Monday, June 20, 2016

SWALI KUTOKA KWA MSOMAJI WA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO

Habari za leo ndugu zanguni...nimetumiwa huu ujumbe kwa barua pepe yangu..nimeona ni kheri niweke hapa kibarazani ili tusaidiani maana kwenye wengi pana mengi. Karibu tumsaidie huyo dada................................................................

Habari,  mimi ni dada ninayeishi Iringa nina umri wa miaka 18 kwa bahati mbaya mpenzi wangu amenipa mimba na kutokana namna alivyo baba yangu Naamini akifahamu kwamba nina mimba ataniua Kwani mimi ni mwanafunzi.
Nimeongea na mchumba wangu tumekubaliana tukaitoe.
Hata hivyo bado najiuliza kama kutoa mimba  ni kitu sahihi? Na je, nifanyeje Kwani nipo kwenye njia panda.

3 comments:

John S said...

Nipo Yasinta.

Nimeliona hilo swali kutoka kwa msomaji wako wa Iringa.
Kuna mambo mengi sana ya kujadili hapo.
Dada ana miaka 18,
Ni mwanafunzi, nahisi atakuwa kidato cha tatu au cha nne,
Ana mimba ya miezi......(hajasema).
Kwanza tujiulize kwa nini amepata mimba?
Sababu zipo nyingi... Kutamani maisha ya juu, kushindwa kutawala tamaa za mwili, kujiingiza kwenye makundi mabaya kama ya ulevi wa pombe au utumiaji wa madawa ya kulevya.
Kuhusu baba kuhisi kwamba atamuua. Hiyo inaweza kuwa ni hofu kwa upande mmoja au ikawa kweli kwa upande mwingine.
Baba kutaka kumuua mtoto ni jambo ambalo hutokana na hasira dhidi ya binti huyu na kila mzazi yupo hivyo.

John S said...

Nimerudi tena
Kwa kweli inauma sana unapoingia gharama za kumsomesha mtoto halafu akaishia njiani eti kwa sababu ya mapenzi, mapenzi, mapenzi......

Ni afadhali afeli mtihani kuliko kupata ujauzito....

Ni afadhali nishindwe kumlipia ada kuliko kupata ujauzito...

Ni afadhali augue kuliko kupata ujauzito.

Inauma, inauma, inauma, usiombe itokee kwa mwanao.

Nini cha kumshauri?

Kutoa mimba siyo suluhu ya tatizo kwani safari moja huanzisha nyingine. Kama ataitoa hii mimba, uwezekano wa kushika mimba ya pili na ya tatu na ya nne...... ni mrahisi sana ambazo nazo atazitoa pia. Tayari atakuwa ni mzoefu wa kutoa mimba. Atakuwa ni mshauri mzuri kwa wanawake au wanafunzi wengine watakaotaka kutoa mimba. Hilo la kwanza.

Lakini la pili ni kwamba kutoa mimba inawezekana lakini ni pata potea, ni kufa na kupona, ni hamsini kwa hamsini, ni ama zangu ama zake.

Labda niseme hivi..... Kutoa mimba maana yake ni kifo. Ukitoa halafu ukasalimika ujue Mungu bado anakupenda sana, anakuhitaji sana, anataka umtumikie, amekupa nafasi nyingine, amekupendelea.

Lakini hata kama utasalimika, hata kama utapona, usidhani kwamba umepona kweli, bado kuna majanga yanakusubiri.....
Unaweza usizae tena kwani yawezekana ulikuwa na hilo yai moja tu, na wewe umelitoa.

Hebu niambie utajisikiaje? Umeolewa, upo na mumeo anayekupenda sana, upo na mumewo unayempenda sana, upo na mumeo mnayependana sana, halafu kila mwezi damu hiyooooo, kila mwezi damu hiyooooo..... mwaka mmoja, miwili, mitatu, minne, mitano.....
Mawifi wanaanza kukuzodoa, unajaza choo tu, unamfilisi kaka yao tu, kuzaa huzai, kwani umekuja kula hapa?
Aibu inakushuka mtoto wa kike, kisa ulitoa mimba. Janga lingine ni kwamba... Wakati unatoa mimba kizazi kinaweza kupasuka hali ambayo inaweza kupelekea kifo chako, na kama utasalimika italazimu kizazi kitolewe, utaishi bila kizazi, janga la kujitakia.

Kingine ni kwamba wakati wa kutoa mimba ule ukuta wa ndani wa kizazi unaweza kukwanguliwa wote na hivyo kupelekea kuwa na kovu kubwa hali ambayo mimba ikitungwa hukosa mahali pa kujishikiza. Hali hii ikitokea hata damu ya hedhi huwa haitoki.

Janga lingine ni uwezekano wa kupata kansa ya matiti. Utafiti unaonyesha kwamba asilimia karibu 75 ya saratani ya matiti husababishwa na utoaji wa mimba. Hapa anapaswa achague mtoto au kupata saratani.

Janga lingine ni kupata maambukizi yatokanayo na utoaji wa mimba usio salama. Maambukizi haya yanaweza yakaathiri sehemu za siri hasa shingo ya kizazi, kizazi chenyewe, mirija ya uzazi pamoja na mfuko wa mayai. Maambukizo haya yanaweza yakapelekea kupata saratani au ugumba na hata kifo.

Pia wakati wa kutoa mimba anaweza kutokwa na damu nyingi na hivyo kupata tatizo la upungufu wa damu.

Janga lingine ni kupata athari ya kisaikolojia. Kumbuka kutoa mimba ni jambo ambalo hatakuja alisahau kamwe maana linahisisha mwili na akili. Muda wote mpaka anaingia kaburini akili yake itakuwa inamkubusha jambo hili.
Lakini pia jambo hili litamuathiri kiroho maana ni tendo la kutoa uhai, ni tendo la mauaji.

Majanga ni mengi kwa kweli.

Kuhusu baba kutaka kumuua linaweza likatokea kweli au lisitokee....hakuna anayejua.

Nini kifanyike,?

Atafute watu wanaomheshimu baba yake ili wakaongee naye na kumuomba amsamehe binti kwani tayari jambo limeshatokea, tayari maji yameshamwagika. Kama njia hii itakwama akaripoti serikali za mitaa au polisi, na kama njia hii nayo ikikwama basi aende akakae kwa ndugu yoyote ambaye yupo mbali na baba.

Kubwa kuliko yote ni kwenda kumuona mchungaji au shehe ili akatubu kwa hili alilofanya pamoja na kumuomba kiongozi huyo wa dini ili akaongee na baba yake.

Yasinta Ngonyani said...

Utajisikia huzuni, hasira pale ikitokea mtu anaanza kuzungumzia suala la utoaji mimba pia unaweza kujikuta una hisia mbaya unapowaona watoto wadogo hasa wale watakaokuwa umri sawa na yule mtoto uliyemuua kwa kutoa mimba yake pia unaweza kujikuta hapendi kabisa kushika watoto au kuwagusa watoto wenye umri sawa na yule ambaye angekuwa mtoto wako.
Pia ufahamu kwamba madhara ya kutoa mimba ni zaidi ya unavyofikiria, kuna wanawake hupoteza maisha wakati wa kutoa mimba na wengine huugua kiasi cha kufa.
Inawezekana ni kweli baba yako atakasirika sana kusikia una mimba, pia naamini mzazi mwenye busara hawezi kumuua binti yake kwa kuwa ana mimba ya mjukuu wake. Naamini baba yako atakasirika na mwisho atakusamehe.
Inawezekana katika kutoa mimba ukapoteza kizazi au uzazi na siku moja ukaolewa na kushindwa kupata watoto na utajisikiaje utakapomwambia mume wako mpenzi kwamba huweza kupata mimba kwa kuwa ulimuua mtoto ambaye alikuwa tumboni mwako?
Inawezekana kwako kupata hiyo mimba ni bahati mbaya, hata hivyo mbele za Mungu huyo mtoto si bahati mbaya bali ni mpango wa Mungu kwamba azaliwe duniani na mtoto kama mtoto hana kosa ila wewe na mchumba wako.
Je, ingekuwaje kama wazazi wako nao wangekuua ungali tumboni mwa mama yako?
Jiulize ni namna gani wangekosa unavyocheka, unavyo tabasamu, unavyotoa machozi, unavyowapenda na vitu vyote vinavyowapa furaha ya maisha.
Achana kabisa na wazo la kutoa mimba.
Kumbuka kutoa mimba ni dhambi ya uuaji na hapa Tanzania pia ni kosa