Monday, May 20, 2013

PALE INAPOKUWA EMBE MOJA KUGAWANA WATU WANNE....

 Leo tumetamani kweli EMBE ..lakini bei yake mmmh, embe moja shilingi 2300.. Basi tukaishia kununua moja ili angalao kupunguza hamu ya embe....
...na mwisho wake vikatokea vipande vinne..kila mtu akapunguza hamu ...iliishia kwenye ulimi tu hata shingoni haikufika..mweeeeeh maisha haya kaaaaziii kwelikweli..Nakumbuka januari nilikula embe mpaka kuziacha na pia kutupa sasa....mmmmhhh.

13 comments:

Anonymous said...

Da Yasinta huo ni ubahili kwa kweli! Yani mara moja kwa msimu kila mmoja akila lake sio mbaya..si mnafanya kazi ili mle tena mle vizuri tu. Ha unavyotuonyeshaga matunda ni muhimu sana mwilini wakati kumbe wewe mjanja unabahilia pesa unaishia kula matunda ya bei ndoogo! Haya maisha ya nje kazi sana, poleni na mrudi basi Bongi kwenye kuangua mwenyewe au bei sawasawa na dezooo! Ila sasa nje kila kitu ni ghali uki-convert kwa TShs. nadhani unaweza usinunue vyakula vya asili kwa msimu huku. Familia yako ni ndogo sana dada Yasinta mie nadhani mna-afford na Mr. Au na wewe ushakuwa bahili kama wazungu? mana wanaijua pesa hao acha kabisa. Sijapenda ulivyowatamaisha hao watoto next time mkinunua moja wapeni Camilla na Erick tu wagawane na nyie muishie kumeza mate tu!!!

Rachel Siwa said...

Linavutia saana. .

emuthree said...

Hicho kipande kimoja thamani yake ni mara dufu, ....kuliko hata ungelinunua maembe mia.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina hapo juu ! wewe hujui ni vipi kuishi hapa la sivyo usingeseama ...Ahsante
Kachiki..Si unaona!

emu-3 Ahsante sana ,,nakubaliana nawe ni angalao napata radha ya embe...fikiria ningenununua kumi na ynaniozea????...

Anonymous said...

Sikubalianai na kununua embe kumi kwani si niliandika manne tu! Kila mmoja na lake!!! hayo kumi ya kukuozea ungetaka mwenyewe. Watanzania wengi huwa hatujibu maswali au mada tunakurupuka tu! Asiye na jina hapo juu ameandika kweli ila nakubaliana na Yasinta kusema kuwa kuishi nje ni kugumu ila kwa kuwa familia ni ndogo kulikuwa hakuna tatizo kununua embe 4 once per year! Aliyeongeza maembe mia wala hata haileti mantiki hapa. Aliyesema umepata ladha ya embe anaweza kuwa sawa! Kwani nje maisha hamyamudu? Na kama hamyamudu milango iko wazi Tz. si mrudi tu....(Najua hapa majibu yatakuwa ya hasira sana) Kubaliana na hali hakuna haja ya kulalamika oh nimekula robo au nusu! just take it simple and do not try to compare it from Tanzania, mana kila kitu kina raha zake na shida zake. Hivyo hata hapa Sweden kuna raha zake na shida zake na Tz hivyo hivyo kuna raha zake na shida zake.

ray njau said...

Ukarimu upo moyoni mwa mtu na hakuna shule ya kufundisha ukarimu asilia!!!

Salehe Msanda said...

Usisikitike sana kuhusu kula embe moja watu wanne,umesahau kula kwa mduara enzi hizo,wakati tumetoka shule au shambani,watoto wa kike kula na mama,bibi,shangazi na watoto wa kiume kula pamoja na babu,baba,mjomba na umuhimu wake katika kujenga utamaduni wa kuwajali wengine na kuwa na mshikamano katika familia na jamii.
Kila la kheri

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu zangu wapendwa..Hapa si kwamba ni ubahili au nini. Nia yangu ilikuwa kuwaambia mara nyingine inaweza ikawa hivi yaaani katika maisha lazima kujifunza kuishi kwa kugawana/kile ulichonacho mgawia na mwenzako si lazima kiwe kikubwa...Nimependa huo mfano wa kaka Salehe kwa kweli ..Ahsanteni.

Anonymous said...

Leo tumetamani kweli EMBE ..lakini bei yake mmmh, embe moja shilingi 2300.. Basi tukaishia kununua moja ili angalao kupunguza hamu ya embe....

Anonymous said...

hADI ULIBADILI KWA TSHS. THEN UNASEMA KUISHI KWA KUGAWANA, KAMA NI HIVYO USINGEÁNDIKA BEI YA EMBE TENA ILIYOKUTIA UCHÚNGU KWENYE TSHS. MUNGU ATUSAIDIE KTK NCHI ZA UGENINI ILI TUWEZE KUISHI BILA KUBADILISHA PESA SEK TO TSHS KABLA HATUJAANZA KUNUNUA EMBE NK. MANA VINGINEVYO TUTAISHIA KUTAKA KUISHI ULAYA NA WAKATI WA KUNCH, DINNER NA B´REAKFAST TUNAENDA KULA TANZANIA, YANI KILA SIKU.

Yasinta Ngonyani said...

Ndiyo usiye na jina....bei ni hiyo lakini kwa kutaka kuwaamvbia ya kwamba Unaweza ukanunua embe moja na kuongezea na matunda mengine ndo maana ni kaandika hivyo...kujifunza matumizi ya pesa....

Anonymous said...

NASHUKURU DADA WA KUTUELIMISHA. NATUMAINI SIKUKUKWAZA.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na Jina! La hasha si unajua jina langu la utani KAPULYA..na kuuliza ni kujifunza..na kupata majibu ni kujifunze pia..Ahsante