Sunday, October 6, 2013

NI JUMAPILI YA MWAKA C:LEO TUTEMBELE KIJIJINI KWETU LITUMBANDYÓSI/PAROKIANI

Kanisa hili nimesali mara nyingi sana ni KANISA LETU LA PAROKIA YA LITUMBANDYÓSI . NAWATAKIENI JUMAPILI NJMA SANA WOTE MTAKAOPITA HAPA.


4 comments:

Fadhy Mtanga said...

Safi sana da Yasinta. Nimefurahi kuona mandhari yakuvutia ya kanisa hilo. Nikiyaona majengo haya nakumbuka wakati nikisoma huko Kingonsera wilayani Mbinga. Uwe na Jumapili njema wewe na familia yako.

sam mbogo said...

Hakiyanani!!! unaweza kosea kutamka jina la kijiji hiki alikotoka dada Yasinta. hongera ,kanisa zuri sana pia umenikumbusha likizo yangu mwaka huu kijijini kwetu kanisa ni la matofali ya kuchoma,pia nilijisikia vizuri kusali kwa lugha yangu ya kiswahili,japo kuwa misa inachukuwa muda mrefu.ila safisana unapotoka ulaya nakwenda mojakwamoja kijijini kwako niraha ya pekee. kaka s

ray njau said...

1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.

2 Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;

3 Siku ile walinzi wa nyumba watakapotetema; Hapo wenye nguvu watakapojiinamisha; Na wasagao kukoma kwa kuwa ni haba; Na hao wachunguliao madirishani kutiwa giza;

4 Na milango kufungwa katika njia kuu; Sauti ya kinu itakapokuwa ni ndogo; Na mtu kusituka kwa sauti ya ndege; Nao binti za kuimba watapunguzwa;

5 Naam, wataogopa kilichoinuka Na vitisho vitakuwapo njiani; Na mlozi utachanua maua; Na panzi atakuwa ni mzigo mzito; Na pilipili hoho itapasuka; Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele, Nao waombolezao wazunguka njiani.

6 Kabla haijakatika kamba ya fedha; Au kuvunjwa bakuli la dhahabu; Au mtungi kuvunjika kisimani; Au gurudumu kuvunjika birikani;

7 Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.

8 Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili!

9 Walakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akatafuta-tafuta, akatunga mithali nyingi.

10 Huyo Mhubiri akatafuta-tafuta ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, yaani, maneno ya kweli.

11 Maneno yao wenye hekima huwa mfano wa michokoo; na kama misumari iliyogongomewa sana; ndivyo yalivyo maneno yao walio wakuu wa makusanyiko, ambayo yatoka kwa mchungaji mmoja.

12 Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.

13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya. _Mhubiri 12:1-12 ==================================
Majina ya vijiji vyetu ndivyo yalivyo.Mkolowony ndiyo kijijini kwetu.Asante Yasinta kwa salamu za Jumapili na kuonyesha jengo la ibada.Ibada ni jambo jema na kila mmoja wetu ana wajibu katika hilo maana ni wajibu wetu sote.Mashahidi wa Yehova wanatoa mwaliko wa kutmbelea majengo yao ya ibada katika ujirani wako (Jumba la Ufalme) kwa ajili ya mikutano mitano (ibada)ya kila juma na funzo la biblia bila malipo katika makazi yako.Kwa habari zaidi tembelea:www.jw.org

Yasinta Ngonyani said...

Mtani wa mimi Fadhy...Kwanza naseama karibu sana tena hapa maisha na mafanikio ni kipindi kimepita....Aise kumbe ulisemaga Caigo? Yaani sio wewe tu mimi napenda sana majengo ya aina hiyo. Naamini nawe ulikuwa na jumapili njema yangu iliishia kazini.

Kaka wa mimi Sam Mbogo...nyumbani ni nyumbani na hapa Litumba ni bonge la sehemu ..

Ray! Ahsante kwa mchango wako..na karibu sana Litumbandyósi..kutafuna karanga na korosho pia kula wali:-)