Sunday, March 30, 2014

HAPA NI LEO ASUBUHI NA HIKI NDICHO KILICHOKUWA CHAKULA CHANGU CHA ASUBUHI AMBACHO MIKONO YANGU ILITENGENEZA/KAZI YA MIKONO YANGU

 MAANDAZI
Nilikuwa katika mazoezi ya kukimbia na mara nikawaza MAANDAZI ...kufika nyumbani nikaanza kushughulika. Na hapa ni kikombe changu cha chai na maandazi . Karibuni tujumuike nasi:-) JUMAPILI NJEMA SANA KWA WOTE .

9 comments:

Manka said...

Jamani Dada yangu Yasinta umenitanisha sana,ndo nimeamka kufungua tu blog yako nakutana na mandazi.Naomba ukiwa na nafasi utuwekee recipe jamani.Asante.Jumapili njema.

Anonymous said...

Da Yasinta, maandazi matamu sana. tunataka na vitumbua pia. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Manka! nakwambia leo ilikuwa kama vile sikuu maana ni karibia mwaka nilikuwa nimekula maandazi, wote leo hapa nyumbani Jumapili imekuwa njema sana...Recipe yake wala si ngumu yaani jinsi mimi nifanyavyo ni:- Hamira nusu kijiko, bekingi poda kijiko kimoja za sukari, Sukari vijiko vitatu vya mezani(chakula), maji vuguvugu vikombe(dl) 2-3, Mafuta vijiko 3 vya mezani(chakula) na unga wa ngano vikombe (dl) 13.
Jinsi ya kufanya:- Changanya unga,sukari, hamira na beking poda kwenye bakuli. Halafu weka mafuta, baadaye tia maji vuguvugu kidogo kidogo mpka kinyunga kinakuwa laini. Sukuma kinyunga na kata vipande upendavyo kwa muundo upendao kwa mfano 2x4cm. acha vipande viumuke dakika 30. Na baadaye kaanga kwenye mafuta ambayo ni ya moto kutosha dakika kadha mpaka uonapo ni tayari....Karibu kujaribu:-)

Kaka Salumu! Nafurahi kusikia umeyapenda maandazi yangu..Na wala usikonde VITUMBUA VINAKUJA:-)

Anonymous said...

Haya maandazi yamenipita mie! Ila yanaonyesha ni matamu sana. Mie nina swali mafuta unayokandia huyachemishi kwanza?

Yasinta Ngonyani said...

Aise usiye na jina wa 3:34PM..pole sana ila bado yapo we njoo tu. Kwa Recipe yangu sichemshi ila najua wengine wanachemsha..hii ni recipe ya haraka/kijeshi ya Kapulya:-)

Manka said...

Yay...Asante sana Dada Yasinta nitajaribu.Ubarikiwe Dada yangu.

Yasinta Ngonyani said...

Manka! wala usiwe na shaka utaweza tu na utayafurahia ....ubarikiwe nawe pia. Kila la kheri.

Manka said...

Dada Yasinta jamani asante sana kwa recipe nilijaribu jana ni matamu ajabu..yaani ni miaka 2 tangu nile mandazi na hii ni mara yangu ya kwanza kuyapika asante sana,shem wako nae kayafurahia kweli.

Yasinta Ngonyani said...

Manka dadangu .....nimefurahi kusikia umefanikiwa na shem wangu kayafurahia. ..tupo pamoja