Sunday, March 23, 2014

KUMBUKUMBU...LEO NI MIAKA MITATU TANGU MPENDWA WETU ASIFIWE NGONYANI ATUTOKE

ASIFIWE WAKATI WA UHAI WAKE
Ni vigumu kuisahau tarehe 23/3/ 2011, siku hii ndiyo tuliyompoteza mpendwa wetu Asifiwe Ngonyani. Na leo imetimia miaka mitatu tangu ndugu yetu mpendwa Asifiwe atutoke. MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA. AMINA.....TUTAKUKUMBUKA MILELE....

8 comments:

NN Mhango said...

Mungu ampe pumziko jema na kuwaliwazeni mliobakia. Amina.

Anonymous said...

Salamu za rambirambi kwa Ngonyani.God awabariki wote, Salamu
kutoka Ubelgiji Guido majaribio ya ndege katika Brussels! Pepe (thespecialist@skynet.be)

Rachel siwa Isaac said...

Pumzika kwa Amani....Asifiwe...

Nicky Mwangoka said...

Tunamwomba Mungu wetu mwenye huruma, amsamehe alipochafuka na aipokea roho yake pema Mbinguni. Amina. RIP Asifiwe Ngonyani

Anonymous said...

Mungu awatie nguvu katika kumbukumbu hii siku ya leo. Kweli mavumbini tutarudi.

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii kuwashukuruni wote mliopita hapa kwa kutufariji kwa kuacha maoni na pia wale waliopita njia. Mwenyezi Mungu awabariki sana kwa ushirikiano wenu na azidi kuwapa moyo. Ahsante sana kwa kuwa pamoja nasi siku hii ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Asifiwe.Tunakukumbuka daima.

Rafikio wa hiari said...

Nisamehe kutonesha kidonda chako tena rafiki yangu, lakini nimeonelea hii isinipite hivi hivi bila kumuombea kwa Mungu mdogo wetu Asifiwe aendelee kupumzika kwa amani.
Raha ya milele umpe Eee Bwana, na mwanga wa milele umuangazie. Astarehe kwa amani. Amina

Yasinta Ngonyani said...

Rafiki yangu wa hiari...ahsante sana ni faraja kubwa kuona upo nami kimaombi.