Monday, June 6, 2016

VITU AMBAVYO WATOO WA SIKU HIZI WANAVIKOSA AMBAVYO NI TOFAUTI NA EZI ZETU YAANI NI HIVI:-

Nimetumiwa hii na msomaji wa MAISHA NA MAFANIKIO nikaona niweke hapa ili na wenzangu mkumbuke na labda kuna la kuongezea...KARIBUNI

1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapoondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua/kuzama, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukikaa na kusikiliza wazee/wakubwa wanapoongea utachapwa
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
28. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
29. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
30. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
31. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa
33.uki...................................utachapwa tu .....................endelea na wewe mengine
PANAPO MAJALIWA TUTASEMA TENA...PAMOJA DAIMA KAPULYA!

7 comments:

kasian wa mdunduwalo said...

Usipoenda kanisani au mskitini utachapwa

Anonymous said...

Ukichelewa shuleni utachapwa! By Salumu

Yasinta Ngonyani said...

Ukichelewa toka kuteka maji/kisimani utachapwa

NN Mhango said...

Ukiwa mchafu utachapwa
Ukifeli mtihani utachapwa
Ukisema uongo utachapwa
Ukimcheka kilema utachapwa
Uchekacheka hovyo utachapwa
Mbuzi au Ng'ombe uliowachunga wakivamia shamba la mtu utachapwa
Ukiomba fedha utachapwa
Ukiwakodolea macho watu wazima utachapwa
Ukipenda makamasi wakati unakula utachapwa
Ukiongea wakati unakula utachapwa
Ukipiga chafya bila kuzipa pua utachapwa
Ukila hovyo hovyo utachapwa
Ukiongea mambo ya kiutu uzima utachapwa
Ukiuliza mtoto anatoka wapi ukaambiwa hospitali ukabisha utachapwa
Ukiruka chakula utachapwa
Usipompokea mtu mzima mzigo utachapwa
Usipomsalimia mtu mzima utachapwa
Ukiwaita wazazi wako kwa majina yao utachapwa
Ukisukuma baiskeli ya mtu mzima ukaipanda utachapwa
Mkipewa lift kwenye gari la mtu ukaweka kishoka utachapwa tu
Ukimkata kijicho mwenzio wakati mnakula uchapwa
Ukikojoa kitandani utachapwa
Ukitoroka shule utachapwa
Ukirudi nyumbani sare za shule zimechafuka utachapwa
Ukicheza mchezo wa kijificha halafu ukakosa adabu utachapwa sana
Ukiwaadhibu wanyama au kukata miti hovyo hovyo utachapwa
Ukicheza rafu kwenye mpira wa miguu utachapwa
Ukiwachungulia wasichana utachapwa
Kwa ujumla ukikosa adabu utachapwa kweli kweli.
Huku Ulaya mtoto akifanya hayo anapewa candy au kuambiwa sweet usifanye hivyo.

Yasinta Ngonyani said...

Ukimega tonge kubwa la ugali unachapwa

Anonymous said...

Usinikumbushe ya kukojoa kitandani mwenzenu nilikula bakora za uhakika kutoka kwa mama halafu mzee anamalizia

ray njau said...

Naam ndiyo!!