Tuesday, March 4, 2014

UTAMU WA VYAKULA VYA ASILI ..MABOGA, MAHINDI NA MAGIMBI

Asubuhi ya leo nimeamka huku nikiwa na hamu ya chakula hiki cha asubuhi. Maana huu ndio msimu wake hasa kwetu Songea maana ndio msimu wa mvua....mmmmhhh....halafu nikakumbuka ....

 ..mahindi jinsi mtu aendavyo tu shambani kukata/kuvunja mahindi na kwendajikono kuchoma au kuchemsha pamoja na maboga wakati huko nje mvua inanyesha..Ahhh nausikia utamu wake. Halafu nina kahadithi kamoja kuhusu mahindi  tulikuwa tunaitumia sana tulipokuwa wadogo inakwenda hivi:- Kila mtu anakuwa na muhindi, sasa wale wadogo huwa hawawezi kula basi wakubwa walikuwa wakiwaambia leta mimi nikutengenezee barabara ya kwenda ....anataja mji. Sasa yule mdogo aelewi anampa kumbe mwenzake yale mahindi atengenezayo barabara yote yanaingea tumboni ...Utoto bwana. Nilijaribu siku moja na wanangu, nilifanikiwa:-)...mmmhh ngoja niache  niwahi Madaba/matetereke

...maana ndiko nilikojifunza/onja mara ya kwanza Magimbi. Kwa hiyo leo nimekaa na kuota vyakula vingi. Natamani magimbi haya yawe mlo wangu wa mchana huu. Je kuna mlo ambao na wewe unautamani/hujala muda mrefu?

7 comments:

Anonymous said...

Umewahi kula mawungu?

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina ..Halafu nahisi kama vile wewe ni mngoni:-) Mavungu nimewahi kuyaona na nayajua ila sijawahi kula kwa kweli..ila kwa hisia zangu nahisi yananoga kama kumbukumbu vile:-)

Anonymous said...

Natamani senene, lakini samaki nchanga simtaki. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu ...kwelu humtaki samaki nchanga? Na sato je?

Anonymous said...

Yasinta samaki nchanga unanjua? kama humjui basi ni panya waleee ulioweka kama mboga siku moja hapa na ugali!!!!!!sijui nimepatia kaka Salum?

Yasinta Ngonyani said...

Oh...kumbe. duh, hizi lugha hizi...basi twende huko kwenye senene kaka Salumu au pia kama likungu lipo

Anonymous said...

Umepatia. Samaki nchanga ni yule panya alokuwa kwenye ugali katika picha moja iliyowekwa hapa! Sato wa MZA ni wanono mno! By Salumu.