Hivi karibuni niliweka habari ya diwani mmoja huko mkoani Songea kufuamaniwa akifanya mapenzi na mke wa Shekhe, habari ambayo niliidesa katika mtandao wa Jamii Forum.
Sio dhamira yangu kulizungumzia tukio hili kwa undani zaidi, lakini kinachonifanya nilizungumzia tukio hilo ni kutokana na jinsi jamii inavyolitazama swala zima la fumanizi.
Je ni haki kweli mume kulipwa fidia pale anapomfunia mkewe? Hilo ndio swali ambalo nimejiuliza mara baada ya kusoma ile habari, na baada ya kulipwa ile faini, ni nini kitaendelea? Je mwanamke yule ataendelea na ndoa yake au ndio itakuwa ni mwisho wa ile ndoa? Na je kama ni mwanamke kamfumania mumewe, anayo haki kweli ya kudai fidia kwa yule mwanamke aliyemfumania?
Tunasoma katika Biblia takatifu kitabu cha Yohana Mtakatifu 8:2-1,1 Pale wale waandishi na mafarisayo waliompeleka yule mwanamke kumshitaki kwa Yesu kuwa amezini, tuliona jinsi Yesu alivyowaambia wale washitaki. Aliwaambia, na asiye na dhambi na awe wa kwanza kutupa jiwe kumpiga mwanamke huyu……….wale washitaki walikimbia baada ya kushitakiwa na dhamira zao.
Bila shaka Bwana Yesu alifahamu kabisa kuwa yule mwanamke hakupaswa kuwa pale peke yake. Mnamleta huyu kwangu, je mwanaume aliyezini naye yuko wapi? Kitendo cha kuzini ni lazima kifanywe na watu wawili wenye jinsia tofauti, yaani mwanaume na mwanamke, sasa inakuwaje aletwe huyu mwanamke peke yake?
Kuna ukweli ulio dhahiri kwamba wanaume wengi huwachukulia wapenzi au wake zao kama mali zao, ambazo ni wao tu wanaotakiwa kuzimiliki. Yaani wanawachukulia wanawake kama viumbe dhaifu wasio na uwezo wa kuwa na maamuzi yao wenyewe kama wanadamu.
Kwa mfano ukisoma vyombo vya habari vya nyumbani Tanzania, mauaji mengi yanayotokana na fumanizi, wanawake ndio wanaouwawa zaidi ukilinganisha na wanaume. Lakini kama ukilinganisha kati ya wanaume na wanawake, itakuwa wanaoongoza kwa kutoka nje ya ndoa ni wanaume tena kwa kiwango cha juu hasa.
Kama ingekuwa wanawake nao wanawauwa waume zao pindi wanapowafumania basi wanaume wangeuwawa sana. Inashangaza sana kuona kwamba linapotokea fumanizi mwanamke ndio wa kwanza kubebeshwa lawama badala ya kulaumiwa wote, kwani pale anayeonekana kutia aibu ni mwanamke lakini mwanaume ataonekana ni kijogoo, na jamii haitamzungumzia kama atakavyozungumziwa mwanamke.
Unaweza kukuta mwanaume kufumania ujumbe wa simu ya mapenzi kwenye simu ya mkewe au mpenzi wake ikatosha kabisa kumuua mwanamke huyo. Huo ni ujumbe wa simu, je akimfumania wazi wazi akizini, ni nini kitatokea, bila shaka mnaweza kutabiri kitakachotokea.
Sio kwamba nawatetea sana wanawake, la hasha, ni kweli kwamba wanawake wamekuwa wakiwafumnia sana wanaume tena kwa kiwango cha kutosha, lakini kuuwa ni nadra sana.
Na ndio maana narejea lile tukio la Diwani wa Songea kutozwa faini baada ya kufumaniwa na mke wa Shekhe lina uhalali kweli?
Tutafakari kwa pamoja
13 comments:
Da Yasinta mada ya leo siyo ya kuitolea maoni kichwa kichwa, ngoja nizame chimbo kwanza!
Kataa usikatae lakini bado Duia kwa asilimia kubwa inaendeshwa kwa mfumo dume na ukichunguza bado kuna dume ndilo Stelingi.
Ukiachana na hili la kufumaniwa, ukichunguza mengi mpaka ya Miss Tanzania/Miss Kibaha yote yako kimkao wa mwanamke ni kifurahisha macho na kisaidia siku ya mwanaume kupita shwari na sio sawa na mwanaume.
Ukipita na Majumbani utakuta wanawake wengi majumbani hutambulika kwa shughuli zao tu za nyumbani za kama wasaidizi tu ndio hutambulika na hapo nyumbani hata ukiwauliza wao watadai kichwa cha nyumba ni Mwanaume.
Sasa ukisikia Waungwana mpaka WANAWAKE bado wanamtazamo na wanakubali Mwanamume ni kichwa cha nyumba unafikiri MWANAMKE AKIMFUMANIA MME WAKE atakuwa na nguvu kweli ya kukata kichwa ili nyumba ibaki bila kichwa?
Na ukitaka kufuatilia hili swala utakuta humo humo, Uchumi, Saikolojia, Elimu, ambayo yote yanachangia kwanini jamii inaweza kumsamehe mwananume ambaye kwanza nidio hakimu akifumaniwa na sio Mwanamke.
Jambo hili si rahisi kulielezea kifupi kwakuwa huwezi pia kusahau mchango wa DINI ,Mila na Desturi, na mengine mengi ambayo yanaweza labda mpaka kukuchanganya katika kujaribu kuelewa ni kwanini hata wazazi wengi wakichacha watakaye mpeleka shule ni mwanaume. AU kwanini katika jamii kibao abakiaye na jina na uwezo wakulichafua ni mwanaume kwa kuwa wanatarajia binti atabadili jina.
Na wanawake sehemu kibao DUNIANI umuhimu wao kimila bado hautambuliki zaidi ya ule wa kuwa Wazazi na kulea watoto na mpaka hutairiwa ili kujaribu kuwafanya wasistukie tamutamu ya mshawasha. Sasa aaminikaye ni mzazi akistukiwa kuwa anatumia naye kidude cha kizazi kujiburudisha nacho kama pepsi kuna wasio elewa na kwa hilo watahukumu.
Naacha ila BADO napinga usemacho DADA YASINTA kuwa anayezini anahitaji mtu wa jinsia nyingine katika ulimwengu huu na hata ule wa sodoma na gomora.
Samahani kwa kuandika harakaharaka kama kumewezesha kuchanganya mpakuo wa hoja!:-(
Kitururu!! Yaani unauma na kupulizia hapo hapo.
Yule sheikh, ni njaa tu, lakini kwa mtazamo wa Yasinta, labda huyo sheikh ni mpole maana mwanamke wake hakupigwa wala nini, faini juu kwa juu
Huu ni mfumo dume ndio maana jamaa akapigwa faini, na kama Sheikh angefumaniwa yeye mkewe asingedai faini
Hapa lazima kuna chanzo mpaka huyu mama akatoka nje inawezeka sheikh kaoa mke kijana wakati yeye ana umri mkubwa sasa anashindwa kumpa chakula yake vizuri ndio maana mama akatoka
Kwanza naomba nitoe maoni yangu kwa kumnukuu kaka yangu na kiranja wa wanablog ambaye hata hivyo hawajibiki ndugu Simon Mkodo Kitururu {Jina zuri zana hili}
Nakunukuu hapa chini kaka>
"Naacha ila BADO napinga usemacho DADA YASINTA kuwa anayezini anahitaji mtu wa jinsia nyingine katika ulimwengu huu na hata ule wa sodoma na gomora."
Mwisho wa kunukuu.....
Nakubaliana na wewe kwa baadhi ya maeneo katika hoja yako, hasa juu ya mfumo dume lakini kwa hiyo segment niliyoinukuu, kaka naomba ufafanuzi zaidi,,,,,,
Je Neno kuzini linawakilihsha kitendo gani?
1.Tendo la ngono kati ya mwanaume na mwanamke ambao hawajaoana kihalali, yaani bila kufuata taratibu, iwe za kimila, kidini au kiserikali
2.Tendo la kuingiliana kinyume na maumbile, yaani iwe ni mwanaume kwa mwanaume au mwanaume kwa mwanamke
3. Tendo la kusagana kati ya mwanamke kwa mwanamke.
Usahihi uko wapi?
naomba msaada kwa hilo au tuombe msaada BAKITA.
Pili ningependa kumpongeza dada Yasinta kwa mada hii ambayo kusema kweli inatoa picha ya jinsi mfumo dume unavyozidi kukandamiza mwanamke hata katika karne hii ya 21,
Zinapigwa kelele nyingiii na za kila aina lakini hakuna mabadiliko ya msingi katika kuweka uwiano kwenye mambo ya msingi.
Mtu mwingine anaweza kuona kuwa siku hizi wanawake wanapewa vipaumbele katika baadhi ya maeneo, hasa ya kisiasa na kiuchumi, naomba niweke wazi kuwa haya yanafanyika mijini tu...kule vijijini bado zile sheria zanazomkandamiza mwanamke bado zipo sana tena kwa kiwango cha kutosha, kwa huo mfano wa Songea, hilo ni tukio dogo sana, huwezi kuamini wapo wanwake leo hii wanlazimishw kurithiwa pindi waume zao wakifariki. na kwa swala la kufumania, hilo ndio kabisaa, mwnmke hana haki ya kumfumania mumewe ni kosa na mara nyingi huambulia kipigo au kuachwa yeye...kuna baadhi ya makabila nyumba ndogo hupewa heshima mke hatakiwi kuibughuzi nyumba ndogo ya mumewe..dhubutuuuu ataondoka yeye na nyumba ndogo itabaki, lakini ole wake afumaniwe yeye, hata ni tusi kubwa sana na kama ni kusamehewa labda kama mgoni atatozwa faini na kulipa, lakini huko nyumbani ni lazima moto utawaka.....jJamani na mimi naacha, niwapishe na wengine...
@Mkuu Ramson:
Hicho ulichonukuu nilikuwa nagusia alichoongea Dada Yasinta kama ninukuuvyo: ''Kitendo cha kuzini ni lazima kifanywe na watu wawili wenye jinsia tofauti, yaani mwanaume na mwanamke, sasa inakuwaje aletwe huyu mwanamke peke yake?'' mwisho wa nukuu.
Kuzini kirahisi kwa weza kutafsiriwa kama ulivyosema kwenye pointi yako uliyoipa namba (1) hasa kama tafsiri ya kuzini itumikayo inamisingi ya kidini [mfano Kikristo), au tu kimila fulani na desturi fulani fulani.
Tatizo ni kwamba hata ndoa tafsiri zake hutofautia kwa kufuata hata misingi hiyo hiyo ya kidini, mila au desturi fulani ambazo ndizo hutumika kugeuza kufanya ngono iwe ni tendo la ndoa na sio tu kuwa ni kula uroda.
Na tukianza kufuatilia ndoa hapa duniani utashangaa jinsi tafsiri zake zilivyokuwa nyingi na ni zaidi ya wengi watafsirivyo kwa kufuata misingi miwili tu kwa sana hasa Tanzania ambayo nguzo zake zimeegemea kwenye maadili ya Kikristo au Kiislamu hasa katika kuhalalisha tu kufanya tendo la ndoa a.k.a kujaribu kukwepa kutekeleza kwa furaha uasherati.
Mimi naamini katika dunia hii ambayo imejaa zaidi ya Wakristo na Waislamu ni udhaifu kuchukulia tafsiri za kitendo kihusucho hata wasiofuata maadili au dini husika kuchukuliwa ni kweli tupu wakati watu kibao wafuatao maadili tofauti kwao si kweli.
...INAENDELEA TARARILA!
:-(
@Ramson:
Nikirudi kwenye hoja:
Nilitoa hoja hiyo kwa kuchukuwa ukweli kuwa tukianzia Tanzania maeneo kama ya Musoma ambako Mwanamke kimila za makabila fulani aliruhusiwa kuoa mwanamke, mke wa huyo mwanamke wakati anagawa kidonda kwa ruhusa ya mme wake ambaye ni mwanamke ilikuwa si kuzini mpaka juzijuzi baada ya UKIMWI kuanza kubobea maeneo ndio vita yakufuta hii mila inakua. Ilikuwa Mwanamke ambaye kachukuwa bomba la demu akitaka watoto demu wake kuonjesha ruksa kwa achaguliwaye na mme wake mwanamke na haikuwa kuzini.Ndio hapa bado nagusia hasi na chanya katika kubiringishana.
Nikilenga na dini fulani fulani au labda hata ukristo: Kuna watakao kuambia ukitamani au kuwazia kuiba au hata kumbiringisha mtu basi inabidi utubu kama vile tu tendo ulishalivulia chupi.
Sasa katika dunia hii ambayo wote sio wakristo au waislamu na kwenye dunia hii ambayo Nchi kibao Wasenge wanaoana na Wasagaji wanaoana na wao wahusika hata kama ufikiriavyo wanavyofanya ni kuchezea mavi bado wao tendo wafanyalo wanaliita ni la ndoa hata kama staili iliyotumika inaweza kumlainisha mtu kinyesi kabla ya kwenda chooni.
Na wasenge na wasagaji nao ukiwauliza utastukia wnamatatizo ya nyumba ndogo kumdokoa hausigeli nk katika stili hizo hizo na waitacho na kulalamika ni kuwa mume wangu au mke wangu kazini hasa kama ni Wakristo wa yale hata makanisa yaruhusuyo siku hizi hata Padre au Mchungaji msenge ruksa na kama akiwa ni sister msagaji basi ni siri yake hukohuko kwa masista na kirahisi hatuta mstukia .
Ndio akina dada Wasagaji WANAOANA SIKU HIZI KISHERIA ingawa labda wahusika wanafanana vifaa vya kupanuliana wakiwa wanasaidiwa kutekeleza mengine kwa kutumia pembejeo kama dildo . Na Msenge siku hizi anaolewa na BASHA na hata usitake wakishaoana wanapenda kuingizana muhogo nyama kwa zamuzamu na kwa hilo ni tendo la ndoa. Na wote wakidokoa nje au kabla waaminicho ni ngono iliyohalalishwa hudai ni kuzini wafanyacho na sio kuwa wanapeana utamua kwakuwa wamegundua tu wanavipele vya kusikilizia utamu mpaka kwa nyuma .
Kwa hiyo Kuzini ni swala la tafsiri. Na tafsiri ya kitu inategemea na mengi yaliyokujenga maadili mpaka unaweza ukaamini Jumapili ni siku ya mapumziko ukiwa Mkatoliki, Ijumaa ukiwa Muislamu au Jumamosi ukiwa Msabato kwa kutegemea unaegemea wapi kuipa maada misingi ya KWELI YAKO.
Kwa hiyo ni vigumu kuwa na maana moja ya KUZINI wakati misingi yakuzini imfanyaye mmoja awe na mke mmoja inamhalalishia mwingine wake wanne au akina King Solomon wa kwenye Biblia wake mia nane .Na chakusikitisha maadili yajengayo watu watafsirivyo ni kibao ndio maana Saddam Husein inaaminika alikuwa muuuaji na Barack Obama sasa hivi kwa amri yake watu wanaendelea kufa Afghanistani na kwingineko na kitafsiri kwa wamchekeao bado sio Muuaji.
Kwa kifupi Mkuu Ramson nimeshindwa kukufafanulia swala ulilo nilenga nalo kwa manati!:
Kaka yangu Simon Mkodo Kitururu, nakushukuru sana kwa kujitahidi kujenga hoja katika kutetea kile ulichokisema awali…….Labda hilo lina ukweli kutegemea na tafsiri yako.
Lakini kwa kuwa kibaraza hiki kinakutanisha wadau mbali mbali wenye mitizamo tofauti tofauti, basi tuvute subira labda yupo atakayekuja na jibu sahihi….Inshaaalah.
Kaka Simona umezungumzia jambo moja hapo juu kuhusiana na mila za makabila fulani huko Musoma ambayo yanaruhusu mwanamke kumuoa mwanamke mwingine, eti ili azaliwe watoto na mwanamke huyo, baada ya kutembeza kidude chake hovyo bila kujali atakumbana na maradhi gani……Labda kaka yangu CHACHA WAMBURA wa kule Musoma yuko kwenye nafasin nzuri kulielezea hili.
Mimi nina ushuhuda mmoja nilioupata kutoka kule kisiwani Ukerewe, nakumbuka miaka ya 1990 niliwahi kutembelea kisiwa kile nikifanya utafiti wangu kuhusiana na swala zima la umasikini, hapa sizungumzii juu ya utafiti wangu huo, bali nataka kuzungumzia jambo moja lililonistaajabisa sana.
Nakumbuka nilikuwa kwenye kilabu kimoja cha pombe za kienyeji, mimi sio mnywaji wa pombe, lakini kutokana na utafiti wangu nililazimika kuwepo mahali pale ili kukusanya taarifa fulani fulani.
Nikiwa mahali pale nilitambulishwa kwa bwana mmoja ambaye, baadae niliambia kuwa pamoja na shughuli zake za uvuvi pia ndiye anayewafanyia wanawake wajane tambiko linaloitwa KUSOMBOKA, eti ili kuondoa mkosi.
Kusomboka ni kitendo cha kumuingilia mwanamke aliyefiwa na mumewe ili kuondoa mkosi, na kama ilivyo kwa wanawake na hata wanaume nao wakifiwa na wake zao huwaendea wanawake wataalamu wa hili tambiko la kusomboka na kuwaingilia ili kuondoa kitu kinachoitwa mkosi.
Tambiko hili hufanywa kwa malipo yaani yule aliyefiwa awe ni mwanamke au mwanaume hulazimika kumlipa huyo aliyemfanyia hilo tambiko la KUSOMBOKA.
Kilichonishngaza ni kwamba, hao wanaofanya hayo matambiko ni wanawake walioolewa au wanaume waliooa, na wake zao au waume zao wanajua kabisa kinachofanywa na wake au waume zao. Sina uhakika sana kama hilo tambiko la KUSOMBOKA badolipo, maana hizi kelele za UKIMWI huenda zimezima hili tambiko. Ila niliuliza, hivi kama muhusika, awe ni mwanamke au mwanaume aliyefiwa na mwenzi wake kutokana na huu ugonjwa wa UKIMWI, Je hawa jamaa wanaofanya hili tambiko watasalimika kweli? Nilijibiwa kuwa wanalindwa na mizimu, kwa hiyo sio rahisi kupata ukimwi….Nilishikwa na butwaa..
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba zipo mila pia zinamdhalilisha mwanamke na ninadhani hii ni mojawapo, na huenda iliasisiwa na wanaume ili kukidhi haja zao za kimwili.
Nimelizungumzia hili baada ya kuvutiwa na kile alichokisema kaka yangu Simon Mkodo Kitururu, na mimi nikaona si vibaya nikisimulia kile nilichokishuhudia kule Ukerewe, kama nilivyosimuliwa, iwapo yupo anayefahamu tofauti na maelezo yangu, basi namkaribisha hapa atuelezee kwa ufasaha….....NAWASILISHA
sielewi nini maana ya kufumania na kufumaniwa. nani mwenye hatimiliki? hivi nitakuwa njinga mapa nisubiri kumfumania wife? najifanya sioni kwana wanaondoka nayo?
ule mfano wako wa biblia wale mabwana walimshitaki mwanamke sio kwa sababu alifanya vibaya. walimkuta mama wa watu anafurahia mchezo akilialia kama zoba kwa furaha isiyoelezeka na wakamwonea wivu yule bwana wake na kutaka wote wawe wakosaji na kuamua kumtwanga stone.
mwisho wa yote wakamwacha na yesu pekee wakati ni jinsia tofauti kidogo hapo!!!! patamu pia na kuna mahali yesu alimfauta mama moja mtoni waliwa wawili.
haya mambo ya kuoana harafua mnaishi mbaali, unadhani kuna umhuhimu? we fanya tu mama sitojua mimi na sitaki kujua. anyway ni wivu tu kwamba ufurahie peke yako. hivi nini kinaumaga ukimfumania mwenzio? ule ujinga wote anaokufanyiaga sasa kaupeleka kwa wengine, ni wivu tu.
Sory nimecharaza
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote mliochangia mada hii, pamona na kwamba yapo mapya nimeyapata humu, kama vile hekaya ya kaka Kitururu ya wanawake kuoa wanawake wenzao ili kuwazalia watoto baada ya kutembea huko nje. Lakini iliyoniacha hoi ni ile hekaya ya kaka Ramson ya lile tambiko loa Kusomboka, hii ningeomba niiweke kibarazani kwangu ili nipate maoni toka kwa wadau mbali mbali kama kama bado hii mila inaendelea, naamini wenyeji wa Ukerewe wako kwenye nafasi nzuri kutuhabarisha juu ya hili.
Hata hivyo naomba nikiri kuwa bado wanawake tunayo safari ndefu kuelekea kuutokomeza huu mfumo dume, lakini naamini taratibu huenda wanaume watalitambua hili.
Nisingependa kufunga mjadala huu ili kuwapa nafasi wengine wenye maoni yao wawe huru kutuwekea hapa.
vilken bra fråga och ämne att ta upp..det e synd att man ska bedöma kvinnan hårdare när man egentligen eller rättare sagt båda har felat lika mycket...otrohet år otrohet oavsett kön...,
Det äe sant Nuru och ala vet att det finns inte fel och det finns int rätt. Som du sade båda har felat och det gör så ont oc se att allt det kvinnors fel.
Hey! Would you mind if I share your blog with my
twitter group? There's a lot of folks that I think would really appreciate your content. Please let me know. Many thanks
Also visit my page :: diet that works
Post a Comment