na tahariri ya Dr. Kilemile (2009), Kibena ni lugha tajiri sana kwa maneno na ni pana sana ikiwa na lahaja kuu tano: Ki-Kilavwugi (Maeneo ya Ilembula); Kisovi (Kuanzia Lusisi hadi Makambako), Kimaswamu (Imalinyi, Njombe mjini na sehemu ya kata ya Mdandu), Ki-Lupembe (Lupembe)na Kimavemba (Uwemba na sehemu ya tarafa ya Igominyi ambayo si ya Maswamu).

Lugha ni moja tu; tofauti ni ndogondogo, zikitokana na matamshi, mfano kukaza "dz", kwa lahaja zote isipokuwa Kikilavwugi ambacho ingawa inaandikwa "dzi" inatamkwa kama "dji" umuhudji; na Kilupembe inaandikwa "dzi" lakini watumiaji wanatamka kama "chi" umuhuchi, achile - amekuja, wakati "adjile" (Kikilawugi)... Wengine wote wanakaza adzile, umuhudzi. Tofauti nyingine ni ya kutumia k na h. Mfano: Kamwene/ Hamwene, Kangi?hangi, ukukulima/uhulima n.k.

Suala lingine ni tofauti ya baadhi ya maneno mfano: Asubuhi: Lwamilawu/palukela; Kuketi: kwikala/hwikala/ kutama; Chuma mboga: hukova/kukova imboga na huyava/kuyava imboga; Zizi la Ng'ombe: Ligoma na livaga; nyumbani: hukaye na hunyumba; habari za kazi: mwidaliha na madzengo nk.

Kamusi inatakiwa kujumuisha maneno yote yanayohitilafiana na kudokeza yanakotumika. Maana kamusi ni kihenge cha lugha. Hivyo kuita kamusi yale maneno machache ya Kibena aliyoorodhesha Dr. Joshua ni dhihaka kwa lugha hii ambayo ni tajiri mno kwa misamiati.

Kwa mfano neno kupiga tu lina maneno zaidi ya 100 yakionyesha huyo aliyepigwa amepigwa wapi na ku-suggest hali yake baada ya kupigwa. Pia huashiria hali ya mpigaji. Mfano: (tumia) "k" au "h" kutokana na eneo unalotoka: hutova(general) lakini: hupafula (kiganja), hupefula (nyuma ya kiganja), hututa, hukinya, hung'ilula; hung'alula, hutununa, huwindula, hupwinda, hupana,hulibinga, hufidula, hutadisa, hugong'ola, huniabula, hukinya, huhudugula, huniesa n.k. Habari kutoka sw.wikipedia.org.

3 comments:

Fadhy Mtanga said...

Mimi hoi.
Ahsante sana da Yasinta kwa darasa muruwa. Mtani nakupa gwala. Umenifumbua macho kwa mengi hapo kuhusiana na kabila langu.

Mwanasosholojia said...

Hakika da Yasinta wewe ni mwalimu murua! Heko!

Yasinta Ngonyani said...

Fadhy kumbuka ya kwamba ubenani ni nyumbani kwangu na nameishi sana na wabena.Nashukuru kama umefumbuka macho.

Mwanasosholojia ulikuwa umepotea kweli vp u salama kakangu. Ahsante kwa kutochoka kunitembela na asante kwa hiyo sifa.