Thursday, March 27, 2014

PALE WAZAZI WANAPOAMUA KUWACHAGULIA WATOTO WAO WACHUMBA NA MWISHO WAKE MAISHA YANAPOKUWA MATESO...JE? NANI WA KULAUMIWA?

Mara nyingi sana nimekuwa nikifikiri hili jambo la kuchaGULIWA MCHUMBA. Nimekuwa nikijiuliza je ni nani ataishi na huyu mume au mke? Kwa bahati nzuri leo nimeamka nikiwa nikisoma mail zangu nimekutana na hii habari ambayo nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mfanikio...Jiunge nami na kisa hiki za huyu mdada.....
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kuna mwanadada mmoja ambaye ni miongoni mwa watu wasomi sana. Amemaliza chuo hapa Milimani. Wakati alipokuwa chuoni alibahatika kupata mchumba walikubaliana kuoana. Na walikuwa katika maelewano mazuri katika uchumba wao.

Baada ya uchumba huo kuendelea, aliamua kumpeleka kwa wazazi wake na kuwafahamisha kuwa mimi nimepata mtu ambaye naona atanifaa katika maisha  yangu. Baada ya kuwafahamisha, mama habari hiyo, mama wa dada huyo alikubaliana na wazo lake la kutaka kuolewa na huyo mchumba wake, lakini upande wa baba yake kulikuwa na shaka. Huyu binti alikuwa karibu sana na baba yake na aligundua kuwa baba yake hataki kukubaliana na wazo lake. Baada ya mazungumzo ya hapa na pale na baadaye mvulana yule kuondoka, binti alimfuata baba na kuzungumza naye na akasema kwa jinsi nilivyomuona huyo mvulana hakufai. Binti akamwambia si vizuri kumhukumu mtu kwa kumwangalia tu. Mimi nimekuwa naye kwa muda mrefu namfahamu vizuri sina shaka naye. Baba yake bado hakukubaliana na hilo lakini upenda wa mama yake hakukuwa na shida.

Uchumba uliendelea na yule mvulana akasema inaonyesha baba yake hataki kabisa, lakini nitaumia sana endeapo kama bado ataendelea kuwa na msimamo wake huo. Ni mtu ambaye nimekuzoea, tumeheshimiana sana. Yule binti akamwambia kila kitu kinawezekana na itawezekana tu.

Siku moja yule binti akiwa katika mizunguko yake ya hapa na pale akiwa mjini, alikutana na kaka mmoja akiwa katika mavazi ya kijeshi, na alikuwa na mwonekano mzuri sana, lakini cha kucshangaza yule kaka baada ya kumwona binti huyu aliduwaa. Baada ya kuduwaa kwa kipindi aliamua kumfuata binti na kumsalimia na kumwuliza kila kitu, na baadaye walianza kuwasiliana mawasiliano ya kawaida kabisa. Lakini mwanajeshi huyo alikuwa na mawazo tofauti, na ndipo siku moja akamweleza  kuwa angetamani siku moja awe mke wake. Yule binti akamwambia hapana, mimi tayari nina mtu wangu na tunaheshimiana sana, mwanajeshi akamwambia sawa. Kwa vile ni marafiki alimrudisha mpaka kwao, kumbe lengo lake yule kijana ni kutaka kujua binti anaishi wapi.
Na ndipo siku moja yule kijana aliamua kwenda peke yake nyumbani kwa wazazi wa binti huyo na kukutana na baba yake (Baba wa binti). Na ndipo alipozungumza ukweli wa kile alichokiona na lengo lake ni lipi. Na mzee aliweza kumdadisi kijana na kumweleza kila kitu. Kwa wakati huo yule binti pamoja na mama yake walikuwa hawapo na binti aliporudi akalezwa na baba yake kuwa kuna kijana mmoja alikuja yupo hivi na hivi aamenieleza kila kitu, nadhani huyo ndiye atakayekufaa. Binti alamwambia hapana, wewe ndiye umemwona na mimi itabidi nimwone. Baaye yule mjeshi akaja wakazungumza.
Baada ya mazungumzo marefu ya hapa na pale yule kijana mjeshi aliamua kuondoka, na kwa kuwa binti hakutaka kukofishana na baba yake aliamua kukubaliana na mawazo yake na baadaye wakamwita tena kijana huyo mjeshi. Baadaye taratibu zote za kuoana na mjeshi huyo zikafanyika, kisha binti huyo alienda kwa mchumba wake wa kwanza na kumweleza yote yaliyotokea na kumrudishia pete ya uchumba waliyovishana hapo awali. Kijana huyo alisikitika sana kwa uamuzi aliouchukua lakini hakuwa na jinsi aliamua kufuata shinikizo la baba yake. Hatimaye baadaye yule binti aliolewa na mwanajeshi na ndoa ilifungwa kanisani.
Baada ya ndoa tu, kilichotokea sasa hivi ni kwamba kosa kidogo tu anaambuliwa kipigo ambacho hajawahi kukipata, kiasi kwamba inampeleka kumkumbuka yule wa kwanza ambaye walikuwa wakiongea naye kwa utaratibu kabisa.
Ndipo baadaye binti (ambaye sasa ni mke wa mwanajeshi) akamfuata yule mchumba wake wa kwanza na kumweleza kila kinachotekea. Lakini kijana huyo aliajaribu kumweleza namana ya kufanya ili waendelee kuishi vizuri na mume wake na kuzidi kumwombea ili waishi vizuri.
Kwa wakati huu kijana huyo alikuwa bado hajaoa na anamweleza binti kuwa itachukua muda mrefu kwa sababu kwanza, itabidi nikusahau wewe, pili nikae chini  nitulie, tatu nianze upya. Hivyo itachukua muda sana.
Kikubwa zaidi ni kuwa binti hyuyo amekubali kuolewa na mwanajeshi kwa shinikizo la baba yake, lakini kinachoendelea ni kwamba kosa dogo tu anaambulia kipigo kisicho cha kawaida. Na kinachomuuma zaidi huyo dada ni kuwa walipotoka nje walienda sehemu ile ile ambayo walikuwa wakienda na mvulana yule wa kwanza na hivyo kuumia zaidi

Swali la Kapulya:- Je? huu kweli ni uungwanana? je? ungekuwa wewe ungmsikiliza baba au ungefuata jinsi moyo wako unavyopenda?

3 comments:

Anonymous said...

Nashukuru kwa simulizi hii. Ni kama nimesemwa mie kwa kiwango kikubwa.
Nimesoma, lakini sikuwa na choice nzuri katika mahusiano maana kila wakati niliangalia kufurahisha wazazi.

Kila niliyempenda hawakumpenda, matokeo yake, maisha yangu hata hayaeleweki. Ndoa niliolewa ili mradi. Ee Mungu nisaidie.

Miss FASILI YA 37/38

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu yangu Miss FASIHI YA 37/38! kwa kweli naweza kuungana nawe mkono kwa asilimia 80% katika hili. Wasichana wengi sana huolewa tu kwa vile wazazi wamempenda kijana. wanataka kuwafurahisha wazazi na wanajisahau wenyewe furaha yao itakuwaje..inasikitisha sana lakini ndivyo ilivyo.

Anonymous said...

Asante ndugu yangu. Hata sijapoa. Madhara yake yananiendesha puta hata leo.
Nilikuwa na sifa njema jamiini until things fell apart na sijaweza hadi kufanikiwa kuokota vipande vyote na kuviunganisha.

Huwa nasikitika sana sana sana. Kuna methali kikwetu (naamini karibu kila kabila ipo) kuwa ' kosea vyooote lakini sio ndoa'.
Basi ndio mie hapa. Yaliponifika ya kunifika , baada ya miaka 5 niliona nipumzike na hiyo taasisi nisije nikafa bure kwa kihoro. Hapo ndio nikawa nimezua uadui na kila pahali.

Jamiini naonekana mkosefu , Kanisani ( ambako nilikuwa nang'ara) naonekana kituko, familiani hawaachi kunisonta vidole.

Faraja yangu ni kama hivi, kwenye utandawazi, blogs najiangalizia wengine wanavyofurahia maisha haya ambayo tunayaishi mara moja tu, nasema hivi mie nimekosa nini? lakini nawaombea baraka wote ambao wamefanikiwa kufaidi maisha ya mapenzi na ndoa.

Ni mie Msikitikaji wa daima,
FASILI 37/38 (na sio FASIHI Yasinta- refer misamiati mipya tuliyoipata Bunge la Katiba. Fasili ni kama section au sub-section- nami nimejifunza punde tu. Nakupa homework utafute hizo fasili zinahusu nini basi hata utajua why I chose them to represent me. ) Pole kwa kijijarida