Tuesday, June 28, 2016

KUMBUKUMBU ISIYOSAULIKA...NIMEKUMBUKA MIAKA ILE NILIPOKUWA BINTI MDOGO NA KAZI YA KUTWANGA MIHOGO ILI KUPATA UNGA WA UGALI KULE NYUMBANI LUNDO/NYASA!

Ama kweli tumetoka mbali...nakumbuka shughuli hizi kama vile ilikuwa jana. Ila mama yangu huko aliko asterehe kwa amani. Ahsante mama kwa kunifunza hizi kazi, hata kama ilikuwa kwa mikwala:-) maana nakumbuka nilikuwa nachukua mihogo na vifaa vingine na kwenda kwa rafiki zangu Oliva,,, na huko sasa nikitoka saa nane  nyumbani kurudi saa kumbi na mbili. Kisa kucheza mipira wa kudaka(rede...redesta)...mmmmhhh we acha tu...je nawe unakumbuka shughuli  yoyote ile....

2 comments:

NN Mhango said...

Nimeipenda sana hii. Huu ni ushahidi kuwa tusidharau mbegu; kwani hujui kitatoka nini. Wote tumetoka huko. Waliotudharau sasa wajidharau wenyewe.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango..yaani ww acha tu. Yaani kuna wakati inasikitisha sana unaposikia watu wengine jinsi wanavyodharau haya mambo wakati kuna watu ambao sio wazaliwa wanahusudu sana ...sasa sijui hii ni nini?