Wednesday, March 12, 2014

SEHEMU FULANI TANZANIA :- TWENDEN WADOGO ZANGU TUTACHELEWA NAMBA....

Picha hii imenikumbusha enzi hizo:Amka, amka kumekucha x2  Twendeni shuleni.  au Panda, panda  panda, panda mlima panda  panda.....hapo mtu ulishaoga na sasa josho linakuvuja tena ...Duh  kaazi kwelikweli....Je? hapa ni mazingira ya wapi katika Tanzania yetu?

9 comments:

ray njau said...

Hizi ndizo changamoto za kwetu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Kumbe ni kwenu/kwetu hapa...Nimefurahi kusikia:-)

Emmanuel Mhagama said...

Picha hii inanikumbusha mbali sana. Hapo mkononi nilikuwa na dumu la maji au mzigo wa kuni au tita la nyasi. Mguuni hakuna kiatu, kaptula yangu ina vilaka kama viwili hivi, shati sina uhakika ni rangi gani. Nafika shuleni naambiwa nimechelewa namba. Nachapwa viboko kwa kuchelewa namba, viboko vinafumua vilaka vyangu na kunilazimu kwenda kushona upya. Hela ya kupeleka kwa fundi hakuna, naishia kushona kwa mkono. Mmmh!! Kama si Mungu aliyekuwa pamoja nasi, mwanadamu na aseme sasa.

Yasinta Ngonyani said...

Mlongo wa nene kaka Mhagama! Yaani umenikumbusha pia halafu hapo sasa si viboko tu hapana unapewa na adhabu ya kumwagilia maua au kesho yake uje na mzigo wa kuni..mweee....kaaazi kwelikweli..Ama kweli Mungu alikuwa nasi.

Interestedtips said...

duh...hii picha imenikumbusha kijijini kwetu nilikosoma

Yasinta Ngonyani said...

Mama Alvin! unaona mambo ya kale yalivyo na kumbukumbu...Kale wanafunzi walikuwa makini sana kuliko sasa. Maana sasa mambo ni mengi mno .....

Manka said...

Dah..Dada Yasinta hii picha imenikumbusha mbali sana hadi machozi yamenitoka.Jamani Tusisahau tulikotoka.

Yasinta Ngonyani said...

Manka! Naamini ni machozi ya furaha yalokutoka.....ama kweli tusisahau kabisa tulikotoka.

obat vimax said...

vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg