Monday, March 31, 2014

JUMATATU HII YA MWISHO WA MWEZI HUU WA TATU TUANGALIE JINSI YA KUSEMA NENO HABARI ZA KAZI KWA BAADHI YA MAKABILA YA TANZANIA.....

Kwa vile mimi ni MNGONI basi nimeona nianze na KINGONI, na baadhi ya lugha nafahamu na nyingine nimefanya utafiti kuwauliza marafiki na ndugu. Kwa hiyo kama na wewe una lugha/kabila unajua ni namna gani kusema HABARI ZA KAZI basi usisite kuniambia au tu kuandika hapa kibarazani nitashukuru.  KARIBU:-)
1. Kingoni husema:- HABARI za MAHENGU?
2. Kipogoro husema:- HABARIza MAHENGU? pia
3. Kibena husema :- KAMWENE za MADZENGO?
4. Kinyasa husema :- HABARI za NCHITO?
5. kinyakyusa husema.- TWAMBOMBO?
6. Kimatengo husema : HABARI ja MAHENGO?
7. Kijaluo husema : WOCHI MATOCHI?
8. Kinyamwezi/Kisukuma husema :- MAMILIMO?
9. Kichaga cha Marangu/Vunjo husema:- MBONYI TSA KIRUNDIO?
10.Kikurya husema :- AGH-EMEREMO?
11. Kigogo husema :- MILIMONYI?
NAWATAKIENI WOTE JUMATATU HII YA MWISHO YA MWEZI HUU WA TATU IWE NJEMA...

10 comments:

Anonymous said...

Kihaya ni Aga milimo?

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana usiye na jina kwa kabila hili la KIHAYA...NTAWEKA KATIKA KUMBUKUMBU:-)

sam mbogo said...

utafiti mzuri, salaamu nyingine unakuta zina fanana kwa baadhi ya makabila. kwaupande wa wasukuma /wanyamwezi tuna salam inayo fanana ila nilikuwa sina uhakika ka na wasukuma wana semama MAMILIMO. umepatia na mara nyingi husikia nduguzangu ama nyumbani wakisema VIHE ZYAMILIMO (vipi za kazi) jibu huwa NSOGA DUHU. ikiwa na maana ni nzuritu.

kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kaka Sam kwa mchango wako..na pia kwa kunipa wazo jingine la utafiti wa jinsi ya kuitikia...USENGWILI SANA...Jamani makabila yetu ni mazuri:-)

Rafikio wa hiari said...

sisi WaRuli wa Musoma tunasema - JA MILIMO?

Yasinta Ngonyani said...

Rafiki wa hiari! ahsante sana halafu sikujua kuna kabila la WaRuli. ......umeona hapa makabila yanavyofanana ? Raha kweli:-D

Ester Ulaya said...

Kifipa ni MWAOMBA

Yasinta Ngonyani said...

Aise hapa paduri mama Alvin...na KUOMBA inaitwaje?

Anonymous said...

Kwa kibena navyojua mimi, kama ulivyosema, lakini hapo hapo waweza tumia malimo au waweza tumia makassi, vile upendavyo na maana ni ile ile

Yasinta Ngonyani said...

Eeeehhh....ni kweli usiye na jina hii za makassi nimeitumia sana na kuisikia. Ahsante kunikumbusha.